Zitto: Kamati zote za Bunge zina hadhi sawa ndani ya Bunge

Ritz

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
49,680
39,008
Wanaukumbi.

Zitto.

Kamati zote za Bunge zina hadhi sawa ndani ya Bunge. Kila mbunge ana haki ya kuwa kwenye kamati yeyote ile na hakuna mbunge bora zaidi ya mwingine. Kanuni zimeweka utaratibu wa uteuzi kwenye Kamati ikiwemo maombi ya mbunge, uzoefu na ujuzi wa eneo husika.

Wanaolalamika leo upangaji wa Kamati ndio usiku wa kuamkia jana walimshinikiza Spika asiwapange mahasimu wao kisiasa kwenye Kamati wanazoona wao ni nyeti. Ni unafiki uliopitiliza unapojenga hoja ya uzoefu, chaguo la Mbunge na ujuzi wakati huo huo wenye vigezo vyote hivyo unawapiga vita kwa sababu za kisiasa.

Ni dhahiri kuwa mpangilio wa Kamati unajenga Bunge kibogoyo. Nilitahadharisha toka Bunge la 11 lilipoanza kwamba, kuna dalili za Serikali kutaka kulidhibiti Bunge ( kumbukeni sarakasi za Tulia Ackson ambaye sasa ni Naibu Spika) .

Kiongozi unapokwenda kwa Spika kusema 'fulani asipangwe Kamati fulani kwa sababu atapata sifa' halafu ukataka 'Mtu' wako ndio wapangwe huko ujue unaisadia Serikali kudogosha Bunge. Spika anapoamua Nyote, huyo usiyemtaka na Mtu wako wasiende huko ujue amekudharau sana.

Unapoona Viongozi wa Serikali wanahangaika kupanga Kamati za Bunge watakavyo wao ujue viongozi hao ni dhaifu, hawana nia njema na hawataki kuwajibishwa. Twendeni kwenye hizi hizi Kamati tulizopangiwa kuwafanyia kazi Watanzania. Twendeni tukaonyeshe kuwa Bunge litabaki Bunge tu na Wabunge tusikubali Bunge Kibogoyo. Ni lazima Bunge lidhibiti Serikali hata Serikali hiyo ikiwa inaongozwa na Malaika.

Serikali ni chombo cha mabavu lazima idhibitiwe, na ndio kazi ya Bunge kwa mujibu wa Katiba Ibara ya 63.
 
Nashangaa wabunge wa chama chetu tu ndio wanalalamika kupangwa kamati ambazo hazikuwa matarajio yao,sasa sijui utaratibu wa kupangwa ukoje? nani mwenye mamlaka ya kupanga? na je kuna wabunge maalumu kwenye kamati maalumu?
 
ila kwa ukweli tunaenda kuwa na Bunge kibogoyo, lusinde kuwa mjumbe wa PAC, hilary aeshi kuwa makamu mwenyekiti PAC, sio bure ndugai anaumwa
 
ila kwa ukweli tunaenda kuwa na Bunge kibogoyo, lusinde kuwa mjumbe wa PAC, hilary aeshi kuwa makamu mwenyekiti PAC, sio bure ndugai anaumwa

Dah yaaani hizi siasa za kipuuzi sana,huyo Aeshi ni mpiga dili mkubwa pale mpanda yeye na mtoto wa mkulima,ndio kapelekwa kamati hiyo kupiga madili ya kufa mtu
 
Dah yaaani hizi siasa za kipuuzi sana,huyo Aeshi ni mpiga dili mkubwa pale mpanda yeye na mtoto wa mkulima,ndio kapelekwa kamati hiyo kupiga madili ya kufa mtu

inakera sana ndugu kwa upuuzi aliofanya ndugai, aeshi hata darasa la saba sijui kama alimaliza, unampanga martha mlata kuwa mwenyekiti kamati ya nishati na madini, hivi kweli tuko serious au ni upuuzi wa hali ya juu unaendelea pale bungeni? NDUGUA MUST GO BACK TO INDIA HE IS SICK
 
Kwa aish apo apana spika inakaa walikosea dozi uko ulikoenda tibiwa India maana aish ni fom4 felia mhun flan wa sumbawanga pale yaan inabid spika achunguzwe
 
Kumbe sumbawanga wameendelea ,hadi kuna wahuni sikuhizi?


Yeah,kamati za bunge bunge hili zimepwaya sana,hakutakua na msisimko wowote
 
Badala ya kuwalalamikia waliomshinikiza spika kupanga hivi na vile, kwa nini asimlaumu spika ambaye ndiye mwamuzi wa mwisho?
 
Na kama kamati zote zina hadhi sawa, kwa nini achukie badala ya kufurahi kwa kuteuliwa kuwemo ktk moja ya kamati?
 
Kumbe sumbawanga wameendelea ,hadi kuna wahuni sikuhizi?


Yeah,kamati za bunge bunge hili zimepwaya sana,hakutakua na msisimko wowote
Ukawa hawana tatizo na ilo wao shida yao kubwa ilikuwa kuona Zitto hayumo kwenye PAC basi.

Teh teh teh!!
 
zitto wkt mwingine yupo vzr, alikuwa ni assets nzuri sana hasa 2020 chadema, sema naye kazid mijimambo
 
...naona bora huyo 'kiongozi' aliyetaka wabunge wake wapewe hizo kamati,hata km wamekosa,ila wao ni wapinzani.Tumeona mara ngapi yeye zitto akiifanyia kazi ccm,anataka kumlazimisha nani amuamini,km angewekwa safari hii asingeifanyia kazi ccm?!
Namuona Zitto km amechanganyikiwa,pamoja na kujipendekeza kote kwa Magufuli wakati wa ile hotuba bungeni,bado katoswa,wapinzani wengine hawamuamini,hawawezi kufanya nae kazi,sijui masikini wa watu atakuwa na impact gani ndani ya hili bunge...muacheni aendelee kupayuka tu,amechanganyikiwa!!
 
Back
Top Bottom