MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,976
Tarehe 20 Januari 2020, Chama cha ACT-Wazalendo kupitia Katibu Mwenezi wake, Ado Shaibu kiliitisha mkutano wa waandishi wa habari na kuahidi kuwa iwapo serikali kupitia TCRA itazima laini za simu za mkononi kwa wananchi ambao wametuma maombi au wale ambao NIDA imewapatia vitambulisho, ACT-Wazalendo wataipeleka serikali/TCRA mahakamani.
Ni ukweli kuwa mpaka sasa wananchi wengi katika makundi ambayo ACT-Wazalendo wameyataja wameishazimiwa simu zao.
Naomba ACT-Wazalendo mtimize ahadi yenu kwa kwenda kuishitaki TCRA/ Serikali mahakamani ili ''haki ya waliozimiwa simu zao ipatikane''.
ACT-Wazalendo kumbukeni kuwa ahadi ni deni hasa pale ambapo unatoa ahadi bila kuombwa!
Kutimiza ahadi yenu ya kuishitaki serikali mahakamani kutajenga imani kwa wapiga kura kuwa mkiahidi mnatekeleza!

VIDEO ya Katibu Mwenezi, Shaibu wakati akitoa ahadi ya kuishitaki TCRA/Serikali mahakamani