Zitto Kabwe: Nyerere wangu mimi!

Zitto Kabwe: Nyerere wangu mimi!

You must be stupid questioning someone's vision, ambitions or plans!!

Even kids wants to be pilots, doctors, engineers! whats wrong with that??

please format your brain
Wapingaji watapinga kila kitu,watayakataa mpaka majina yao ili kutimiza malengo yao!sijui kama Zitto amekosana na chama au wanachama ?naona chuki zimepitiliza!
 
This ends up talking more about Zitto than Nyerere.
You nail it Kiranga!Mr Zitto was simply celebrating Mwalimu's life highlighting his own experience during Mwalim's era.We should have focused on that but see where the discussion is heading now!
 
Mbona kila kitu anamtaja mama Shida Salum pekee? Huyo baba mzee Kabwe vipi? Yeye kama anautaka uongozi wa juu ajue hakuna cha kuficha juu ya maisha yake. Hata kama mzee aliachia ngazi kwa tabia mbovu za mama aweke hapa hadharani.

Mmeshindwa kwenye siasa sasa hivi mnataka kuzungumzia maisha binafsi ya familia ya Zitto tena hamna uhakika.
 
You nail it Kiranga!Mr Zitto was simply celebrating Mwalimu's life highlighting his own experience during Mwalim's era.We should have focused on that but see where the discussion is heading now!

Sasa wewe ukisoma hio post ya Zitto, imemwongelea zaidi Nyerere au Zitto.
Usijibu haraka tulia kwanza.
 
hii ya kuzungusha mkono juu ya kichwa kugusa sikio ili uingie darasa la kwanza, iliishia miaka ya mwanzo ya 1970's!!! huyu wa 1980's kakopy na kupest kunogesha story!!!!
 
Wako kwenye njia sahihi yakupambana na mkoloni mweusi kaburu fisadi maharamia wanyonyaji magaidi majangili wahujumu uchumi na wanaoiua miili ila hawawezi kuziua roho yaani CCM. Wakati wewe uko kwenye njia yakumtetea huyo ccm ambaye nimeeleza sifa zake hapo juu wewe nikibaraka.
mtu asubuhi anajifanya mjamaa wa kweli wa kukumbuka hisani ya mwalimu wakati ule - Elimu bure, Haki sawa kwa wote nk Then jioni yupo na mafisadi wanagonga glass huku wakipanga mikakati ya kuua upinzani - huyo mtu ni hatari sana.
 
You must be stupid questioning someone's vision, ambitions or plans!!

Even kids wants to be pilots, doctors, engineers! whats wrong with that??

please format your brain

Povu Povu Povuuuuu!!!!! kwani kusema Nyerere alisema hivyo ni kosa??!!kwani si kweli Nyerere alikuwa na VISION hiyo??!!
 
nimependa sana hii speach lakini mwalimu nyerere akuwa msaliti na nyuso mbili kama wewe unajifanya mpinga mafisadi lakini hao unaowapinga unakaa nao na kura nao pesa za wizi na kuandaa nao mikakati ya kuvuruga upinzani kisa umimi mwalimu akuwa mbinafsi hakutaka madaraka kama unavyotaka wewe kuongoza chadema kwa kutumia njia ya kuvuruga chama mimi kwa wewe hauniongopei wewe ni mamluki ni mnafiki na ni muongo acha kuraghai watanzania badilika rudi kundini omba wakusamehe
 
Mmeshindwa kwenye siasa sasa hivi mnataka kuzungumzia maisha binafsi ya familia ya Zitto tena hamna uhakika.

Kwani hii topic anazungumzia nini zaidi ya maisha yake binafsi? Sasa akihojiwa kuhusu alilolianzisha inakuwa nongwa? He
 
Hii tabia ya wanasiasa kuonea ufahari umasikini imeanzaje?
 
Dah!
Post ni nzuri na inatukumbusha tulikotoka na vision za baba wa taifa katika usawa wa binadamu kama moja ya misingi mikuu.
Nakumbuka pia tulikuwa JKT Bulombora na watoto wa kina Mzindakaya tulifoleni kwenye ugali bila kubaguliwa chini ya kina afande Kaitira na kina Nyangusi.
Zitto alitaka tu kuonyesha huu usanii unaoimbwa na viongozi wetu kuwa wanamuenzi mwalimu. Ukiwauluza watoto wao wanasoma shule gani ili uone huo usawa!
Wanaimba kuanzisha shule za kata ambazo kiuhalisia ni shule za daraja la chini sana,lengo lao ni nini watawala wetu hawa? Ni kuandaa watoto wao kuendelea kukalia madaraka!
Nani atamaliza Nyakitondo secondary school then akutane na product ya UK siku ya interview ya kazi na aweze kushinda?
Zitto uko sawa kabisa.......mnyonge mnyongeni haki yake mpeni!
 
Kwenye maelezo yako bwana zito kiswahili nacho Shida KAPTURA au KAPTULA ungefanya marekebisho ingekuwa vyema
 
Usituletee unahii wako hapa! Hivyo ni vitu viwili tofauti unavyo vizungumzia wewe.

Sent from my SM-G800H using Tapatalk

Acha ushabikii mkuu,usipende kudanganywa na ilhali anayekudanganya anajua kuwa anakudanganya.Atakudharau.
We kama mtu alisema alisoma kwa sababu alikulia kwa babu,aliyekuwa kiongozi japo hakujua kusoma na kuandika na leo aseme alisomeshwa level hiyo hiyo ya msingi na alipelekwa shule na mama yake atuacha kupata shaka na kuomba kumbukumbu ziwekwe sawa?
Sina shida na Zitto,ila kanikanganya kidogo kwenye hizo storyy mbili.
 
Nyerere hakuwa na price Tag Mgongoni kwake! Wengi walijaribu kumrubuni lakini walishindwa! Nyerere alipinga siasa za ukabila na ukanda kwa nguvu zote! Nyerere alikuwa na msimamo thabit hakuyumbishwa hata siku moja! Nyerere hakutumiwa na Makaburu weupe wala weusi alikuwa anawapa za uso! Zile Transactions za Ujerumani plus Deals za Kuvuta fedha za EPA kwa Ballali, ukiongezea na Ukimya wa Buzwagi saga plus Matrillions za Uswis zinamfanya ZZK kuonekana kikaragosi cha mtoto wa kindagaten Mbele ya Nyerere... Acheni Kumtusi Baba wa Taifa... RIP Mwalimu
 
Nyerere hakuwa na price Tag Mgongoni kwake! Wengi walijaribu kumrubuni lakini walishindwa! Nyerere alipinga siasa za ukabila na ukanda kwa nguvu zote! Nyerere alikuwa na msimamo thabit hakuyumbishwa hata siku moja! Nyerere hakutumiwa na Makaburu weupe wala weusi alikuwa anawapa za uso! Zile Transactions za Ujerumani plus Deals za Kuvuta fedha za EPA kwa Ballali, ukiongezea na Ukimya wa Buzwagi saga plus Matrillions za Uswis zinamfanya ZZK kuonekana kikaragosi cha mtoto wa kindagaten Mbele ya Nyerere... Acheni Kumtusi Baba wa Taifa... RIP Mwalimu

Kweli yako nyerere hakubagua kati ya msukuma na mnyamwezi, lakini Jeshini aliwajaza wana Musoma kibao. Na pia alikuwa mkatoliki sana.
 


Zitto na Demokrasia

Nyerere Wangu Mimi!


Mwaka 1984 nilianza darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Kigoma, katika mji wa Kigoma. Nakumbuka kupelekwa Shule siku ya kwanza na mama yangu mzazi Bi Shida Salum (Mungu amrehemu) nikiwa sina viatu yaani pekupeku wala begi la mkononi, nilikuwa nimebeba mfuko wa nailoni. Nakumbuka usiku wa kuamkia siku ya kwanza kwenda shule, sikulala kwa furaha na hamu ya kuwa msomi, nilijisikia fahari kuanza shule japokuwa sikuwa na kitu chochote cha zaida zaidi ya kaptula ya shule na shati liloshonwa kwa kitambaa cha sanda. Pia nilianza shule nikiwa nimechelewa kwa mwaka mmoja maana wenzangu walianza wakiwa na miaka 7. Mwaka 1983 nilipopelekwa shule mkono wangu haukuweza kushika sikio upande wa pili, ambacho kilikuwa kipimo cha kuandikishwa darasa la kwanza.

Hali ya maisha wakati huo ilikuwa mbaya sana. Nakumbuka kwenda shuleni nikiwa sina kitu tumboni au siku nzima nilikunywa uji usio na sukari. Uji wenyewe ulikuwa ni wa unga wa njano uliotokana na mahindi ya njano ambayo tuliambiwa nchi yetu ililetewa kama msaada kutoka nchini marekani.

Shule yetu kama zilivyokuwa shule nyingi za wakati huo hatukuwa na madawati ya kutosha na vyumba vya madarasa vilikuwa vichache sana. Ilikuwa ni kawaida kwa wadogo (darasa la kwanza mpaka la tatu) kusomea chini ya mwembe na kukaa juu ya matofali. Hali hiyo ilipelekea kaptura yangu ya shule kuwekwa viraka vingi maana ilikuwa inachanika mara kwa mara. Nyakati nyingine ilibidi kwenda shuleni na shati likiwa halijakauka hasa siku za alhamis, siku ya usafi na iwapo nikiwa zamu ya mchana kwani nilikuwa nina shati moja tu tena lililotokana na kitambaa cha sanda.

Kwa dhahiri, watoto wa masikini na matajiri tulikuwa shule moja, darasa moja hata wote kukaa kwenye matofali. Watoto watawala na watawaliwa tulicheza mpira pamoja, kuruka dana na hata kuruka kamba. Hatukujisikia wanyonge kwa sababu hatuna viatu au kuvaa kaptura zenye viraka na mashati ya sanda. Kamwe sikumbuki kudharauliwa shuleni sababu ya uduni wa maisha yangu. Heshima ilitokana na uwezo wako darasani na kupitia hilo nilipata marafiki wa kutoka madaraja yote ya maisha. Nakumbuka mtoto wa Mkurugenzi wa Maendeleo Mkoa wa Kigoma ndugu Daniel Masanja ndiye alikuwa rafiki yangu wa karibu na kwa kuwa sikuwa na hata pesa ya kununua bajia wakati wa mapumziko, yeye alikuwa ananinunulia.

Huko baadaye, ada yangu ya kidato cha kwanza ililipwa na Mzee Sebastian Kasomi ambaye mwanaye Kasomi Mabula alikuwa rafiki yangu mkubwa mara alipohamia shuleni kwetu akitokea mjini Shinyanga. Mzee Kasomi alikuwa Mkuu wa idara ya Kodi ya Mapato mkoani Kigoma.

Licha ya uduni wa maisha watoto wengi tuliishi kwa matumaini makubwa sana. Mwalimu wetu Mkuu ndg. Daniel Andulile alikuwa mkali sana kwa watoto wote bila kujali daraja la maisha la wazazi wao. Alikuwa anatucharaza viboko kwa makosa na utundu bila ubaguzi. Alisisitiza sana kusoma kwa bidii ili kujenga Taifa. Dhana hii ya kujenga Taifa iliingizwa kwenye akili zetu na sisi kumeza bila kujali maana yake. Wakati mwingine tulikuwa tunarudi nyumbani huku tukijadili kitoto kuwa tunajenga Taifa. Kila siku mwendo wa kilometa Sita kwenda na kurudi shuleni.

Elimu hii isiyo ya kibaguzi sasa najua ilitokana na sera za Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Jitihada zangu darasani ndio ziilikuwa kipimo cha utu wangu na sio uwezo wa kiuchumi wa wazazi wangu.. Elimu iliyompa fursa sawa za kuendelea na kusonga mbele mtoto aliyekuwa kigoma, kantalamba au Dar es salaam. Elimu iliyokuza ndoto, kuinua ari na kujenga matumaini ya kila mtoto wa kitanzania. Elimu iliyovunja na kusambaratisha matabaka ya kiuchumi na dhamana. Elimu iliyojenga uzalendo na hamasa ya kutumikia taifa letu kwa misingi ya haki, uadilifu na upendo.

Sikuwahi kukutana na Mwalimu Nyerere isipokuwa niliwahi kumwona akiwa ndani ya gari nikiwa nimepanga mstari barabarani alipofanya ziara mkoani kwetu mwaka 1987 nikiwa darasa la nne. Lakini nilikuwa kama ninaishi naye kutokana na namna nilivyotaka kuwa kama yeye. Nikiwa darasa la pili nakumbuka katika mkebe wangu ( mathematical set) mkuu kuu niliweka picha ya kukatwa kutoka kwenye gazeti ya Mwalimu na Kawawa. Na nilijisikia fahari kuwa na picha zao, mara zote nilipokuwa nafungua mkebe kutoa kalamu nilijisemea kimoyomoyo, "siku moja nitakuwa kama wewe"

Licha ya maisha magumu tuliyokuwa tunaishi, maisha ya kupanga mawe kwenye mstari wa kununua mahitaji muhimu kama sukari, sabuni na mafuta kutoka duka la ushirika, maisha ya kushindia uji wa yanga na kutembea mwendo mrefu kwenda shuleni, niliishi kwa imani kubwa kuwa mimi na watoto wengine tupo sawa. Usawa katika kupata elimu, usawa katika kucheza na usawa katika ndoto na matumaini. Nimemaliza elimu ya Chuo Kikuu, ndoto niliyoruhusiwa kuwa nayo kwa sababu ya sera za Ujamaa, za Mwalimu Nyerere.

Ujamaa haukuwa katika usawa wa elimu tu ambapo kila mtoto alipata elimu bure na bora katika Shule za umma bila ubaguzi bali pia namna jamii iliishi. Mtoto alikuwa analelewa na jamii nzima. Ukifanya makosa mtaani mzazi yeyote anakuadhibu ili kukurekebisha. Ukifanya jambo jema, mzazi yeyote anakupongeza.

Mwaka 1985 mwezi Novemba nilipokuwa natoka shuleni, karibia na Benki ya Taifa ya Biashara Tawi la Obed Katikaza, nilikutana na Mama Colleta Furugunya tuliyekuwa tunaishi mtaa mmoja na nikimwita bibi Colleta. Aliponiuliza matokeo yangu ya mtihani wa kumaliza muhula wa pili wa darasa la pili kwa kujiamini nikampa karatasi yangu ya matokeo. Nilikuwa nimeshika nafasi ya tatu darasani nyuma ya Ramadhan Kalukula na Haki Manyaga. Bibi Colleta alinishika mkono mpaka duka la Viatu, Bora Shoes na kuninunulia jozi yangu ya kwanza ya viatu. Viatu vile viliitwa Asante Salim, aliyekuwa Waziri Mkuu wa mwisho wa Mwalimu Nyerere ambaye alikuwa anajaribu kubadili hali mbaya iliyokuwepo. Hivyo ndivyo nilivyopata viatu vyangu vya kwanza vya shule. Shukrani kwa sera nzuri ya ujamaa, mshikamano na upendo.

Hizo ni enzi.

Chanzo: Zitto Kabwe blog

My Take:
Najua kuna watu mtakaopinga kwa maslahi yenu binafsi, ila hapa ni ukweli usiokuwa na itikadi!

 
Zitto amenikumbusha enzi zile wakati ambapo watoto wa mkuu wa mkoa/wilaya walisoma shule moja na watoto wa walalahoi na tuliheshimiana kwa uwezo wa kichwa darasani!
 
ZZK.
UNATAMANI MAISHA AMBAYO WOTE TUNAYATAMANI. lakini kuna jinsi ambavyo wengi humu hawataelewa kwa sababu mambo uliyoyaeleza kwa wengine ni hadithi tuu na historia ambayo hawajawahi kuishuhudia. umeorodhesha UZURI WA KUWA NA USAWA BAINA YA WANAJAMII na hilo hata mimi nalitamani sana. lakini kwa namna ya kifasihi ambayo mbururas wengi humu wanaweza wasielewe, umeelezea mateso na ugumu wa maisha ambao watanzania tuliupitia kipindi cha mwalimu nyerere. kuvaa viraka,kusomea chini ya miti, kutokuwa na viatu na kula unga wa yanga. hili watu hawataliona kutoka kwenye andiko lako maana wengi wao hawana akili hiyo.
by the way. you might be the one and only modern politician to live you dreams and exercise you preaches. waliobaki wooote ni chenga tuu
 
Back
Top Bottom