Zitto na kamati yako lichunguzeni hili ili kuikoa tanesco | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto na kamati yako lichunguzeni hili ili kuikoa tanesco

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sammosses, Apr 26, 2012.

 1. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #1
  Apr 26, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Tetesi ambazo zinanisikitisha zinadhihirisha kufilisika kwa serikali yetu na kufa kwa shirika hili.Ikitokea shirika likashindwa kujiendesha na bado likazidi kuhujumiwa basi ujue kaburi lake liko wazi.Hali tete ndani ya shirika hili ambalo ni shirika mama kwa uchumi wetu inatishia uhai wa shirika hili.Kila mmoja anajitahidi kulinyonya kwa staili anayoweza ndo maana sisi kama watanzania wenye uchungu na nchi yetu tunahoji gharama hizi zisizo na mashiko ni za nini ndani shirika hili kama si kuliongezea mzigo na kuliua kabisa.

  Kitendo cha Tanesco kuipa tenda kampuni ya Quality group ku supply matairi na rim zake kwa magari yake aina ya Land cruiser model 78 ambayo ubavuni yameandikwa emergency yalifuata sheria ya manunuzi ya umma?Wote ni mashahidi tangu kuingia magari haya yana mwaka lakini rim na tairi zake zina badirishwa kwa magari yote bila magari hayo kuonyesha yanahitaji huduma hiyo kwa sasa.Mbaya zaidi hizo rim zinazo wekwa kwa sasa hazikidhi mahitaji ya barabara zetu nikimaanisha rim za aluminium zinawezaje kuhimili hali ya barabara zetu huko vijiji inakopita miundo mbinu ya umeme.Ifike hatua tuwe wazalendo na mali za umma vinginevyo nchi ina elekea kubaya

  Inakadiriwa sportage rim moja yenye material ya aluminium gharama yake inasimamia si chini ya Tshs 780,000/- bila tairi,na tairi ambayo ni tubeless inasimamia si chini ya 560,000/-,hebu fikiria kwa mkoa mmoja wenye gari ambazo si chini ya nane na kila gari lina matairi yasiyo pungua matano gharama yake ni kiasi gani.Kitaalamu rim ya gari hizi huchukua si chini ya miaka miwili hadi mitatu,na hii inategemea kama wheel balance haiko sawa.Tuna hoji kulikuwa na sababu gani kwa Tanesco kufanya madudu haya bila kuyakagua kwanza magari yao na kufuata ushauri wa kitaalamu.

  Kitendo kignine ni cha rim zilizotlewa kuchukuliwa na hao Quality group kwa shughuli zingine maalumu,kwa hali kama hii tunaitaka kamati yako kuchunguza kwa makini tetesi hizi kwani lengo ni kuinusuru nchi yetu kuondoka na gonjwa hili ufisadi ulio likumba
   
 2. h

  hebronipyana JF-Expert Member

  #2
  Apr 26, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 261
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Bongo ni zaidi ya uijuavyo.
   
Loading...