Zitto kugomea posho ya laki 3!!!

Zitto kugomea posho ya laki 3!!!

Status
Not open for further replies.
Huyo ndio Zitto, mzee wa Walkie the Talkie. Ni miongoni mwa wanasiasa wachache wenye uwezo wa kusimamia misimamo yao kwa vitendo. Kwenye hili suala la posho, Tanzania itamuheshimu sana kijana huyu.
Lile brief case lekundu alilopokea toka kwa Kimei mbele ya wapambe wa TISS angepeleka kwa mayatima badala ya kuenjoy yeye na familia yake tungemwita mzee wa walk the talk vinginevyo anajidanganya mwenyewe na wapambe wake
 
WanaJF,

Wakati wabunge wa bunge la JMT na wajumbe wa bunge maalumu la katiba wakililia posho iongezwe, kwa mhe. Zitto imekuwa tofauti kwani yeye amepanga kugomea posho hiyo.

Maamuzi ya mhe. Zitto ya kugomea posho sio mageni, kwani ni mbunge wa kwanza wa bunge la JMT kuwahi kukataa posho za vikao na kusimama na msimamo huo mpaka hii leo.

Mhe. Zitto ameonekana kuwashangaa sana wabunge wanao simamia suala la kuongezeka kwa posho kwa kigezo cha kuongezeka kwa gharama za maisha. Hapa alihoji," hizo gharama za maisha zinakuwa kwa wabunge pekee?! Vipi na kwa Watanzania wengine hasa walala hoi?"

Aidha, mhe Zitto amewataka wabunge na wajumbe wa bunge maalumu la katiba kusimamia mambo ya msingi yaliyo wapeleka bungeni na kuyapa kipaumbele zaidi badala ya kuvalia njuga suala la maslahi yao binafsi.

msanii tu, zinawekwa kwenye akaunti yake
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom