Faru John II
Senior Member
- Dec 27, 2016
- 134
- 135
Binafsi nimeingiwa na masikitiko kumuona ndugu Zitto Kabwe akilivalia njuga suala la Mbowe kuhusishwa na madawa ya kulevya. Nimesikitika pia Mbowe kujitetea sana wakati hata hajui anaitiwa nini. Kwanini Ujijitetee kiasi hicho? Kwanini Uogope kufika Central ikiwa wewe ni msafi na unataka tulio-nyuma yako tuamini kuwa wewe ni msafi? Kujitetea kwa ghadhabu kiasi hiki kunanipa picha kuwa suala hili sio lelemama, ni kubwa kuliko tunavyodhani.
Jambo lililonifanya nipigwe butwaa ni huyu Mbunge wa Kigoma mjini kuamini kuwa tuhuma hizi dhidi ya Mbowe ni vita dhidi ya Upinzani Tanzania huku akishindwa kufafanua kivipi. Pia, Zitto aliamini kuwa Wapinzani ni malaika wasioweza kabisa kuingia ktk aibu ya namna hii, haya ni makosa makubwa.
Nachokiona kwa Zitto Kabwe ni kujiingiza ktk kadhia asiyoijua. Kama anatafuta mvuto wa kisiasa na kutafuta kukubalika na Wana-CDM atakuwa anapoteza muda bora chama chake kibuni mbinu za mapambano kwa kutazama udhaifu wa CCM na Chadema ktk kukabiliana na changamoto za Wananchi kuliko kuendelea kumpigia mbuzi gitaa.
Ni vyema wote tukaweka maslahi ya Utaifa mbele kupambana na vita dhidi ya Mihadarati. Tuwe tayari kuwaanika hata wazazi wetu wanaojihusisha na biashara hii inayopunguza jitihada za kuondoa Umasikini nchini kwetu. Tuwe na dhamira moja, ajenda moja tu ya KUPAMBANA na mihadarati.
Natoa Wito kwa Serikali na kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuendelea kupiga sehemu yenye Makelele Mengi