Zitto, Lema, Mwigamba na Maamuzi ya Kamati Kuu Chadema

Filipo Lubua

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2011
Posts
339
Reaction score
579
Ni dhahiri kwamba yanayotokea leo, ya Zitto na Kitila Mkumbo kusimamishwa nafasi zao yalishajionyesha wiki chache zilizopita. Chadema wametekeleza maamuzi haya zikiwa ni siku chache tu baada ya Zitto na Lema kushambuliana waziwazi katika mitandao huku wakiitana wasaliti, wachanga katika siasa na majina mengine mengi.

Ingekuwa vyema, kabla ya Kamati Kuu ya Chadema kutoa maamuzi dhidi ya tuhuma mpya za Zitto, wangetakiwa watujulishe maamuzi yao juu ya Samsoni Mwigamba ambaye alituhumiwa kuandika habari za uzushi mitandaoni. Vilevile nadhani ingekuwa vyema suala la Zitto na Lema kutifuana huku mitandaoni lingejadiliwa kwanza. Leo ni kama hoja ya Mwigamba na mitandao, Zitto na Lema mitandaoni, zote zimefukiwa ardhini na kuinua hoja nyingine mpya ya Waraka wa Siri.

Ni wazi kuwa, hata kuja kwa Lema na kutoa hoja kuwa Zitto ni msaliti, kulikuwa kunaonyesha kuwa kuna jambo lingine zito lilikuwa likifuata. Ujasiri wa Lema kumwandika aliyekuwa Naibu Katibu wake kwa lugha ya vijembe kiasi kile ulikuwa ni ujasiri ulioonyesha kuwa kweli siku za Zitto zilikuwa zikihesabika chamani. Si vyema, kwa Chama makini kama Chadema, chama chenye intelijensia ya hali ya juu, kuacha mambo yaende kama Lema alivyoyapeleka. Vikao halali vya chama navitumike kuwasuta viongozi wasaliti badala ya mitandao kutumika.

Hata hivyo, niwapongeze Kamati Kuu ya Chadema kwa kuchukua maamuzi haya muhimu na muafaka ya kumsimamisha Zitto nafasi yake. Zitto tangu zamani, tangu apate umaarufu katika siasa za Bongo, amekuwa mpinga mapinduzi ya kichama, huku akiendekeza siasa binafsi, za kujiletea umaarufu binafsi. Zitto alifanya siasa za upinzani ndani ya chama chake na kujitafutia wafuasi kwa nguvu. Zitto amehusishwa sana katika mkanda wa Lwakatare na Saed Kubenea, Zitto amehusishwa sana na akina Mwampamba na Juliana ambao wamekuwa wakiutukana uongozi, Zitto amehusishwa sana na njama mbalimbali akishirikiana na Mwigulu Nchemba. Mambo mengi yalishaonyesha tangu zamani jinsi Zitto alivyokuwa akitumiwa na vigogo wa serikali na CCM. Ni wazi kuwa maamuzi yaliyochukuliwa dhidi yake ni sahihi.

Mwisho kabisa, nimtakie Zitto mapumziko mema ya Kisiasa na nimkumbushe tu kuwa aliyoyafanya ndiyo yaleyale aliyoyafanya rafiki yake mkubwa, Kafulila ndani ya NCCR Mageuzi. Leo kwenye siasa za Tanzania, Kafulila ameshafulia na nguvu ya awali alokuwa nayo imepotea. Kwa Dk. Kitila Mkumbo, wewe sina la kukuambia ila nadhani umejifunza kuwa siasa za kutumiwa, hasa kwa msomi kama wewe, mwisho wake ni aibu na fedheha.

Kwa Kamanda Godbless Lema, nakushauri uache siasa za magomvi na mashindano ambayo yanaweza kukipasua chama. Mambo yote yafuate utaratibu mzuri wa vikao vya Chama, na sisi wanancho tutawaunga mkono.
 
Hapa ndo utaona kuwa ccm ni chama kikubwa sana hakunaga vitu kama hivi vya kutimuana Naibu Katibu Mkuu; khaa anasimamishwa khaaaa
 
Filipo Lubua nimeipenda hiyo. Zitto na Lema walionesha uchanga sana kubwatukiana kwenye mitandao. Lakini pia msaliti anapaswa KIFO.
 
Last edited by a moderator:
Hapa ndo utaona kuwa ccm ni chama kikubwa sana hakunaga vitu kama hivi vya kutimuana Naibu Katibu Mkuu; khaa anasimamishwa khaaaa
Sema hawana uwezo wa kuchukua maamuzi magumu. Kwahiyo hii si taarifa ya kujivunia kwa wao kushindwa kutekeleza maamuzi magumu.
 
Mawazo finyu sana haya,

Wewe kama unadhan zitto alikua anapambana na chadema umepotoka sana,zitto anapambana na wale wanaohujumu taifa hili,so hata kama akifukuzwa chadema ili wachaga waendelee kushika hatamu bado ataendelea kupigania haki hizo hata nje ya hapo,

HARAKATI NI POPOTE PALE.TAMBUA HILO...
 
Kweli, kule hata uwe jangili, ubake denti na kumpa virusi unapeta tu...
 
Mawazo finyu sana haya,

Wewe kama unadhan zitto alikua anapambana na chadema umepotoka sana,zitto anapambana na wale wanaohujumu taifa hili,so hata kama akifukuzwa chadema ili wachaga waendelee kushika hatamu bado ataendelea kupigania haki hizo hata nje ya hapo,

HARAKATI NI POPOTE PALE.TAMBUA HILO...

Ulipiga kelele GESI HAITOKIII, CCM WANATUNYANYASA WANA KUSINI umeshughulikiwa umebadilika rangi. mnafiki kama wanafiki wengine.
Aione kiwatengu ..
 
Last edited by a moderator:
Subirin impact yake,bila zitto chada isingekuwa na ndoto za kuionja Ikulu mwaka 2025 hakika nawaambien sasa ndo sku na miaka inasogea mbele CDM ukulu mpaka 2035 hv
 
Sema hawana uwezo wa kuchukua maamuzi magumu. Kwahiyo hii si taarifa ya kujivunia kwa wao kushindwa kutekeleza maamuzi magumu.

jamani haya mambo yaliaza kwa wanachadema kurushiana maneno kupitia kwenye mitadao. baadaye chadema ikawa inatoa habari nyingi na ambazo siyo zi kiuugwana kwa zitto kuhusu chadema. baada ya hapo chadema kwa uzembe wake kupitia wanachama limbukeni ikaaza kuudanganya wawatanzania kuwa hayo yalikuwa yatokea dani ya chadema ni mpango ya ccm. sasa basi mimi nauliza kuwa hivi yaliyotokea jana ambayo mimi nayaona kama yametikisa ramani nzima yatanzania ccm nayenyewe ulikuwemo kwenye maamuzi yalitokea? naomba wanachadema munijibu.
 
Mawazo finyu sana haya,

Wewe kama unadhan zitto alikua anapambana na chadema umepotoka sana,zitto anapambana na wale wanaohujumu taifa hili,so hata kama akifukuzwa chadema ili wachaga waendelee kushika hatamu bado ataendelea kupigania haki hizo hata nje ya hapo,

HARAKATI NI POPOTE PALE.TAMBUA HILO...

Taifa la kufikirika nini. Taifa gani alipiganie Zito? msiwape watu sifa wasizokuwa nazo
 
HIVI WATU WASAHAULIFI HIVI?
HAWAKUMBUKI HILI BALAA LILIANZA BAADA YA MWINGAMBA KUPOKONYA LAPTOP ?NA HAKIKA LEMA ALIKUW ANA CONFO KWA KUWA ALISHASOMA HUO WARAKA NA MENGINE MENGI KUTOKA KWENYE LAPTOP YA MWIGAMBA. sasa kipi mlichokisahau hapa?
 
Naumia kumpoteza Zitto,, but sio kwamba alikuwa perfect saaana!! Suala la kutaka madaraka kawake halikuwa geni..Lakini kwa kutaka kupandikiza ukabila na udini hapo amechemkaaaa!!!Pointi zake zingekuwa kwahoja nyingine tungeweza kumuunga mkono sana lakini kwa kuingiza swuala la udini na ukabiladirectly,,kijana kachafua hali ya hewa..ZITTO KAONDOKA LAKINI CHADEMA ITABAKI KUWA CHADEMA
 
Ili mti wowote uendelee kuzaa matunda, ni budi ku-prune matawi yale yasiyozaa pamoja na mapandikizi!! Hongera CHADEMA.
 
Hakuna cha CCM kuwa chama kikubwa zaidi nikulinda maslah ya wakubwa wa chama na si chama. Kwani umesahau ya Katibu wa Chama aliyepo yaliyomkuta siku za nyuma au huna historia nzuri na chama... Au unataka kusifia historia za chama kumpoteza Kolimba na wenzeka mpaka kuzimu??
 
Ni dhahiri kwamba yanayotokea leo, ya Zitto na Kitila Mkumbo kusimamishwa nafasi zao yalishajionyesha wiki chache zilizopita. Chadema wametekeleza maamuzi haya zikiwa ni siku chache tu baada ya Zitto na Lema kushambuliana waziwazi katika mitandao huku wakiitana wasaliti, wachanga katika siasa na majina mengine mengi.

Ingekuwa vyema, kabla ya Kamati Kuu ya Chadema kutoa maamuzi dhidi ya tuhuma mpya za Zitto, wangetakiwa watujulishe maamuzi yao juu ya Samsoni Mwigamba ambaye alituhumiwa kuandika habari za uzushi mitandaoni. Vilevile nadhani ingekuwa vyema suala la Zitto na Lema kutifuana huku mitandaoni lingejadiliwa kwanza. Leo ni kama hoja ya Mwigamba na mitandao, Zitto na Lema mitandaoni, zote zimefukiwa ardhini na kuinua hoja nyingine mpya ya Waraka wa Siri.

Ni wazi kuwa, hata kuja kwa Lema na kutoa hoja kuwa Zitto ni msaliti, kulikuwa kunaonyesha kuwa kuna jambo lingine zito lilikuwa likifuata. Ujasiri wa Lema kumwandika aliyekuwa Naibu Katibu wake kwa lugha ya vijembe kiasi kile ulikuwa ni ujasiri ulioonyesha kuwa kweli siku za Zitto zilikuwa zikihesabika chamani. Si vyema, kwa Chama makini kama Chadema, chama chenye intelijensia ya hali ya juu, kuacha mambo yaende kama Lema alivyoyapeleka. Vikao halali vya chama navitumike kuwasuta viongozi wasaliti badala ya mitandao kutumika.

Hata hivyo, niwapongeze Kamati Kuu ya Chadema kwa kuchukua maamuzi haya muhimu na muafaka ya kumsimamisha Zitto nafasi yake. Zitto tangu zamani, tangu apate umaarufu katika siasa za Bongo, amekuwa mpinga mapinduzi ya kichama, huku akiendekeza siasa binafsi, za kujiletea umaarufu binafsi. Zitto alifanya siasa za upinzani ndani ya chama chake na kujitafutia wafuasi kwa nguvu. Zitto amehusishwa sana katika mkanda wa Lwakatare na Saed Kubenea, Zitto amehusishwa sana na akina Mwampamba na Juliana ambao wamekuwa wakiutukana uongozi, Zitto amehusishwa sana na njama mbalimbali akishirikiana na Mwigulu Nchemba. Mambo mengi yalishaonyesha tangu zamani jinsi Zitto alivyokuwa akitumiwa na vigogo wa serikali na CCM. Ni wazi kuwa maamuzi yaliyochukuliwa dhidi yake ni sahihi.

Mwisho kabisa, nimtakie Zitto mapumziko mema ya Kisiasa na nimkumbushe tu kuwa aliyoyafanya ndiyo yaleyale aliyoyafanya rafiki yake mkubwa, Kafulila ndani ya NCCR Mageuzi. Leo kwenye siasa za Tanzania, Kafulila ameshafulia na nguvu ya awali alokuwa nayo imepotea. Kwa Dk. Kitila Mkumbo, wewe sina la kukuambia ila nadhani umejifunza kuwa siasa za kutumiwa, hasa kwa msomi kama wewe, mwisho wake ni aibu na fedheha.

Kwa Kamanda Godbless Lema, nakushauri uache siasa za magomvi na mashindano ambayo yanaweza kukipasua chama. Mambo yote yafuate utaratibu mzuri wa vikao vya Chama, na sisi wanancho tutawaunga mkono.
Mkuu kuwa mkweli tayari Chadema kimesambaratika.
 
Well said mkuu,japo yataongewa mengi sana juu ya haya yaliyotokea,kwa upande wangu nimefurahi sana,ila sikupendezewa kwa mwalimu wangu Dr.KITILA kufuata MKUMBO wa akili ndogo yenye tamaa kama ya hawa wasaliti,ni bora tuendelee kuwa chama pinzani hata baada ya 2015,kuliko kukaa na wasaliti.
 
For sure usaliti wa Zitto watu waliuona siku nyingi sema walimstahi. Tunamshukuru kwa yote mazuri yote ambayo ameitendea nchi hii nayale anayokusudia kuyatenda.. Kama yeye nimzalendo wa kweli tunategemea ataendelea kutenda mazuri kwa kwa Faida ya Watz wote bila kujali dini wala ukabila!!!
 
Back
Top Bottom