Zitto Kabwe: Mauzo nje kutoka sekta ya Viwanda yameporomoka kwa takribani $272m(Tshs 600bn)

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,278
Mauzo nje kutoka sekta ya Viwanda yameporomoka kwa takribani $272m ( tshs 600bn ) Ndani ya mwaka mmoja tangu Serikali ya awamu ya Tano iingie madarakani wameandika The Citizen wiki iliyopita.

Hii maana yake nini?

Ama uzalishaji viwandani umeshuka au ubora wa bidhaa zetu umeshuka na hivyo kukosa masoko nje. Kwa vyovyote vile na hasa Kama uzalishaji viwandani umeshuka, ina maana kuwa kuna mamia ya Watanzania wamepunguzwa kazi ( retrenched) na hivyo kuongeza watu wasio na kazi ( unemployed) mitaani.

Zaidi ya hapo Serikali itakuwa imepoteza mapato kwa sababu kodi ya wafanyakazi ( PAYE ) inachangia zaidi ya 25% ya mapato yote ya kikodi ya Serikali ya Tanzania. Vile vile wale wanaodaiwa na Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi hawataweza kulipa mikopo Yao.

Serikali inayohubiri Viwanda kila kukicha haina budi kujitathmini kwa kina kwanini mauzo nje ya bidhaa za viwanda yamepungua.

Hivi tumewahi kujiuliza idadi ya kazi ambazo zimepotea au kuzalishwa tangu Novemba 5, 2015?

NB

( by the way, nimesikia kilio cha Watanzania wengi kuhusu makato ya 15% ya kulipa HESLB. Ifahamike kuwa mabadiliko haya yaliletwa kupitia miscellaneous amendments na hayakuja kwenye Kamati ya Bunge husika. Hivyo tutajadiliana na wenzangu kwenye Kamati ili kuona namna ya kupendekeza mabadiliko. Ni Kweli makato ni ya juu mno na wabunge tunapaswa kutazama upya jambo hili).
 
Serikali inayohubiri Viwanda kila kukicha haina budi kujitathmini kwa kina kwanini mauzo nje ya bidhaa za viwanda yamepungua.

Hivi tumewahi kujiuliza idadi ya kazi ambazo zimepotea au kuzalishwa tangu Novemba 5, 2015?
 
mauzo yako juu sema kuna viwanda vinabrand bidhaa za tanzania kama nchi jirani kama kile cha mbolea
Unazungumuzia malalamiko ya wafanyakazi kukatwa 15% ya mikopo waliyochukua bodi hayakupitia kwenye kamati mbona ulikuwa kimya wakati wafanyakazi wanapinga fao la kujitoa au kwa sababu nssf walishakupa rushwa
 
Hii serikali afadhali kuishi kuzimu, Ina kera sana kila siku yanaongea viwanda wakati hakuna mikakati yoyote ya viwanda, ona sasa tuna face unfavourable balance of payment, watu watapunguzwa kwenye ajira. Lakini yapo tu kazi kukimbizana na wapinzana tu.
 
Back
Top Bottom