Zitto na Lissu wameruka kiunzi cha kwanza

Ado Shaibu

Member
Joined
Jul 3, 2010
Posts
99
Reaction score
111
ZITTO NA LISSU WAMERUKA KIUNZI CHA KWANZA

Na Ado Shaibu.

Zitto Kabwe, Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa ACT Wazalendo na Tundu Lissu, aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA wanao wajibu wa kipekee katika kuiondosha CCM madarakani kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Kama nilivyoeleza kwenye makala ya wiki iliyopita, serikali ya awamu ya tano imeshindwa kabisa kusimamia uchumi wa nchi na imekubuhu katika kuvunja haki za binadamu pengine kuliko kipindi kingine chochote katika historia ya Tanzania.

Kila kundi muhimu kwenye jamii (wakulima, wafanyakazi, wafanyabiashara, wavuvi, wanafunzi, Asasi za Kiraia, vyama vya siasa, wasanii n.k) kwa namna moja ama nyingine limeonja madhila yanayotokana na utawala wa kimabavu wa awamu ya tano.

Kinachohitajika ni uongozi madhubuti wa kuyaunganisha na kuyaongoza makundi yaliyoguswa na utawala wa awamu ya tano kuikabili na kuidondosha CCM.

Zitto na Lissu wamejijengea heshima na taswira ya kuwa vinara wa kuikabili serikali ya awamu ya tano. Wote wawili wamejenga ushawishi mkubwa kwenye jamii na kwa hakika wanastahili kuwa vinara wa kuyaunganisha makundi niliyoyataja kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Lakini, kabla ya kuutekeleza wajibu huo ambao nitaufafanua vizuri mbeleni, ni muhimu wote wawili wafahamu kuwa kuna vikwazo kadhaa vya kuvishinda. Vipo vikwazo binafsi, vikwazo vya kitaasisi na vikwazo vya dola.

Vikwazo Binafsi na vya Kitaasisi
Zitto na Lissu ni wanasisa wa muda mrefu na wanaofahamiana vyema. Mpango wowote unaowaleta pamoja ni lazima utambue kuwa wanasiasa hawa wamewahi kuhasimiana.

Wakiwa wote CHADEMA, Zitto akiwa Naibu Katibu Mkuu Bara na Lissu akiwa Mwanasheria Mkuu wa chama hicho, uhasama wao uliwahi kufikia kiwango cha juu. Hili lilionekana dhahiri kipindi cha Zitto Kabwe kuvuliwa uanachama wa CHADEMA. Kipindi hicho kilitawaliwa na matamshi ya kutoaminiana kutoka katika pande zote.

Kwa kuzingatia historia hii, si rahisi kwa mtu kuwaza kwamba Zitto na Lissu wanaweza kupatana na kufanya kazi pamoja kwenye uchaguzi mkuu 2020. Kila wazo hili linaposemwa, baadhi ya watu, ndani ya CCM na kwenye vyama vyao (CHADEMA na ACT Wazalendo) hukumbushia historia hii ya uhasama kuonesha ni mwujiza kwa Zitto na Lissu kupatana na kufanya kazi pamoja.

Kwa maoni yangu, watu wanaodhani kuwa Zitto na Lissu hawawezi kufanya kazi pamoja 2020 kwa kigezo cha historia ya uhasama na kutoaminiana baina yao na baina ya vyama vyao wameshindwa kusoma alama za nyakati. Siasa ni zao la matakwa ya nyakati. Wanamikakati katika medani ya siasa daima huumiza bongo kujiuliza kuhusu matakwa halisi ya wakati husika na kutafuta mbinu zinazoendana nao.

Historia ya dunia na hata ya hapa Tanzania imetufunza mifano chungutele ya namna matakwa ya nyakati yanavyoweza kuzika historia. Iwapo matakwa ya nyakati yanazalisha maslahi mapana, vidonda vya kihistoria huponywa kwa maridhiano na msamaha.

Ni mtu wa ajabu peke yake anayeweza kung'ang'ania kuwa mtumwa wa historia hata kama historia hiyo inamnufaisha adui na kukwaza ukombozi.

Jambo la kufurahisha, viongozi wa CHADEMA na ACT Wazalendo kwa kiasi fulani wameelewa matakwa ya wakati tulio nao. Kuna kila dalili kuwa viongozi wakuu wa vyama hivyo wameelewa kuwa tunaishi katika zama ambazo CCM ikipata upenyo itaumaliza kabisa mfumo wa vyama vingi ambao hivi sasa inaudhoofisha.

Pili, wameelewa kuwa kuikabili CCM ambayo inataka kuvizika vyama makini vya siasa, ni lazima kuzika tofauti za kihistoria na kufungua ukurasa mpya wa ushirikiano.

Kwa maoni yangu, kati ya mwaka 2017 na mwaka 2019, kazi kubwa imefanywa na viongozi wakuu wa CHADEMA na ACT Wazalendo kupunguza uhasama na tofauti za kihistoria baina ya vyama hivi viwili na viongozi wake.

Hapa nitataja mifano ya matukio makuu matano (5) ambayo kwa kweli ndio yaliyochangia kupunguza msuguano:

Tukio la Kwanza: Zitto "Punda" wa Mbowe?

Mwezi Februari 2017, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Paul Makonda alimtaja Mwenyekiti wa CHADEMA Ndugu Freeman Mbowe kuwa mmoja wa washukiwa wanaojihusisha na biashara ya madawa ya kulevya wanaopaswa kuhojiwa.

Zilikuwa tuhuma mbaya sana ambazo bila shaka zililenga kumchafua na kumvunjia heshima Ndugu Mbowe kama ilivyokuwa kwa wengine wengi wakati wa sakata hilo.

Zitto Kabwe alichukua hatua ya kipekee kwa kushiriki mkutano wa waandishi wa habari wa Mbowe na kuongea maneno mazito ya kumkingia kifua.

Kwanza, Zitto alisema yeye anafahamiana vizuri na Mbowe kwa muda mrefu na kama Mbowe angekuwa anauza madawa ya kulevya basi yeye Zitto angekuwa ndiye "punda" wa kumbebea madawa hayo.

Pili, aliweka bayana msimamo wake kuwa shambulio dhidi ya Mbowe na CHADEMA ni shambulio dhidi ya upinzani na yeye hatakubali kuona upinzani ukishambuliwa kisha akae kimya.

Tukio hili, ambalo Zitto liliwahi kumletea rabsha kiasi ndani ya chama kwa maoni kuwa alivuka mstari na kumtetea kupita kiasi Mbowe, lilianza kupanda mbegu ya kufungua ukurasa mpya wa maelewano baina ya marafiki hawa wawili waliopishana zamani (Mbowe na Zitto) na baina ya CHADEMA na ACT Wazalendo kwa upande mwingine.

Tukio la Pili: Lema Ndani ya Mkutano Mkuu wa ACT Wazalendo.

Tarehe 25 Machi 2017, ACT Wazalendo walifanya Mkutano Mkuu wa Kidemokrasia jijini Arusha. Tofauti na matarajio ya wengi, Mbunge wa Arusha Mjini Ndugu Godbless Lema alihudhuria na kuhutubia mkutano huo.

Kwenye hotuba yake, Lema alisema anamshukuru Rais Magufuli kwa sababu kwa utawala wake wa mabavu anaviunganisha vyama vya kisiasa (ambavyo vilikuwa na uhasama) na makundi mbalimbali ya kijamii pia kama vile viongozi wa dini, wafanyabiashara, Asasi za Kiraia, wakulima n.k

Tukio hili la Lema lina umuhimu wa kipekee kwa sababu, mosi, lilikuwa ndio tukio la kwanza la kiongozi mkubwa wa CHADEMA kuhudhuria na kuhutubia tukio kubwa la ACT Wazalendo.

Pili, mjumbe alioutoa Lema ulikuwa wa kipekee. Ulikuwa ni ujumbe wa kuviamsha vyama vya siasa kwamba vinapaswa kusahau ya nyuma na kuungana ili kumkabili Rais Magufuli na serikali yake ya CCM ambao wanalenga kuviangamiza.

Tukutane wiki ijayo kwa mifano matukio matatu yaliyobaki ambayo kwa hakika yamewafanya Zitto na Lissu kujengewa mazingira ya kushinda kikwazo cha kwanza cha uhasama wao binafsi na taasisi zao.
 
Unaandika habari za ACT_WAZALENDO au habari za zitto acha utumwa na fikra kijana
 
Mkuu naona unatumia zaidi propaganda ili upate kuimiliki hoja ya Tundu Lissu ya kushambuliwa kwake ktk tukio lile la kihayawani. Lkn pia kama vile ambavyo Yericko Nyerere ameelezea kwa kina, ACT Wazalendo mnajaribu kutumia ukaribu wa sasa wa Zitto na "learned brother' kwa habari ya kumtembelea mgonjwa mara tano, ukilinganisha na viongozi waandamizi wa CDM.

Mkuu, natambua hata TL na familia yake, wanatambua fika watu ambao wamejitoa muhanga ktk kuhangaika na madhila ambayo ameyapitia. Sidhani kama siasa inahitajika ktk mazingira kama haya.
 
Napokea sms nyingi kwamba nijibu mapigo kwa mashambulizi ninayofanyiwa na baadhi ya vijana wachanga katika siasa za kiswahili, lakini nataka kuwajibu wale wanaonishauri nijibu kwamba, huwa sijibu mashambulizi binafsi yanayolengwa kwangu, bali huwa najibu mashambulizi ya HOJA zangu tu. Siku wakijibu hoja zangu watapata bahati ya mtende nitawajibu kwa hoja pia.

Hoja zangu za tangu juzi ziko wazi na hazihitaji mishipa ya kichwa ikutoke kujibu, hoja hizi zilitokana na tweets mitandaoni za Ndugu na Kaka yangu Zitto Kabwe baada tu ya kufika Ubelgiji kumjulia hali Mwanasheria wa Chadema Wakili msomi Mh Tundu Lissu, na katika moja ya tweet alisema, Tanzania inawanasiasa wawili tu ndio watakaoleta mabadiliko, ambao yeye Zitto na Lissu. Tweet nyingine ikasema, "what a pair? What more Tanzanians need? The pair will Transform economy and reform criminal Justice system". Tweet hii ikaambatana na video akiwa na mh Lissu huko Ubelgiji na huku akitamka "we are coming"

Baada ya tweet hiyo nikamwambia haya,

Nanukuu.

"Huu ni uchonganishi na ufitinishi unaoufanya ndugu @zittokabwe ama unajua unachokifanya au hukijui unachokifanya,
Lengo lako ni kumgombanisha Mh Lissu na Chama chake, Na hili kwa siku kadhaaa umekuwa na juhudi za kumtenganisha Lissu na chama chake, juhudi za kubomoa chadema kwa staili ya kumremba huku ukimtoa kwenye mitazamo ya chama chake.

Hii tabia acha mara moja, acha haraka mkuu, upinzani nchini unahitaji umoja lakini umoja wenye nia ovu ya kuvunja chama kingine haukubaliki.
Chadema itatoa mgombea, Chadema itasimamisha mgombea wake, kushirikiana na vyama vingine ni suala la chama kama taasisi kukaa vikao na kuamua sio suala la mtu mmoja, Chadema ina mtaji mkubwa wa watu wenye sifa ya Kugombea urais, ukianza na Mwenyekiti Mbowe, Lissu, Nyalandu, Sumaye, na mifano mingine kedekede, hawa wanaweza kusimama bila kuhitaji msaada wa Ziito ikibidi,
Zitto tunakuhitaji kama mwanachama tunakuhitaji kama kiongozi, lakini hatukuhitaji utugawe kwa maneno ya aina hii, jenga chama chako, usibomoa chama chetu, Nenda muone mgonjwa lakini usianze kumtenganisha ama kumgombanisha na chama chake. Lissu ni Chadema, huwezi kumpenda Lissu kisha ukachukia chama chake.

Nyendo zako zinafahamika hatua kwa hatua, unaihitaji Chadema sawa na chadema inavyohitaji vyama vingine lakini mwenendo wako na mipango yako inaondoa uaminifu wako kwa wapinzani wenzako. Kumlisha uongo Lissu kwa maslahi yako kisiasa hii haitakubali.

Hii tweet yako ni kipimo muhimu sana na alama ya tabia yako kuwa haujabadilika licha ya kujutia kwako mara kadhaa. Nakushauri kijana mwenzangu, pitia njia sahihi ya chadema kufikia malengo yako na yetu ya Umoja wa Upinzani nchini.

Njia unayopita sio sahihi, si njia ya kutupeleka kwenye umoja wa Upinzani, bali ya kutugawa na kuinufaisha ccm juu ya mgawanyiko wetu. Njia sahihi ni moja tu, peleka maombi rasmi ya kichama mezani pa Chadema, chadema itayachakata na kukusikiliza ama kukubali ama kukataa, Hii lobbing yako ni ya kisaliti. Tutaizuia". Mwisho wa kunukuu.

Hoja za mjadala zilikuwa kama hivi hapo juu, hivyo wanaojaribu kujibu hoja hizi wazijibu sio kunitukana mimi, mie nilishatukanwa tangu nikianza balehe hadi leo nimezeeka na ndevu za shaba na situmii vumbi la kongo, hivyo hakuna tusi ambalo sijawahi kutukanwa na huwa sijibu kabisa,

Labda niwafafanulie kwanini niliamua kumshauri na kumkanya Zitto kwa kuweka hoja hapo juu. Kimsingi wote tunataka muungano ili kurahisisha kuiondoa ccm, lakini hoja inakuja tunaungana ili kufurahisha watu waone muungano au tunaungana na chama kilichomakini chenye commitment kama yetu Chadema?

Chama hicho ni kipi? TLP? Cuf? NCCR? ACT?
Hulka za wakuu wa vyama hivyo hapo juu zinachakatika?

Baada ya Uchaguzi Zitto ameleta maombi katika chama akitaka kurudi, chama hakikukurupuka kumpokea kikaamua kumtafakari kwanza, na baadae akageuza kibao kati ya 2016 hadi septemba 7, 2017 akawa anatushambulia kuliko tunavyoshambuliwa na ccm, Baada ya Lissu kushanbuliwa kwa risasi, akaleta maombi kwamba anaomba asije yeye bali aje kwanjia ya muungano kichama yaani ukawa mpya,

Maombi hayo yakasikilizwa katika kikao cha viongozi na wadau wa siasa kilichofanyika Hoteli ya Verde, na baadhi ya viongozi walioshiriki walimwambia Zitto kwamba maamuzi yanayohusu muungano au mashirikiano yanafanywa na vikao vikuu vya chama, hivyo wao kama wawakilishi wa chama hawana mamlaka ya kuamua hilo jambo, wakampa kazi Zitto kwamba kwa sasa kila chama kijenge chama chake na kueneza sera zake, muda wa uchaguzi ukifika kama kutakuwa na ulazima basi chama kupitia vikao vyake kitatafakari maombi hayo kwakutathimini kwa umakini faida na hasara za mashirikiano hayo,

Chama chetu kiko kwenye mchakamchaka wa kujenga mtandao wake, huku kikiwa bado hakijampa nafasi ya maombi bwana Zitto, na hili sio kwa bahati mbaya bali ni kutafakuri athari zake kwa sasa kulingana na malengo ya uanzishwaji wa chama hicho cha ACT na tabia ya kiongozi wake. Wakati maombi yake yakisubiri mjadala wa kichama kivikao, mwaka jana chama kikamkaribisha kama mshirika kwenye mambo madogomadogo hasa kufungua kesi ya kikatiba kupinga sheria ya vyama vya siasa, kikao kilichokalika makao ya chadema na ikaamuliwe iwe siri, ajabu kikao kikiwa kinaendelea ni zitto huyohuyo akatangaza mitandaoni juu ya kikao hicho na picha juu,

Chama kikaona huyu bado ni walewale, kikaamua kusubiri kidogo maombi yake, wakati subira hiyo ikiendelea, yeye akapanda ndege kwenda Ubelgiji na kujaribu kupeleka "uongo" flani ambao ungekubalika ungetugawa, akiwa palepale ubelgiji akijua kua ni uchonganishi, akaposti mitandaoni na kutangaza ushirikiano kuelekea 2020 akimtaja mwanachama wetu Lissu katika tweet zake jambo ambalo ni kuingilia mamlaka ya taasisi nyingine, amefanya haya kama njia ya kushinikiza maombi yake yajibiwe na chama, kwamba cc ikikaa isiamue tofauti na alichokitangaza mitandaoni na umma ukamshangilia..

Hivyo kitendo chochote cha sisi watiifu kwa chama tungekaa kimya ilikuwa ni kubaliki shinikizo la Zitto kwa chama chetu, maana chama kingeamua tofauti watu wengi ambao wanamwamini Zitto na ambao waliona tangazo lake la Muungano na video akiwa na Lissu wangetuona sisi CHADEMA hatufai. Ndio sababu ya sisi wanachama wa kawaida kumjibu zitto on the spot. Hivi ndivyo siasa zinavyotakiwa, matamanio yako yasiyumbishe maamuzi ya taasisi.

Kwa sasa Zito ana cheza michezo miwili kwa wakati mmoja, moja, Zitto anataka afanikiwe kuinasa Chadema/Lissu ili abebwe kisiasa bara angalau apate wabunge kadhaa na kisha ACT kuja kuwa chama kikuu cha upinzani akiwa na uhakika kuwa Zanzibar hakosi wabunge 20 hivi akijulimsha na viti maalumu basi atakuwa na wingi wa viti bungeni.

Pili ni kujaribu kuiblackmail ccm kwamba sasa Zitto anaunga na Chadema watakuwa na nguvu ya kuiondoa ccm, hivyo anaitongoza ccm ikae nae chini ifanye nae biashara ile aliyokuwa akifanya nayo utawala uliopita...hili anacheza kamari zaidi hana uhakika kulingana na misimamo ya mwenyekiti wa ccm.

Ni uamuzi wa Chadema kama itaamua itumike kuwa daraja la siasa za ACT au ilinde mtaji wa wanachama iliovuna vya kutosha toka Chadema ni msingi ambao hado leo inakadiriwa kusajiri wanachama milioni 36.
Kwa dalili hizi za Zitto ni wazi huyu hajabadilika bado ubinafsi ni mkubwa na unamtesa sana na njia sahihi kwa Chadema iachana na kushughulikia maombi yake, isimame kwa kutumia mtaji wake wa kisiasa, raslimali zake, na mgombea wake muhimu ambae dunia inamjua na itasimama nae daima. Tuendelee kumuombea Lissu wetu apone haraka.

Na Yericko Nyerere
 
Hivi kuna watu bado mnamwamini Zitto na huyo Lissu,hawa jamaa si wataiuza nchi yote pamoja na Watanzania wote,wajinga ndio waliwao,hawa jamaa wanajenga mazingira ya kupiga pesa ndefu kutoka kwa Miembe,Zitto alichukua chake mapema,bahati Miembe ukaishia kushika mkia kwenye ndoto za kukaa jengo la ufukweni
 
Mpaka hivi sasa hakuna baraka zozote zilizotoka Chadema makao makuu, na ni ishara inayoonyesha ni njaa ya mtu mmoja anayelazimisha mlo bila kujua mpishi amepika au ana nia ya kupika.

Hata wale vinara wa fujo wa Chadema, na wao pia wamefunga midomo hawataki kuhusishwa kabisa na hili swala. Cha msingi huu muungano ni mfu (dead on arrival), na hata hivyo, Kwa hivi sasa Lissu ana wakati mgumu kurudi kama allivyokuwa zamani. Kwasababu siasa hazina likizo, ukipwaya kidogo tu, ukirudi unakutana na kundi lingine la vijana ambao wana kasi kuliko wewe.
 
Mh Zitto haaminiki. Analindwa,hata Mkulu hawezi kumfikia Zitto. Yale "matusi" kwa mkulu, kashfa ya pesa za mifuko ya jamii..... Mh Zitto angekuwa ndani ananyea debe; lakini wapi. Wanasiasa maarufu wa upinzani hapa Tz wamechezea sana buti na virungu vya polisi,wamekaa ndani;lakini si Zitto. ACT Wazalendo si tishio kwa chama tawala. Tunahitaji upinzani makini,wenye hoja, sio mamluki na wajasiria siasa
 
Back
Top Bottom