Zitto kwanini unapenda kupotosha umma at your expense?

Stroke

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
36,981
45,903
nimekua nikifuatilia hoja zinazoibuliwa na mwanasiasa wa Upinzani kupitia ACT nyingi ya hizo zinabase katika Taarifa zisizo sahihi hivyo kupotosha umma.

kwakua Zito tayari ana base ya followers ni rahisi sana ku consume wrong information ambazo ipo siku zitazua taharuki.

Zito akijua kabisa kwamba sio kweli: amepotosha Tafsiri ya mkataba wa Jumuia ya Afrika Mashariki kuhusiana na mgawanyo wa uwakilishi wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki.

Zito akijua kabisa kuwa sio kweli: alipotosha hali ya chakula hapa nchini kwa kutoa Taarifa za njaa ilhali hakuna hali kama hiyo hapa nchini.

Taarifa za zito kuhusiana na mchanga wa dhahabu na matukio mengine hapa nchini kwa kiasi kikubwa yamejaa taarifa zisizo za kweli zenye upotoshaji .

Binafsi nashindwa kuelewa aina ya siasa anayoifanya sasa zito na nini hasa malengo yake ukizingatia kwamba mtu wa kaliba yake anapaswa kuhakiki habari zake kabla ya kutoa kwa umma.
 
Wanasiasa wote ni wanafiki; Yaani ni wachumia tumbo hakuna jipya.
 
Upotoshaji ndo aina ya siasa tulizo chagua,ni muhongo huyuhuyu alie sema tanzania itakua na umeme mwingi hadi tutawauzia nchi za jirani.na ni huyuhuyu muhongo anashangilia tanzania kununua umeme toka Ethiopia.
 
nimekua nikifuatilia hoja zinazoibuliwa na mwanasiasa wa Upinzani kupitia ACT nyingi ya hizo zinabase katika Taarifa zisizo sahihi hivyo kupotosha umma.

kwakua Zito tayari ana base ya followers ni rahisi sana ku consume wrong information ambazo ipo siku zitazua taharuki.

Zito akijua kabisa kwamba sio kweli: amepotosha Tafsiri ya mkataba wa Jumuia ya Afrika Mashariki kuhusiana na mgawanyo wa uwakilishi wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki.

Zito akijua kabisa; amepotosha kuwa sio kweli: alipotosha hali ya chakula hapa nchini kwa kutoa Taarifa za njaa ilhali hakuna hali kama hiyo hapa nchini.

Taarifa za zito kuhusiana na mchanga wa dhahabu na matukio mengine hapa nchini kwa kiasi kikubwa yamejaa taarifa zisizo za kweli zenye upotoshaji .

Binafsi nashindwa kuelewa aina ya siasa anayoifanya sasa zito na nini hasa malengo yake ukizingatia kwamba mtu wa kaliba yake anapaswa kuhakiki habari zake kabla ya kutoa kwa umma.
nimevutiwa sana na andiko lako kuwa zito kuwa anapotosha umma je unaweza kututhibitishia hizo kauli ni za uongo,kifupi ni kwamba hakuna mwanasiasa anayeaminika hata upande unaamini ww! labda siasa ya la tumbo binafsi
 
Upotoshaji ndo aina ya siasa tulizo chagua,ni muhongo huyuhuyu alie sema tanzania itakua na umeme mwingi hadi tutawauzia nchi za jirani.na ni huyuhuyu muhongo anashangilia tanzania kununua umeme toka Ethiopia.

Ndiyo siasa za sarakasi hizi, Yaani ukijipindua kwa mbele akisikia anapasuka tumbo, basi wanajipindua kwenda nyuma kujaribu kama mgongo utaweza kumbeba.
 
Zitto alishaacha Siasa muda mrefu sasa hivi anashindana na wakina Wema na Diamond kupata followers kwenye mitandao ya Jamii
 
Back
Top Bottom