Nilitegemea baada ya mgombea urais wa JMT Tundu Lissu kupitia CHADEMA kumuunga mkono mgombea urais wa Zanzibar kupitia ACT Wazalendo, Seif Sharif Hamad, ungejitokeza na kupongeza na pengine kushauri Membe naye amuunge mkono mgombea wa CHADEMA, hujafanya hivyo, labda pengine ni mapema mno bado unaangalia upepo au bado kuna mazungumzo yanaendelea.
Kuna tetesi kuwa huenda unausaliti upinzani kwa kulazimisha Membe agombee ili kuzigawa kura za upinzani, hilo sina uhakika, na kuna wengine wanasema bifu lako na CHADEMA bado halijaisha, kuna wengine nao wanasema ACT Wazalendo ni tawi la CCM wamemleta Membe huko kwa lengo maalumu. Hayo yote nakuachia wewe na wasomaji wataamua.
Nia yangu hasa ni kujua wewe binafsi kama kiongozi mkuu wa chama, kwa vile huko nyuma umeonekana kuwa mstari wa mbele kuvishauri vyama vya upinzani kushirikiana au kuungana, una msimamo gani hasa baada ya jana Membe kusema ‘HATOKI MTU HAPA’.