Zitto Kabwe: Nyerere wangu mimi!

Zitto Kabwe: Nyerere wangu mimi!

Kama kumbukumbu zangu ziko sawa,
Zitto alisema alikulia kwa babu yake mzaa mama na alijifunza kusoma na kuandika kabla ya kwenda shule ili kumsaidia babu kusoma barua kwani babu hakujua kusoma na kuandika.
Leo anasema alisoma shule ya msingi na alipelekwa na mama yake mzazi,
Sasa hapa kuna mchanganyiko kidogo,kuhusu alisomea kutoka kwa babu au wazazi ?
NB Isije kuwa tunapewa false stories for hidden reasons.
 
You must be stupid questioning someone's vision, ambitions of plans!!

Even kids wants to be pilots, doctors, engineers! whats wrong with that??

please format your brain

Uko sahihi mkuu... mtoto anapolala anaiombea midoli yake ili aikute kesho...yuko sahihi kama zitto tu, na kama wewe tu!! Tatizo lenu ni kulazimisha akili za kitoto wakubwa wazikubali!! Mswahili kutunaka kwa kiingereza mara zote inaonyesha uzembe wa akili ya huyo mtukanaji!! "Mzembe wa akili"!!......
 
Anasema "NJIANI TULIKUWA TUKIJADIRI KITOTO KUWA TUNAJENGA TAIFA",

Sasa hivi "WANAJADIRI KIKUBWA KWAMBA WANAJENGA MATUMBO"!!!!

Safi sana Mh. Zitto nimekuelewa vyema!! Piga dili Mkuu upunguze machungu ya kutembea peku enzi hizo!!
 
Robat0873398 said:
Dah! Sasa nimeanza kuamini yanayosemwa juu ya huyu jamaaa.

Anasema alikua akiangalia picha kimoyomoyo anasema siku moja nitakua kama wewe sasa sijui kuwaje.
 
Mbona kila kitu anamtaja mama Shida Salum pekee? Huyo baba mzee Kabwe vipi? Yeye kama anautaka uongozi wa juu ajue hakuna cha kuficha juu ya maisha yake. Hata kama mzee aliachia ngazi kwa tabia mbovu za mama aweke hapa hadharani.
 
Makala yako imenigusa hata mimi nidhani tupo wengi sana ambao tulisoma bila ya kuvaa viatu tulipokuwa shule ya msingi, ila kwakuwa fursa zilikuwa ni sawa kati ya mtoto wa mwenye cheo na wa maskini(hakukuwa na twisheni wala St schools) ilitufanya tusome kwa uchungu, Mimi nilipenda sana kuwa fundi magari ilinifanya nipende sana somo la sayansi na hesabu, na vilevile nilipenda kujua maeneo mbalimbali ya Tanzania, Afrika na Dunia ilinibidi niibe atlas shuleni nilipokuwa monita darasa la tatu ilimradi tu niweze kusoma maeneo mbalimbali ya dunia hii.
Asante JK Nyerere ulijenga nchi yenye usawa.


Mwaka 1984 nilianza darasa la kwanza katika Shule ya Msingi Kigoma, katika mji wa Kigoma. Nakumbuka kupelekwa Shule siku ya kwanza na mama yangu mzazi Bi Shida Salum (Mungu amrehemu) nikiwa sina viatu yaani pekupeku wala begi la mkononi, nilikuwa nimebeba mfuko wa nailoni.

Nakumbuka usiku wa kuamkia siku ya kwanza kwenda shule, sikulala kwa furaha na hamu ya kuwa msomi, nilijisikia fahari kuanza shule japokuwa sikuwa na kitu chochote cha zaida zaidi ya kaptula ya shule na shati liloshonwa kwa kitambaa cha sanda. Pia nilianza shule nikiwa nimechelewa kwa mwaka mmoja maana wenzangu walianza wakiwa na miaka 7. Mwaka 1983 nilipopelekwa shule mkono wangu haukuweza kushika sikio upande wa pili, ambacho kilikuwa kipimo cha kuandikishwa darasa la kwanza.

Hali ya maisha wakati huo ilikuwa mbaya sana. Nakumbuka kwenda shuleni nikiwa sina kitu tumboni au siku nzima nilikunywa uji usio na sukari. Uji wenyewe ulikuwa ni wa unga wa njano uliotokana na mahindi ya njano ambayo tuliambiwa nchi yetu ililetewa kama msaada kutoka nchini marekani.

Shule yetu kama zilivyokuwa shule nyingi za wakati huo hatukuwa na madawati ya kutosha na vyumba vya madarasa vilikuwa vichache sana. Ilikuwa ni kawaida kwa wadogo (darasa la kwanza mpaka la tatu) kusomea chini ya mwembe na kukaa juu ya matofali. Hali hiyo ilipelekea kaptura yangu ya shule kuwekwa viraka vingi maana ilikuwa inachanika mara kwa mara. Nyakati nyingine ilibidi kwenda shuleni na shati likiwa halijakauka hasa siku za alhamis, siku ya usafi na iwapo nikiwa zamu ya mchana kwani nilikuwa nina shati moja tu tena lililotokana na kitambaa cha sanda.

Kwa dhahiri, watoto wa masikini na matajiri tulikuwa shule moja, darasa moja hata wote kukaa kwenye matofali. Watoto watawala na watawaliwa tulicheza mpira pamoja, kuruka dana na hata kuruka kamba. Hatukujisikia wanyonge kwa sababu hatuna viatu au kuvaa kaptura zenye viraka na mashati ya sanda. Kamwe sikumbuki kudharauliwa shuleni sababu ya uduni wa maisha yangu.

Heshima ilitokana na uwezo wako darasani na kupitia hilo nilipata marafiki wa kutoka madaraja yote ya maisha. Nakumbuka mtoto wa Mkurugenzi wa Maendeleo Mkoa wa Kigoma ndugu Daniel Masanja ndiye alikuwa rafiki yangu wa karibu na kwa kuwa sikuwa na hata pesa ya kununua bajia wakati wa mapumziko, yeye alikuwa ananinunulia.
Huko baadaye, ada yangu ya kidato cha kwanza ililipwa na Mzee Sebastian Kasomi ambaye mwanaye Kasomi Mabula alikuwa rafiki yangu mkubwa mara alipohamia shuleni kwetu akitokea mjini Shinyanga. Mzee Kasomi alikuwa Mkuu wa idara ya Kodi ya Mapato mkoani Kigoma.

Licha ya uduni wa maisha watoto wengi tuliishi kwa matumaini makubwa sana. Mwalimu wetu Mkuu ndg. Daniel Andulile alikuwa mkali sana kwa watoto wote bila kujali daraja la maisha la wazazi wao. Alikuwa anatucharaza viboko kwa makosa na utundu bila ubaguzi. Alisisitiza sana kusoma kwa bidii ili kujenga Taifa. Dhana hii ya kujenga Taifa iliingizwa kwenye akili zetu na sisi kumeza bila kujali maana yake. Wakati mwingine tulikuwa tunarudi nyumbani huku tukijadili kitoto kuwa tunajenga Taifa. Kila siku mwendo wa kilometa Sita kwenda na kurudi shuleni.

Elimu hii isiyo ya kibaguzi sasa najua ilitokana na sera za Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Jitihada zangu darasani ndio ziilikuwa kipimo cha utu wangu na sio uwezo wa kiuchumi wa wazazi wangu.. Elimu iliyompa fursa sawa za kuendelea na kusonga mbele mtoto aliyekuwa kigoma, kantalamba au Dar es salaam. Elimu iliyokuza ndoto, kuinua ari na kujenga matumaini ya kila mtoto wa kitanzania. Elimu iliyovunja na kusambaratisha matabaka ya kiuchumi na dhamana.

Elimu iliyojenga uzalendo na hamasa ya kutumikia taifa letu kwa misingi ya haki, uadilifu na upendo.
Sikuwahi kukutana na Mwalimu Nyerere isipokuwa niliwahi kumwona akiwa ndani ya gari nikiwa nimepanga mstari barabarani alipofanya ziara mkoani kwetu mwaka 1987 nikiwa darasa la nne. Lakini nilikuwa kama ninaishi naye kutokana na namna nilivyotaka kuwa kama yeye. Nikiwa darasa la pili nakumbuka katika mkebe wangu ( mathematical set) mkuu kuu niliweka picha ya kukatwa kutoka kwenye gazeti ya Mwalimu na Kawawa. Na nilijisikia fahari kuwa na picha zao, mara zote nilipokuwa nafungua mkebe kutoa kalamu nilijisemea kimoyomoyo, “siku moja nitakuwa kama wewe”

Licha ya maisha magumu tuliyokuwa tunaishi, maisha ya kupanga mawe kwenye mstari wa kununua mahitaji muhimu kama sukari, sabuni na mafuta kutoka duka la ushirika, maisha ya kushindia uji wa yanga na kutembea mwendo mrefu kwenda shuleni, niliishi kwa imani kubwa kuwa mimi na watoto wengine tupo sawa. Usawa katika kupata elimu, usawa katika kucheza na usawa katika ndoto na matumaini. Nimemaliza elimu ya Chuo Kikuu, ndoto niliyoruhusiwa kuwa nayo kwa sababu ya sera za Ujamaa, za Mwalimu Nyerere.

Ujamaa haukuwa katika usawa wa elimu tu ambapo kila mtoto alipata elimu bure na bora katika Shule za umma bila ubaguzi bali pia namna jamii iliishi. Mtoto alikuwa analelewa na jamii nzima. Ukifanya makosa mtaani mzazi yeyote anakuadhibu ili kukurekebisha. Ukifanya jambo jema, mzazi yeyote anakupongeza.

Mwaka 1985 mwezi Novemba nilipokuwa natoka shuleni, karibia na Benki ya Taifa ya Biashara Tawi la Obed Katikaza, nilikutana na Mama Colleta Furugunya tuliyekuwa tunaishi mtaa mmoja na nikimwita bibi Colleta. Aliponiuliza matokeo yangu ya mtihani wa kumaliza muhula wa pili wa darasa la pili kwa kujiamini nikampa karatasi yangu ya matokeo.

Nilikuwa nimeshika nafasi ya tatu darasani nyuma ya Ramadhan Kalukula na Haki Manyaga. Bibi Colleta alinishika mkono mpaka duka la Viatu, Bora Shoes na kuninunulia jozi yangu ya kwanza ya viatu. Viatu vile viliitwa Asante Salim, aliyekuwa Waziri Mkuu wa mwisho wa Mwalimu Nyerere ambaye alikuwa anajaribu kubadili hali mbaya iliyokuwepo. Hivyo ndivyo nilivyopata viatu vyangu vya kwanza vya shule. Shukrani kwa sera nzuri ya ujamaa, mshikamano na upendo.

Hizo ni enzi.


Zitto Z. Kabwe

Chanzo: Zitto na Demokrasia | Zitto na Demokrasia
 
Nakupenda CHADEMA,nitakupigania na kukueneza popote pale nitakapokuwepo.
Mungu nisaidie.
 
You must be stupid questioning someone's vision, ambitions of plans!!

Even kids wants to be pilots, doctors, engineers! whats wrong with that??

please format your brain
Umetumia kiingera ili kuficha udhaifu wa hoja yako, lini watanzani utumwa wa kichwani utapungua kama sio kuisha? kiingereza chenyewe ulichoandika duh! mlemle na nilivyokuhisi!
 
safi sana zitto
Hatutomtofautisha ZK na mafisadi kwa kutoa simulizi ambazo kila mtu wa makamo yake au aliyemzidi anaweza kuelezea hadithi hizo, Ila tutamtofautisha kwa matendo yake yaliyotofauti na mafisadi!

Hapo safi kwa lipi?? kwa kutambua kuwa enzi hizo kulikuwa na mfumo mzuri uliojengwa na muasisi wa Taifa hili au kwa kushindwa kuishi kama muasisi wa Taifa hili?. Kama ni hadithi kila mtu anaweza kuhadithia, isipokuwa kuna wale wenye fursa hata za kupata sehemu za kusemea kama vyombo vya habari lakini kuna wale ambao ni wazalendo wa kweli hawana hata pakusemea. Kwa mtazamo wako hayo aliyoyaongea hakuna mtu anayeyajua? Unafikiri mafisadi hawayajui?

"Hivi unafikiri chombo cha habari kinapomwalika madharani "Wasira" unazani ni mahitaji ya wasikilizaji na watazamaji kusikia wasira anaongea nini?
 
Uko sahihi mkuu... mtoto anapolala anaiombea midoli yake ili aikute kesho...yuko sahihi kama zitto tu, na kama wewe tu!! Tatizo lenu ni kulazimisha akili za kitoto wakubwa wazikubali!! Mswahili kutunaka kwa kiingereza mara zote inaonyesha uzembe wa akili ya huyo mtukanaji!! "Mzembe wa akili"!!......

umeona eeh, mbavu zangu
 
akina Faizafoxy, Bigshow njoo msome mtu mwenye akili zake anavyomwona Nyerere, nyinyi mtabaki peke yenu hata wanenu hawatawaelewa, JK late atabaki kuwa national icon hadi vifo vyenu vinawakuta, u just need to accept that fact or u'll die a hater, kufa una kinyongo na mtu ni kitu kibaya sana.
 
Kama kumbukumbu zangu ziko sawa,
Zitto alisema alikulia kwa babu yake mzaa mama na alijifunza kusoma na kuandika kabla ya kwenda shule ili kumsaidia babu kusoma barua kwani babu hakujua kusoma na kuandika.
Leo anasema alisoma shule ya msingi na alipelekwa na mama yake mzazi,
Sasa hapa kuna mchanganyiko kidogo,kuhusu alisomea kutoka kwa babu au wazazi ?
NB Isije kuwa tunapewa false stories for hidden reasons.
Usituletee unahii wako hapa! Hivyo ni vitu viwili tofauti unavyo vizungumzia wewe.

Sent from my SM-G800H using Tapatalk
 
Mh! Hizi story za mtu kukumbuka details hivyo za darasa la kwanza huwa zinanitia wasiwasi sana. Kuna huyu Zitto Kabwe na January Makamba. Yani hawa wenzetu wanataka kutuaminisha kua wao swala la uongozi walizaliwa nalo kama haki yao na walioteshwa na Mungu na kuandaliwa toka vichanga!

Utakuta story za dhiki na shida, over exaggeration ya truimph over turmoil, overcoming immense obstacles in dire situations to finally emerge the messiahs to lead us to the promised land.


There stories of tribulation and truimph are sure to make the likes of Job, Moses and Jesus envious to say the least.
Wanataka tuwafikire kama wao ni watu pekee sana na waajabu wakati waliyoyapitia kama yana ukweli kuna waTZ wengi sana wamepitia lakini hawatumii kama kete ya kupata kula/kura!

Hehehe ngoja mimi nitakuja na story yangu muone jinsi nilivozaliwa kwenye zizi la ngombe huku nikimsaidia mama yangu kujifungua mimi, nilivoanza kunywa uji wa mchanga na nilipofikisha miaka mi5 nikaanza kulima na kulisha kijiji!
 
Ndugu Zitto, mimi ni mmoja wa wakubwa zako , waliopendezwa na msimamo wako wa kisiasa na how close you are to the public, lakini kitu ambacho mara nyingi kinaniudhi ni wakati unapoleta siasa sa kinafiki za kujikomba na Hayati Mwalimu na kutafuta umaarufu on his legecy.

Kijana Zitto, i will quote you a bit "" Ujamaa haukuwa katika usawa wa elimu tu ambapo kila mtoto alipata elimu bure na bora katika Shule za umma bila ubaguzi bali pia namna jamii iliishi. Mtoto alikuwa analelewa na jamii nzima. Ukifanya makosa mtaani mzazi yeyote anakuadhibu ili kukurekebisha. Ukifanya jambo jema, mzazi yeyote anakupongeza.""

Huo ni uwongo wa hali ya juu sana, tabia za watoto kulelewa na jamii nzima, haikuletwa na UJAMAA wa Nyerere, bali hiyo ndio mila yet toka enzi za kina babu na babu, hata nyerere mwenyewe alilelewa katika mazingara hayo.

Mdogo wangu ZItto napenda kukushauri uwache hii tabia ya kilio cha maish yako ya kusoma kwa taabu, na sifa za ulivyo kuwa na akili shuleni, na namna ulivyokuwa na shida ya viatu. Zitto hiyo ndiyo hali halisi ilivyokuwa kwa watoto wa kitanzania 85% na kama sio 95%, and it was not only unique for you , this story of yours is becoming very boring.

Pia ningekushauri wewe na wengine, tuwe wakweli kuhusu utawala wa Hayati Baba wa Taifa, ni kweli alikuwa na mengi mazuri, na pia halikuwa na mengine mabaya, au siasa yake ya kijamaa zipo sehemu zilizo leta maafa makubwa kwa Umma, mbona hamuzizungumzi ili vizazi vya nyuma wajue ukweli, ile wale watakao taka kuuridisha Ujamaa wawe kujua hayo matatizo na waweze kuutafutia uvumbuzi mzuri.
 
Asante Mkirindi . Unajua hawa jamaa wanaleta siasa za kuiga za kwa akina Obama na kutulisha hapa! Ni hali ya kusikitisha sana wanasiasa wetu vijana kuwa copy cats na kukosa uhalisia wowote. Kwakweli inashtua kuwa hawa watu wanaoiga mpaka hata hotuba, kweli watakua na njia thabiti za kuendelza Taifa au ni uchu tu wa madaraka.

Mzizi wa Mbuyu katoa comment nzito sana ila wasiotafakari hawajamwelewa. Kasema kuwa Nyerere akiwa kijana alikua na ndoto za uhuru na sio kuwa raisi. Hio statement ni nzito sana, kwa mwenye akili atailewa sababu ina maana pana sana nu ku summarize vizuri tofauti ya viongozi wa enzi hizo na hawa wanaotaka uongozi sasa.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom