OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 52,007
- 114,352
Wabunge wa vyama vya upinzani hapa nchini walisusia Bunge kwa sababu kuu tatu. Moja ni Bunge kutoonyeshwa moja kwa moja na Televisheni ya Taifa na pia vituo binafsi vya televisheni, mbili ni matumizi nje ya mpango wa bajeti iliyopitishwa na Bunge na tatu ni Serikali kutokuwa na ‘instruments’ (mwongozo wa kisheria wa utendaji kazi na majukumu) kwa mawaziri.
Hoja hizi ni hoja za msingi sana. Ni Haki ya wananchi kuona moja kwa moja namna wawakilishi wao wanavyofanya kazi. Hatua hii ya serikali kuzuia uwazi huu bungeni ni moja ya dalili za kujenga udikteta nchini.
Kwamba anayepaswa kuonekana moja kwa moja ni mtu mmoja tu; hii ni dalili ya kujenga kitu kinachoitwa “cult personality” yaani mtu mmoja pekee kuabudiwa kama tunavyoona kwa Korea Kaskazini.
Suala la Matumizi kufanyika nje ya Mfumo wa Bajeti ni suala la kisheria. Bajeti inaongozwa na sheria mbalimbali kama vile Sheria ya Fedha ( The Finance Act), Sheria ya Matumizi na Sheria ya Fedha za Serikali ( Public Finance Act). Kuna taratibu za Fedha za Serikali kuhamishwa kutoka fungu moja kwenda fungu jingine au ndani ya fungu husika.
Katika sheria zote hakuna mahala Rais amepewa mamlaka ya kuhamisha fungu lolote lile. Hivyo, hoja iliyotolewa na Kiongozi wa Upinzani Bungeni kuhusu Wizara ya Ujenzi kuongezewa fedha mara nne zaidi ya fedha ilizotengewa na Bunge ni hoja yenye nguvu sana.
Mwalimu Nyerere alipata kusema “ Kuna mambo Rais akifanya, ya hovyo wananchi wakatae, awe Rais, awe Rais square”. Dhana ya Mamlaka (Power) ni dhana ngumu sana, ukilamba bila kuzuiwa utaendelea kulamba tu. Tumzuie Rais kupoka madaraka ya vyombo vingine vya dola na badala yake tumwunge mkono kutekeleza madaraka yake ya Urais tu.