Zitto kung’oka CHADEMA

Akili ya zitto peke yake ni zaidi ya uongozi wa chadema taifa kwa pamoja yao

Nadhani hiyo itakua ni nafuu kwa CCM kwa sababu mtu mwenye akili nyingi namna hiyo akiondoka kwenye chama kinachowakosesha CCM usingizi si ni afadhari.We huoni kama mchezaji hodari akiwa hayupo ni nafuu kwa timu pinzani.
 


Hapana uko sawa kama SIASA unaangalia an individual or a society...

Wewe uko based with an individual kwahiyo chochote kibaya hautataka kumhusisha just because you love his individualism

Mfano; Angalia ni kwanini Kenyatta yuko THE HAGUE ?

Sasa turudi kwa KABWE... Kwanza alitaka kuanzisha Bendi ya wana KIGOMA na yeye awe kama Investor; WanaKigoma ina Maana waliozaliwa huko... Nchi yetu ya TANGANYIKA haijawahi kuwa na Masuala kama hayo; Hadi enzi za TIMU za MIKOA zilikuwa sio za KIKABILA...

Amepata Matatizo na CHAMA CHAKE yeye as an individual ni kwanini MCHADEMA yoyote aliyekwenda KIGOMA alikimbizwa na kupewa Ultimatum - to leave that REGION as if BOKO HARAM take Over?

Siasa sio CHUKI na Kukomoana au kutishia baadhi ya watu wa upande fulani...

Wanao EMBRACE vitu kama hivyo ina Maana wana ufinyu kimadaraka na pia wana chuki... nadhani uliona Mikwaruzano kati ya BILL CLINTON na OBAMA; BILL CLINTON speech ilisababisha OBAMA akashindwa kura katika jimbo la TEXAS...

Lakini baada ya OBAMA kumshinda HILLARY ni huyo huyo BILL CLINTON aliyetoa speeach mura kabisa iliyowaunganisha DEMOCRATS wote wenye itikadi Mbalimbali... na kumuwezesha OBAMA kushinda kwa LANDSLIDE...

Sasa, ni tofauti gani hizo ZITTO anazo zinazomfanya aondoke CHADEMA na ku create a barrier ?? OBAMA na HILLARY ndio walikuwa wanatupiana Maneno ya ajabu lakini ni tu waliheshimu kura za Wananchi wao

Kwani kweli hatuwezi kuijenga DEMOKRASIA ya kweli ? ZITTO ni only 36yrs OLD ana URAIS KIBAO

Angalia VIZURI hiyo HABARI uliyoiandika - Issue sio KIGOMA Issue is DIVISIONs created by POLITICIANS into their REGION


c.c
chikutentema
 
Kama ameshindwa hata kulitolea tamko marehemu mama yake kupigishwa kura kwenye BMK, sidhani kama anaweza kuaminika kwa chochote.
 
Hivi Zito bado yupo chadema!! Hawezi kutoka bora abane hapo hapo,atapotea.
 
Kama ameshindwa hata kulitolea tamko marehemu mama yake kupigishwa kura kwenye BMK, sidhani kama anaweza kuaminika kwa chochote.

hawezi toa tamko habari za uongo na uzushi
 

Asante kwa kueleza kuwa issue ni division, lakini kwanini hata wanahabari mmekuwa ni sehemu ya hiyo kampeni ku-justify the lies. Sijakataa kuwa Zitto anaumri huo unaousema lakini si yeye pekee kijana kwenye jamii ya watu mil. zaidi ya 45, wapo wengi wenginge hawajapata tu platforms tena yawezekana wenye karama hasaa na huo unaoitwa uzalendo. Mimi mwenyewe sifurahii kwa haya yaliyomkuta kijana huyu Zitto lakini wawezaje kuzuia kitu kilichoasisiwa na muhusika kwani tunaamini kila unachofanya at a moment kina results kesho. Anyway hoja zijengwe tuhukumiane lakini niweke wazi sipendi mtu anayejaji kitu kwa kutumia, dini, kabila, rangi, ufupi, urefu, uzima ama ulemavu kwani hata Mwal. Nyerere alisema mtu wa aina hiyo hana hoja na wala uhalali wa kupewa anachopigania nngu007
 
Last edited by a moderator:

Mkuu Getstart, Hapo kwenye red ndio mtihani mkubwa uliompa ZZK ambao nna uhakika hawezi faulu.Shida inakuja pale ambapo nia yake sio mabadiliko ya watanzania bali maslahi yake na miCCM.

Naamini kama ZZK angekuwa na dhamira safi na CDM haya yote yasingetokea, ila kwa matendo yake na ACT yake nashawishika kusema ametumwa, na huko atakakoenda ataenda kuendeleza kile alichotumwa na kushindwa ndani ya CDM.
 
Zitto unatisha ndo maana Mbowe na magazeti yake wanakufuatilia sana.
 
Zitto anachukiwa na viongozi wa chadema, wakamfitni kisa hatoki kaskazini. Ubaguzi ndani ya chadema ni mkubwa sana


Hii single ilishachuja muda mrefu ,tafuteni nyingine mje nayo.
 
Bado anasubiri nini???? Apotee !!! Au ile kauli yake ya "Nitakuwa mtu wa mwisho kutoka CHADEMA" inamhangaisha????
 
zitto hayupo chadema tulimshamfukuza siku nyingi akakimbilia mahakamani labda na huko ameshashindwa ndo maana aende kwa wanafiki wenzake ccm au act
 
Akili ya zitto peke yake ni zaidi ya uongozi wa chadema taifa kwa pamoja yao
Kumbe wewe ndiye yule mgombanishi aliyetajwa na ZZK. Mwacheni ZZK afanye maamuzi yake mwenyewe. Sasa anattaka kutubu na kurejea CDM yetu hata bila ya uongozi kwani anajua uongozi ni dhamana. Mshindwe wachonganishi wote.
 

Kwani sasa hivi yuko cdm? Mbona alifukuzwa siku nyingi?
 
Zitto anachukiwa na viongozi wa chadema, wakamfitni kisa hatoki kaskazini. Ubaguzi ndani ya chadema ni mkubwa sana

Ubaguzi ndani ya cdm ni mkubwa kama ilivyo wizi wa rasilimaki za taifa ndani ya viongozi wa ccm.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…