Hivi ni kazi ya Serikali kumrudishia uwakili Fatuma Karume?

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
34,176
45,780
Dar es Salaam. Chama cha ACT Wazalendo kimeitaka Serikali kumrejeshea Fatma Karume uwakili wake kama sehemu ya utekelezaji wa ahadi ya Rais Samia Suluhu Hassan kufungua ukurasa mpya wa wakisiasa.

Wito huo umetolewa na Katibu MKuu wa Chama hicho, Ado Shaibu akiwa kwenye kikao na viongozi na wanachama wa Kata ya Lilambo, Jimbo la Songea Mjini, Mkoa wa Ruvuma.

Fatma Karume alifutiwa uwakili wake Mwaka 2019 kutokana na kesi ambayo ilifunguliwa na Ado Shaibu wakati huo akiwa Katibu Mwenezi wa ACT Wazalendo dhidi ya aliyekuwa Rais wakati huo, John Magufuli, kupinga uteuzi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Adeladus Kilangi.

"Baada ya kuapishwa, Rais Samia aliahidi kufungua ukurasa mpya wa kisiasa nchini na ameanza kuchukua baadhi ya hatua ikiwemo kufanya mazungumzo na viongozi wa vyama vya upinzani.

"Dhana ya kufungua ukurasa mpya, inapaswa kutanuliwa na kuwagusa waathirika wote wa utawala uliopita. Inapaswa kuwagusa wavuvi waliochomewa nyavu zao, wakulima walioporwa korosho zao, wafanyabiashara walioporwa mitaji yao, wanaharakati na viongozi waliofungwa au kupotea," amesema Shaibu.

"Leo nina ombi maalum kwa Serikali. Ninaomba imrejeshee Fatma Karume uwakili wake. Bila kuathiri taratibu za kimahakama, nina hakika, hatua ya kumfutia uwakili wake ilitokana na msukumo wa kisiasa ili kumuadhibu kwa kesi aliyoisimamia kwa niaba yangu dhidi ya aliyekuwa Rais wa awamu wa tano

Source: Mwananchi
 

Just Distinctions

JF-Expert Member
May 5, 2016
1,431
1,760
Kwani aliofutiwa sababu iloelezwa ama? maana mi najua masuala ya sheria yana taratibu zake pia ndio maana kuna wakina kibatala mpaka kesho wanafanya kazi zao sa sielewi ye aliyumba wapi, mtupe ufafanuzi tafadhali
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
34,176
45,780
kwani aliofutiwa sababu iloelezwa ama? maana mi najua masuala ya sheria yana taratibu zake pia ndio maana kuna wakina kibatala mpaka kesho wanafanya kazi zao sa sielewi ye aliyumba wapi, mtupe ufafanuzi tafadhali
ACT wazalendo inaomba Serikali imrudishie uwakili!! Mihimili mitatu bunge ,mahakama na Serikali haijitegemei? Serikali ndio hutoa uwakili kwa mwanasheria?
Hivi ACT wazalendo kichwani akili zimo?
 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
12,264
46,721
ACT Wazalendo kumejaa chawa hata huyo Fatma Karume nae ni chawa tu.
 

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
18,680
29,404
ACT wazalendo inaomba Serikali imrudishie uwakili!! Mihimili mitatu bunge ,mahakama na Serikali haijitegemei? Serikali ndio hutoa uwakili kwa mwanasheria?
Hivi ACT wazalendo kichwani akili zimo?
Kwani inajitegemea??

Umesahau JIWE alituambia MHIMILI MMOJA WA KATIKATI umejisimika CHINI ZAIDI, na ndio unaotafuta kulisha mihimili ya pembeni?
 

mshale21

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
1,837
4,301
Hapa swala Ni katiba mpya tu,, haiwezekani serikali akawa mwamuzi wa mambo ya sheria huku mahakama ipo!!

Yani Raisi ana mandate kwa mihimili mitatu,,???!

Hii katiba inampa Rais Umungu Mtu, haipaswi kuwepo!
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
34,176
45,780
Kwani inajitegemea??

Umesahau JIWE alituambia MHIMILI MMOJA WA KATIKATI umejisimika CHINI ZAIDI, na ndio unaotafuta kulisha mihimili ya pembeni?
Usi base kwenye maneno na usiwe mtumwa wa Historia base kwenye sheria
Serikali kazi yake kufutia mawakili uwakili? Na kuwarudishia?
 

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
18,680
29,404
Usi base kwenye maneno na usiwe mtumwa wa Historia base kwenye sheria
Serikali kazi yake kufutia mawakili uwakili? Na kuwarudishia?
Achaga ujinga wakiCCM haki ngapi za watuhumiwa zilidhulumiwa wakati wa JPM? "Plea bargaining" (sina uhakika na spelling) wakanunua uhuru wao ilihali kesi hazikuwa na ushahidi toshelevu?
 

The Khoisan

JF-Expert Member
Jun 5, 2007
14,313
11,145
Usi base kwenye maneno na usiwe mtumwa wa Historia base kwenye sheria
Serikali kazi yake kufutia mawakili uwakili? Na kuwarudishia?
Kwani ni nani aliyemfutia Uwakili Shangazi? As far as I understand ni serikali ndiyo iliyomfutia kupitia akina Feleshi. Did I miss something.....!!?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

2 Reactions
Reply
Top Bottom