Zitto na Jafo, saidieni wanachama wa NSSF

Zitto na Jafo, saidieni wanachama wa NSSF

MPadmire

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2006
Posts
3,956
Reaction score
3,245
Zito na Jafo ni baadhi ya wabunge waliojitolea kutetea masilahi ya fao la kujitoa la wanachama wa mifuko ya Jamii.

Hili tatizo la NSSF inabidi liangaliwe kwa Jicho la Tatu. NSSF inachangiwa kwa asilimia kubwa na wafanyakazi wa Sekta binafsi ambao ni Ngumu kupata dhamana na mkopo katika Taasisi za Fedha.

Ni ajabu kusema mtu afanye kazi mpaka afikishe umri wa kustaafu ndipo ajenge nyumba ya Kuishi.... Maisha bora hapa yako wapi?

Kama mtu ana amana katika NSSF inayofikia millioni 10 mpaka 20? Je NSSF haiwezi kumdhamini akope benki direct?

Mikopo ya NSSF kupitia SACCOS wanayotangaza ni migumu sana almost impossible.

Hili ni Tatizo la mifuko hii kutawaliwa na watu ambao si wafanyakazi, watendaji wa hii mifuko hawatokani na wafanyakazi... Hawajui machungu ya wafanyakazi.

Hili ni Suala la Kitaifa, halina dini wala itikadi ya kisiasa. Huku NSSF kuna wana CCM wanaumia, kuna wana ACT wanaumia, Kuna wana CUF wanaumia, TLP n.k

Kwa hiyo tunaomba kusikia sauti za Wanasiasa katika hili.
 

kapumbiti kapumye - Nimetaja baadhi ya vyama, nikaweka n.k kumbuka viko vyama zaidi ya 15.....So wacha tujikite katika hii kero ya NSSF. Lazima wadau mbalimbali wapaze sauti NSSF Wasikie
 
Jafu na zito?

Hapo ndo wafanyakazi wa sekta binafsi wanapo dondokea pua siku zote pasipo kujua!

mafao ya wafanyakazi ni hoja nzito ambayo inatakiwa ikae mbali na mibunge 'mi-opportunistics' kwa ajili ya unyeti wake, ukizingatia kuwa siri kali hii ya manyang'au inainyemelea kuifilisi na kujimilikisha minoti ya hiyo mifuko,


kwani ile hoja binafsi ya jafu kuhusu ule msaada iliishia wapi kama haikuwa 'changa la macho' a.k.a 'mazingaombwe'

chezeni na moto mwisho wake mtaisoma, walimu tayari wameisha lizwaa...
 
hili ni janga jingine na aina tofauti ya unyanyasaji wa wafanyakazi, haiingii akilin nichangie miaka 15 kwa maana ya miezi 180, eti ikitokea nakosa kazi kabla ya umri wa kustaafu nirudishiwe tu michango yangu na sipo ktk pensionable scheme zao.
Hili suala la ajabu sana kwani kama mwingine akipata kazi na akaweza kuchangia miaka hiyo 15 na akawa amefikisha umri wa kustaafu yeye anapatiwa sehemu ya michango yake (wanasema 24% ya michango yake yote), na kiasi kinachobaki kigawanywe na akipate ktk malipo ya kila mwezi. Hili nalo halipo sawa kwa kweli.
Nategemea wadau wengi watachangia uzi huu kwani una hatima ya maisha yetu wazee tarajari, ukizingatia hadi sasa tunalipa kodi kikamilifu, iweje tupatiwe 24% tu ya makusanyo yetu ya mbele, ukizingatia na hali ya mishahara yetu ilivyo, angalau hata iwe 50% kwa maana ya michango yangu yote na ya mwajili na sehemu ya kodi yangu inisaidie ktk kupata ile mfumo wa kila mwezi yaani pension.

Watajwa wasaidie katika haya:
A: NSSF washauriwe wadhamini au watoe mikopo kwa wanachamna wao kwa masharti nafuu (binafsi na siyo SACCOS)
B: NNSF waangalie hizi tofauti kwanini wote wachangie miezi 180, halafu mwingine awe pensionable na mwingine hapana?
 
Hii ishu Niko nyima ya Zitto kabisa. Hata maandamano nitashiriki
 
Why put your life on the hands of politicians? It gets even worse if you surrender your life to politicians who are opportunistic in nature, corrupt or not trustworthy....

This is your battle as a member who is contributing in these pension funds..You need to fight hard....Where are the so called 'trade unions'? What are they doing?
 
Zitto mwenyewe kachota mamilioni fedha za wafanyakazi kutoka nssf na kupeleka kwenye kampuni yake ya wasanii.
 
Asanteni wachangiaji, hii imethibitisha kuwa NSSF kuna shida. Kama NSSF ni wasikivu, waje hapa wasikilize wanachama wao. NSSF msipuuze kilio cha watanzania. Mr. NSSF uko wapi?

Watanzania tuungane kudai haki, haki haiombwi na wala haki haigaiwi kama pipi
 
Kwanini watumishi wasipate mikopo ya riba nafuu kupitia kwenye mishara yao benk wanatumaliza kwa riba nssf imebaki kukopesha wakumbwa tu
 
Nchi imekosa dira

Mpaka Muhimbili Hospitali kuu hakuna dawa, kisa eti wanadaiwa na MSD.

Wagonjwa wangapi watakufa?
 
Wanataka kujenga daraja wakati wenye NSSF wanakosa mikopo?
Wenye NSSF ni Nani? DAU ndo mwenye NSSF ama wanachama?
 
Jamani JF Members, na wasomaji wote Nini muafaka wa majadiliano kuhusu mada mbalimbali na kero kama mikopo ya SaCcos ya kisanii ya NSSF!
 
Back
Top Bottom