Zitto kufunguliwa mashtaka endapo...

Zitto kufunguliwa mashtaka endapo...

mcubic

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2011
Posts
10,310
Reaction score
6,546

Mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, amepewa siku 14 kufuta kauli yake na kuomba radhi kwa kumhusisha rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein na makosa ya uhaini.

Msimamo huo ulitolewa na wagombea wawili wa nafasi ya urais wa Zanzibar, Juma Ali Khatib (Tadea) na Soud Said Soud, walipokuwa wakizungumzia kauli ya Zitto kudai haikuwa sahihi kwa Rais wa Zanzibar kubakia madarakani wakati serikali yake imefikia ukomo wake Novemba 2, mwaka huu.

Soud alisema kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar Kifungu cha 28 (1)(a), Rais Shein ni Rais halali wa Zanzibar na atabakia madarakani hadi atakapochaguliwa rais mpya kwenye uchaguzi wa marudio.

Alisema kuwa Dk. Shein alichaguliwa na wananchi wa Zanzibar na haikuwa haki kwa Zitto kumhusisha na makosa ya uhaini kwa kuendelea kubaki madarakani kwani yuko kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984. ?Zitto Kabwe afute kauli yake na kuwaomba radhi wananchi wa Zanzibar ndani ya siku 14 na asipofanya hivyo tutamfungulia mashitaka.? alisema Soud pia Mwenyekiti wa Chama cha AFP.

Katika sakata hilo, Juma Ali Khatib, alisema tayari ameanza kutafuta namna ya kuwasiliana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuwasilisha malalamiko yake dhidi ya Zitto kwa kumhusisha na makosa ya uhaini Rais wa Zanzibar.

Alisema iwapo Bunge litashindwa kumchukulia hatua za kinidhamu Zitto, yeye atalazimika kufungua kesi kwa niaba ya wananchi wa Zanzibar kupinga kauli ya Zitto.

Khatib alisema Zanzibar ni nchi na Rais wa Zanzibar lazima apewe heshima yake kwa sababu kuendelea kuwepo kwake madarakani ni matakwa ya Kikatiba.

?Kumdhalilisha Rais wa nchi ni sawa na kutudhalilisha wananchi wake, rais anashauriwa na vyombo vingi vya sheria hivyo hawezi kuvunja Katiba,??alisema Khatib
Viongozi hao si wa kwanza kujitokeza kumtetea Rais wa Zanzibar kwani walitanguliwa na aliyekuwa Kamishna wa Tume ya Rais ya Mabadiliko ya Katiba, Simai Mohamed Said, tangu Zitto alipotoa kauli kuwa Zanzibar haina rais na kuendelea kubakia madarakani Rais Shein ni sawa na kufanya uhalifu wa uhaini.

Katika mkutano wake na wandishi wa habari hivi karibuni, Zitto alisema kwa sasa Zanzibar haina serikali na mtu yoyote anayejiita rais wa Zanzibar kikatiba amepindua nchi na katika hali ya kawaida anapaswa kushitakiwa kwa uhaini.

CHANZO: NIPASHE

Kwa hiyo Shein anatetewa na wapinzani wake????
 
Zito nakuchukia sana ila sometimes maneno yako huwa nimatamu sana, safi sana kabwe wala hapa hakuna wakukufunga.
 
Ndio maajabu hayo. Pili kwani zitto alitoa kauli zile akiwa bungeni? au nje ya bunge na kabla hajala kiapo? sasa kama ni kabla hajaapa Speaker anaingiaje hapo? yaani hizi ni dalili za wanasiasa uchwala
 
Mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, amepewa siku 14 kufuta kauli yake na kuomba radhi kwa kumhusisha rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein na makosa ya uhaini.

Msimamo huo ulitolewa na wagombea wawili wa nafasi ya urais wa Zanzibar, Juma Ali Khatib (Tadea) na Soud Said Soud, walipokuwa wakizungumzia kauli ya Zitto kudai haikuwa sahihi kwa Rais wa Zanzibar kubakia madarakani wakati serikali yake imefikia ukomo wake Novemba 2, mwaka huu.

Soud alisema kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar Kifungu cha 28 (1)(a), Rais Shein ni Rais halali wa Zanzibar na atabakia madarakani hadi atakapochaguliwa rais mpya kwenye uchaguzi wa marudio.

Alisema kuwa Dk. Shein alichaguliwa na wananchi wa Zanzibar na haikuwa haki kwa Zitto kumhusisha na makosa ya uhaini kwa kuendelea kubaki madarakani kwani yuko kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984. ?Zitto Kabwe afute kauli yake na kuwaomba radhi wananchi wa Zanzibar ndani ya siku 14 na asipofanya hivyo tutamfungulia mashitaka.? alisema Soud pia Mwenyekiti wa Chama cha AFP.

Katika sakata hilo, Juma Ali Khatib, alisema tayari ameanza kutafuta namna ya kuwasiliana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuwasilisha malalamiko yake dhidi ya Zitto kwa kumhusisha na makosa ya uhaini Rais wa Zanzibar.

Alisema iwapo Bunge litashindwa kumchukulia hatua za kinidhamu Zitto, yeye atalazimika kufungua kesi kwa niaba ya wananchi wa Zanzibar kupinga kauli ya Zitto.

Khatib alisema Zanzibar ni nchi na Rais wa Zanzibar lazima apewe heshima yake kwa sababu kuendelea kuwepo kwake madarakani ni matakwa ya Kikatiba.

?Kumdhalilisha Rais wa nchi ni sawa na kutudhalilisha wananchi wake, rais anashauriwa na vyombo vingi vya sheria hivyo hawezi kuvunja Katiba,??alisema Khatib
Viongozi hao si wa kwanza kujitokeza kumtetea Rais wa Zanzibar kwani walitanguliwa na aliyekuwa Kamishna wa Tume ya Rais ya Mabadiliko ya Katiba, Simai Mohamed Said, tangu Zitto alipotoa kauli kuwa Zanzibar haina rais na kuendelea kubakia madarakani Rais Shein ni sawa na kufanya uhalifu wa uhaini.

Katika mkutano wake na wandishi wa habari hivi karibuni, Zitto alisema kwa sasa Zanzibar haina serikali na mtu yoyote anayejiita rais wa Zanzibar kikatiba amepindua nchi na katika hali ya kawaida anapaswa kushitakiwa kwa uhaini.

CHANZO: NIPASHE

Waende mbali zaidi na kuona kama kuna haja pia ya kumfungulia aliyekuwa M/kiti ZEC kufuta matokeo ya uchaguzi kama alikuwa na uhalali huo kikatiba.
 
Zito nakuchukia sana ila sometimes maneno yako huwa nimatamu sana, safi sana kabwe wala hapa hakuna wakukufunga.

Zitto ni mnafiki tu. Kama anamaanisha anachokisema basi angetoka nje Dr. Sheni alipoingia bungeni. Kubaki kwake kulimaanisha anamuunga mkono na anakubali kinachoendelea ZNZ.
 
ama kweli maajabu yote ya dunia yapo tanzania! wapinzan wamegeuka kuwa watetez
 
mi naona position ya rais wa zanzibar ifutwe tu, kama ni ncho moja mambo ya kua na marais wawili lazima ipo siku vurugu zitatokea, yaweza isiwe mwaka huu ila it that time will come. kama ni ncho moja basi iwe na katiba moja, sheria moja, rais moja, in other words zanzibar isiitwe nchi igeuzwe kua mkoa.
 
Ha ha ha yaleyale ya Zitto ya kuambatana na CCM kurusha mishare kwa wapinzani naye yameanza kumpata.
 
Jibu lako hili hapa chini.

Ukishangaa ya yamoto kuwa band pasipo kuwa hata na gitaa utayona ya diamond kushinda tunzo America pasipo kuwa hata na single wanayoijua.

Yaani Wanasiasa kila kukicha hutafuta kitu kitakachowafanya wasikike kwenye vyombo vya Habari..kwahiyo hata hawa wanaodai kumbuluza Zitto Mahakamani sio kweli kuwa watafanya hivyo,hapo ndio mwisho,baadae watatafta kingine iliwasikike tofauti kabsa na swala la Zitto.
 
Zitto ni mnafiki tu. Kama anamaanisha anachokisema basi angetoka nje Dr. Sheni alipoingia bungeni. Kubaki kwake kulimaanisha anamuunga mkono na anakubali kinachoendelea ZNZ.

Zitto hakusimama shein alipoingia,ukawa walizomea.
Approach ni tofauti sio wote muwe sawa.
 
Back
Top Bottom