Zitto Kabwe: Nashauri Waziri Mkuu ahitaji maelezo ya kina kutoka Minjingu kuhusu soko lao la Kenya

Karash

Member
Mar 31, 2016
21
12
Jana Waziri Mkuu alionyesha hasira kubwa kuhusu vifungashio vya kampuni ya Minjingu kuonyesha kuwa mbolea ile imetengenezwa Nairobi Mtaa wa Mombasa.

Moja, kifungashio kuwa na jina la mnunuzi ni jambo la kawaida katika biashara hususan mnunuzi anapotaka kudhibiti wizi. Utaona vifungashio vile ni vya Serikali za Majimbo huko Kenya na mbolea ni ya ruzuku. Hata hivyo; hoja muhimu;

Pili, Minjingu hawana kiwanda Nairobi. Ukitazama mifuko ile ni zaidi ya ' branding ' bali mbolea ile ikiwa Kenya itaonekana imezalishwa huko na hapo kuna hoja kubwa mno ya kodi.

Waziri Mkuu amewataka Minjingu kuomba radhi kwa Rais. Nadhani Serikali ifanye uchunguzi kwa kutumia wataalamu wa kodi za kimataifa ( international taxation experts ). Nashauri Waziri Mkuu ahitaji maelezo ya kina kutoka Minjingu kuhusu soko lao la Kenya na aagize International Tax Unit ya TRA ilitazame jambo Hilo. Kwa uzoefu wangu mdogo na nikiwa mmoja wa waanzilishi wa International Tax Unit nchini kwetu ninahisi kuna suala la ukwepaji kodi katika jambo hili. Waziri Mkuu achukue hatua zaidi ya agizo la msamaha. Uchunguzi ufanyike

 
Naona anazidi kupigilia msumari zaidi! ili waonekane wanakwepa kodi!!
Nafikiri wapewe onyo tu kama alivyopendekeza waziri mkuu
 
Naona anazidi kupigilia msumari zaidi! ili waonekane wanakwepa kodi!!
Nafikiri wapewe onyo tu kama alivyopendekeza waziri mkuu
Kwanza tuwachunguze nia na dhamila yao ili tujilizishe Luna zaidi ya tunachofikili na wao nini wanamaanisha kila jambo lina maantiki
 
Kwa taarifa tu majaribio ya mbolea ya minjingu yamefanyika mengi zaidi kenya kuliko tanzania na yakatoa matokeo mazuri. Kenya ni watumiaji wakubwa wa mbolea ya minjingu kuliko tanzania. Haishangazi kuona wameghushi hii nembo.
 
Kwa taarifa tu majaribio ya mbolea ya minjingu yamefanyika mengi zaidi kenya kuliko tanzania na yakatoa matokeo mazuri. Kenya ni watumiaji wakubwa wa mbolea ya minjingu kuliko tanzania. Haishangazi kuona wameghushi hii nembo.
Waziri Mkuu ana kazi kuibua mambo. Utadhani kama kwenye maeneo hayo palikuwa hakuna Mkuu wa Wilaya ama wa Mkoa ili kubaini hayo. Ni kama sakata la faru John ilivyoibuliwa na Waziri Mkuu. Inavyoonekana akiendelea na ziara za Mikoani ataibua mengi zaidi.

Hata hivi karibuni niliona kibao cha shule moja ya Sekondari ya Kata, imeandikwa www.endallah.be ikiashiria ni tovuti ya Ubelgiji.

Tunamtakia Waziri Mkuu afya njema ili aendelee kuibua madudu zaidi!
 
Hilo tatizo sio lazima ashirikishwe rais. Mengine yaishie kwenye level za wizara.
 
Mh. Waziri Mkuu na Mh. Zitto wote hamko sahihi sana.
tunataka viwanda ili:
  1. vitumie malighafi zetu- wanafanya
  2. vitengeneze nafasi ya ajira- wamefanya
  3. viuze ndani na nje ya nchi- ushahidi huo na kama utakumbuka watanzania hasa wa mikoa ya big five waliikataa mbolea hiyo ya minjigu kwa uchochezi wa kibiashara uliobebwa na wanasiasa wakiwemo wabunge
  4. vilipe kodi- inavyoonekana kodi hapa siyo issue
  5. sasa kwa kuweka kwenye mifuko ikiwa ni utekelezaji wa matakwa ya mteja TABU IKO WAPI?
 
Certificate of origin lazima ionyeshe bidhaa imetengemezwa wapi MADE IN TANZANIA. Unaweza ukawa na mifuko na ikawa na vielelezo kama ni ya Kenya, lakini chini kabisa kwenye hiyo bidha lazima ionyeshe ni wapi imetengenezwa. Hii inasaidia kufuatilia ubora wa bidhaa mpaka mahali ilipo zalishwa na kama imezalisha kwa kutumia malighafi inayo kubalika kimataifa na mfumo unao kubalika. Hata ukienda China na ukataka wakutengenezea bidhaa kama nguo au viatu, unaweza ukaandika maneno yote kama bidhaa hii ni ya kitamzania lakini nyuma kwenye label lazima iandikwe MADE IN CHINA.
 
Mbona madukani kuna pasi radio fridge wala hazionyeshi zimetengenezwa wapi, hao waminjingu kama mteja wao kasema iandikwe ''made in china'' ni poa tu ilimradi katupia hela kwenye account.
 
Certificate of origin lazima ionyeshe bidhaa imetengemezwa wapi MADE IN TANZANIA. Unaweza ukawa na mifuko na ikawa na vielelezo kama ni ya Kenya, lakini chini kabisa kwenye hiyo bidha lazima ionyeshe ni wapi imetengenezwa. Hii inasaidia kufuatilia ubora wa bidhaa mpaka mahali ilipo zalishwa na kama imezalisha kwa kutumia malighafi inayo kubalika kimataifa na mfumo unao kubalika. Hata ukienda China na ukataka wakutengenezea bidhaa kama nguo au viatu, unaweza ukaandika maneno yote kama bidhaa hui ni ya kitamzania lakini nyuma kwenye label lazima iandikwe MADE IN CHINA.


Madeni china utaiona tu kwenye bidhaa ambayo imekidhi viwango vya ubora wa china.

Kama imekidhi viwango vya ubora wa mteja kamwe wachina hawata kukubalia kuandika madeni china wataiacha bila kuonesha imetengenezwa wapi.

Na washawasha!
 
Madeni china utaiona tu kwenye bidhaa ambayo imekidhi viwango vya ubora wa china.

Kama imekidhi viwango vya ubora wa mteja kamwe wachina hawata kukubalia kuandika madeni china wataiacha bila kuonesha imetengenezwa wapi.

Na washawasha!

Nadhani maandishi yako yana pande mbili (nilivyoelewa mimi). Made in China inaweza kuwa bidhaa iliyokidhi ubora wa China, lakini haijakidhi ubora wa kimataifa. Bidhaa hiyo inatakiwa kuuzwa ndani ya China tuu (kisheria) ladba kama nchi inayo agiza bidhaa hiyo imeridhika na viwango vya ubora wa China. Upande mwingine, sio kweli kwamba kama mteja ameridhika na ubora wa bidhaa basi wachina hawana haja ya kuandika kwamba bidhaa imetoka kwao. Ukumbuke mnunuzi wa bidhaa husika sio mtumiaji wa mwisho, aliye nunua bidhaa China anaweza kumuuzia mteja, na mteja yule na yeye akaiuza tena, sasa kama kuna tatizi kwenye bidhaa hiyo (sumu) wachunguzi watafuatilia mpaka wapi. Mfano mbolea ya Arusha, imekutwa na sumu, watu wamekula chakula kilichokuzwa na mbolea ilioandikwa Made In Nairobi Kenya. Wachinguzi watafatilia mpaka wapi na huku unakuta kampuni yenyewe Kenya ni bubu?
 
Zitto hana akili.
Hiyo branding kwa jina la mteja watu huweka bei ya juu sana,kwa sababu unaua statistics za exports kwa nchi husika
Kingine ni kwamba order zote zitakwenda nairobi kwa bei ya juu wakati mtengenezaji anapata bei ya chini
 
Back
Top Bottom