Zitto: Kama Rais anaona Bunge ni kikwazo kwake, tufanye uchaguzi upya. Hii si Gangsters Republic

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,739
32,866
Wabunge walitoa Hoja Binafsi kuhusu Madawa ya kulevya ( Esther Bulaya na Faustine Ndugulile ) na kufuatia hoja hiyo Serikali ikaleta Muswada bungeni na Bunge likatunga Sheria ya Kupambana na Madawa ya kulevya mwaka 2015.

Serikali mpya ikaingia madarakani mwezi Novemba 2015. February 2017 Ndio Kamishna Mkuu anateuliwa tena baada ya wabunge kuhoji na kushinikiza kupitia Kamati husika na pia mbunge Esther Bulaya aliyetoa Hoja Binafsi katika Bunge la Kumi.

Rais anasema hakuwa anajua kuwa sheria hiyo ipo. Lakini Rais anapogawa Wizara huwa anatoa instruments na Hizo instruments hutaja kila sheria kwa kila Waziri. Ilikuwaje Rais akasahau sheria hii nyeti kama alikuwa na nia ya dhati ya Kupambana na Madawa ya kulevya?

Rais anaona Bunge kikwazo kwa sababu Bunge linamwongoza afuate sheria. Lakini Kama anaona Bunge linamkera turudi kwenye uchaguzi tu, alivunje.

Kuna mtu anadhani watu watahangaika na Waziri Mkuu. Why? Anajidanganya Sana.

PM ni mbunge mwenzetu. Hatuna shida naye.

Ukitaka kula chura kula aliyenona.

Sasa MABADILIKO waliyoyataka wananchi mungu anayaleta kwa njia zake alizochagua. Njia zinazokomaza Taasisi za nchi yetu.

Heshima kubwa kwa Wabunge wa Bunge la 4 kwa mabadiliko makubwa ya Katiba ya mwaka 1984.

Hii nchi sio Gangsters Republic. Hii nchi ya Nyerere hii ina misingi ya Haki na Utu. Hii ni United Republic of Tanzania.

Kutoka:

Rais hajasema alikuwa hajui sheria kama ipo bali alikuwa anajiuliza kwa nini hajaletewa mapendekezo ya kuteua Kamishna Mkuu wa kupambana na madawa ya kulevya.

Rais amesema Waziri Mkuu alikuwa hafahamu kama yeye ni Mwenyekiti wa tume ya kuthibiti madawa ya kulevya.

Tuacheni kupotosha wakati ukweli upo katika video kuanzia dakika ya 20.

Tumkosoe Rais huku tukitumia ukweli na sio kugeuza maneno ili hoja zetu zikubalike.

Hii hapa ni video kuhusu alichokisema Rais Magufuli kuhusiana na Kamishna Mkuu wa kupambana na madawa ya kulevya. Kama MB zako ni chache, anzia kwenye dakika ya 20.

Gangstar Republic inaongozwa na thugs in suit.

Mkuu wa kijiji aache kupanic aongoze kijiji chake kwakufuata taratibu.

Inachekesha sana na ile kauli yake "hii nchi imeibiwa sana". Sasa kama imeibiwa sana na wewe ndiyo unataka kuvunja sheria?
 
Mungu zidi kuubariki Upinzani wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania. Tumejua na kujifumza mengi kupitia wao. Ongeza ulinzi wa malaika wako kwa Wapinzani wote. Na wazidishie nafsi na roho ya Ujasiri, vikiambatana na maarifa, kwa kila majaribu wanayokutana nayo, haswa katika hawamu hii ya 5.
Ameen.
 
Nimerealize Rais yuko oblivious na vitu vingi sana

Which tunarudi kule kule, kuwa either watu wanaogopa kumshauri au hawamshauri vizuri....

AG na waziri wa sheria wako wapi mpaka Rais anatamka kuwa alikuwa hajui kuna such a law

This goes to show kuwa kuna some people hawafanyi kazi zao ipasavyo mpaka Rais anafanya blunder za wazi wazi e.g kuteua wabunge wa kiume zaidi ya 5, na sasa hili la kitengo sensitive kama hiki kutokuwa na kiongozi for almost 2 years
 
Wabunge walitoa Hoja Binafsi kuhusu Madawa ya kulevya ( Esther Bulaya na Faustine Ndugulile ) na kufuatia hoja hiyo Serikali ikaleta Muswada bungeni na Bunge likatunga Sheria ya Kupambana na Madawa ya kulevya mwaka 2015.

Serikali mpya ikaingia madarakani mwezi Novemba 2015. February 2017 Ndio Kamishna Mkuu anateuliwa tena baada ya wabunge kuhoji na kushinikiza kupitia Kamati husika na pia mbunge Esther Bulaya aliyetoa Hoja Binafsi katika Bunge la Kumi.

Rais anasema hakuwa anajua kuwa sheria hiyo ipo. Lakini Rais anapogawa Wizara huwa anatoa instruments na Hizo instruments hutaja kila sheria kwa kila Waziri. Ilikuwaje Rais akasahau sheria hii nyeti kama alikuwa na nia ya dhati ya Kupambana na Madawa ya kulevya?

Rais anaona Bunge kikwazo kwa sababu Bunge linamwongoza afuate sheria. Lakini Kama anaona Bunge linamkera turudi kwenye uchaguzi tu, alivunje.

Kuna mtu anadhani watu watahangaika na Waziri Mkuu. Why? Anajidanganya Sana.

PM ni mbunge mwenzetu. Hatuna shida naye.

Ukitaka kula chura kula aliyenona.

Sasa MABADILIKO waliyoyataka wananchi mungu anayaleta kwa njia zake alizochagua. Njia zinazokomaza Taasisi za nchi yetu.

Heshima kubwa kwa Wabunge wa Bunge la 4 kwa mabadiliko makubwa ya Katiba ya mwaka 1984.

Hii nchi sio Gangsters Republic. Hii nchi ya Nyerere hii ina misingi ya Haki na Utu. Hii ni United Republic of Tanzania.

Kutoka:

Mkuu wa kaya anaona kama TZ ni chenchi iliyopo mfukoni mwake kila akitembea anazichezesha.. akitaka dafu anachomoa kadhaa nakupokea... UTD RPBLC of TZ
 
Rais hajasema alikuwa hajui sheria kama ipo bali alikuwa anajiuliza kwa nini hajaletewa mapendekezo ya kuteua Kamishna Mkuu wa kupambana na madawa ya kulevya.

Tuachenio kupotosha wakati ukweli upo katika video.

Hii hapa ni video kuhusu alichokisema Rais Magufuli kuhusiana na Kamishna Mkuu wa kupambana na madawa ya kulevya.

Haya aliyasemea wapi wakuu?
 
Rais hajasema alikuwa hajui sheria kama ipo bali alikuwa anajiuliza kwa nini hajaletewa mapendekezo ya kuteua Kamishna Mkuu wa kupambana na madawa ya kulevya.

Mkuu hayo ndio madhara ya kuwa mkali kupita kiasi hata kwa mambo yasiyohitaji ukali. Inafikia mahali unaoshirikiana nao wanaona unajua kila kitu hivyo waanacha utekeleze. Kwa ujumla watu wanahitaji kiongozi makini na baadhi ya sehemu uwe mkali na sio mara nyingi kuongozwa na jazba. Kumbuka ukifanya kazi na watu wazima sio watoto, kufoka sana hakuwezi kukufanya kuwa bora. Udhaifu ninaouna ni mkuu kukosa subira na sheria zisizokidhi tabia yake ya jazba, hivyo kujikuta anatoa sheria za mfukoni zinazokidhi matamanio yake. Kwa namna yake ya jazba ndio tuona wapi sheria zisizo kwenye vitabu vya sheria na kusikia sheria zinazoitwa amri toka juu zinapotoka. Niliposikia anasema mtu kama amehukumiwa kunyongwa acha anyongwe, je sheria zetu zinaruhusu kunyongwa kwa madawa ya kulevya? Kuna haja gani ya kuwa na balozi ambaye hawezi kutetea wananchi wake? Hata kama mtu amefanya makosa lakini ni lazima nchi yetu itumie njia za kidiplomasia kutetea mwananchi wake na kuja kumpa adhabu zinazoendana na taifa letu na sio adhabu za utashi wa rais. Kwa hapa ndio tunaona kwanini Mh. Lema yuko ndani mpaka leo.
 
hahaha Zitto sijui kaandika nini? Vipi hoja ya kutokuwa na imani na Rais anaiwasilisha lini?
 
Back
Top Bottom