Zitto karibu NCCR

unaumwa ugonjwa wa chuki,husuda na kisebusebu
 

Kwahiyo unatushauri nini? tuendelee kukaa na hawa majambazi wetu CCM tu?( zimwi likujualo) kwa maana Silaa hafai na mbowe hafai,
 
Wenyewe NCCR tupo kimya mnao tumika mnakaribisha watu. Kazi ya kumkaribisha alianza kuifanya Mh. Kafulila leo yupo wapi? Nccr ilimshinda Mh. Mrema, Marando, Nswanzigwako,Ngawaiya, Lamwai n.k itakuwa ZITTO mwache aje akishindwa kufuata sera na muongozo wa chama akamuulize swahiba wake Kafulila nini kilicho mfanya alie siku ya mkutano wa kumvua uanachama
 
Hakuna sehemu nimeandika kama anakuja NCCR kwa ajili ya kugombea au kuteuliwa kugombea Uraisi, nimefahamika sivyo ,hata hivyo inawezekana akawa mgombea mtarajiwa ,kitu ambacho hakipatikani wala si cha kuweeka tamaa huko CDM hata akifa Slaa ndio maana yake,m'meona.
 
NCCR na CUF vilifanya kwa zamu ila kwa CDM hakuna zamu ila mkakati madhubuti wa kuikomboa Tanzania, nani asiyejua NCCR ni chama cha kufukuzana na kung'ang'ania madaraka? nani asiyejua uchu wa uongozi alio nao mwenyekiti wa NCCR?

Zinduka kijana hupelekani na hoja zako hata kidogo, unafanania na mzee wa 1947...
 
Imepita CUF hakuna la maana ,imeambiwa Chama cha kidini ,imefika CDM imeambiwa na inaonekana Chama Cha walokole ,sasa ni zamu ya NCCR.

kabla ya CUF na sasa CDM, NCCR ilishatikisa na ikawa maututi

mgonjwa kunywa uji bado anabaki mgonjwa tuu
 
Nakuhurumia kwani unauvivu wa kufikiri.chama makini,chama kinacholeta matumaini,maendeleo na ukombozi kwa wananchi ni kile kinacho toka hatua moja nyuma na kusonga mbele.tafuta historia ya nccr tangu 1995-2012 na historia ya chadema.zitto tulikomboe taifa achana na ccm b.
 


Umshauri aende CCM ambako hata wewe una maslahi.
 

Kabla ya kuchangia jaribu kuperuse baadhi ya thread hapa jamvini.Kuna mambo mengi ambayo Dr.Slaa aliwahi kuja hapa na kuyatolea maelezo,likiwemo suala la kuacha upadri.Mwaka 2010 aliulizwa maswali hapa na kujibu.
 
Hivi Mwiba?
Kwa fikra nlzozisoma kwenye bandiko lako, labda kama nmekosea naomba unirekebishe, ni kwamba unapangwa mkakati wa kumkaribisha Zitto rasmi kwenye chama chenu ili mtoke kwa mara ya pili?
Hivyo ni sahihi kusoma "Zitto= NCCR kutoka kwa mara ya pili" ??
Ok kama sio mkakati wa kumnasa Zitto pekee, kwanini hujawataja hao wengine?
Hivi lini tutaondoa siasa za majina na kujikita kwenye itikadi za ukombozi halisi??
Kama NCCR mnampango wa kurudi kwa mtindo nadhani ndio mtakuwa matapishi hasa.
 
Mchkueni tu coz ni mamluki huyo,CHADEMA 2namwangalia 2
 
Watanzania lazima tuelewe, katika kila kikundi kuna malengo ya kundi na malengo binafsi. Jamii starabu na yenye malengo ya mbele huwa inayapa nguvu malengo ya kkundi. CDM wanataka kuchua dola. Sasa kama kuna upungufu kwa dr. Slaa ukimlinganisha na Zitto basi zitto apewe hiyo nafasi lakini kubadili 'figure' wakati wametumia pesa nyingi kumnadi Slaa itakuwa ni uendawazimu.( sina chama).
 

Mara nyingi ukiwasikiliza vichaa wanapoongea na wenye akili utawasikia, 'mimi nina akili sana kuliko ninyi'
 

Kwanza chama kilichokuwa juu sana katika upinzani nakushuka hadi karibu na usawa wa bahari ni NCCR. Lakini mrudisheni kwanza Kafulila ndio muzumze kuhusu Zito. Nia yenu mbaya sana, mnataka kuharibu future ya Zitto Kabwe.
 

Sio uendawazimu bali hawajui wanalolitenda.
 
Mnyonge mnyongeni jamani. Nilimsikia zitto akiwasilisha hoja juzi kwakweli sioni wa mfano cdm. Hiki kifaa presidential matrrial
 
Mkuu ukienda huko na wewe utaulizwa kuhusu akina Dr. Slaa, Mtei, Joseph Selasini, Chiku Abwao, Shibuda, nk walilelewa na Vyama gani?
 
Mnyonge mnyongeni jamani. Nilimsikia zitto akiwasilisha hoja juzi kwakweli sioni wa mfano cdm. Hiki kifaa presidential matrrial
Utafukuzwa uanachama wewe. Hili suala haliongelewi ndani ya CDM. Suala la uenyekiti na kugombea Urais ndani ya CDM linaongelewa na Mzee wa Chama. Siyo kila mtu akurupuke kuongelea hayo mambo! Naona CCM nao wameanzisha japo la wazee; wao wako wengi ila kwa CDM ni mzee.

ANGALIZO: Sitaki matusi kwa kuwa ndivyo ilivyo. Usithubutu kutukana toa hoja.
 

Kwani leo ni April mosi???
 
Akitoa mguu wake Chadema, umaarufu zero, Kama mwanisha mwamieni ajaribu ....


QUOTE=Mwiba;3243161]:fish2: Mh.Zitto achana na akina Slaa na genge lake ,hao ndio wale wale ving'ang'anizi wasio penda kuachia vijana kuliongoza Taifa hili ,ukibakia hapo utafariki ukijiona.
La muhimu ni kuwa Chama kinakungojea kwa hamu kabisa na safari hii ni zamu ya NCCR kuongoza na kuunyakua uongozi wa kuliongoza Taifa hili la Tanzania kwa kishindo.

Najua wapo watakao beza rasimu hii ya kumkaribisha mheshimiwa Zitto katika mageuzi kwani si jambo la kulitegemea sana kwa upande wao ,waonavyo eti wamemzibiti ,nawambia huko ni kujidanganya.
Kuhusu Mwenyekiti wa NCCR aliepo ,tayari ameshaonyesha dalili za kustaafu au kubakia katika benchi la viongozi wazee wa Chama.[/QUOTE]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…