Lady doctor
JF-Expert Member
- Apr 13, 2013
- 8,756
- 7,005
Kuna watu waliona mbali sana tokea mapema.. thread hii ni 2011 ona yanatimia leo 2013..
umesahau kuwa kama lisemwalo lipo na kama halipo laja
Kuna watu waliona mbali sana tokea mapema.. thread hii ni 2011 ona yanatimia leo 2013..
Zitto Kabwe na Dr Kitila Mkumbo ni marafiki wa muda mrefu. Urafiki huo ulianza Chuo kikuu cha Dsm pale ambapo Dr Kitila alimbeba Zitto hadi akafanikiwa kuwa Katibu DARUSO.
Baadaye Zitto akaukwaa ubunge. Makada wa CCM wakatofautiana kuhusu mkataba wa Buzwagi. Wakampa Zitto deal la kulipua akapata umaarufu. Uchaguzi wa Chadema 2009 akambeba Dr Kitila kuwa mjumbe wa kamati kuu kupitia umaarufu wake. Dr Kitila na Zitto ni wajumbe wa kamati hadi sasa.
Chanzo cha kuponzana;
1) Mwaka 2009 Zitto akataka kumvaa Mbowe kabla wazee hawajamshauri atoe kwa (HIARI?) Katika mchakato huo Dr Kitila alimuunga mkono Zitto waziwazi dhidi ya Mbowe. Dr Kitila akasema yeye ni mshauri wa kisiasa wa Zitto. Wote wakakwama.
2) Mapema mwaka huu baada ya Shelembi kufa. Zitto alishirikiana na baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Shinyanga kumteua Shibuda chap chap ndani ya wiki kurithi nafasi ya marehemu (uenyekiti wa Chadema mkoa wa Shinyanga) Hoja ikapelekwa kamati kuu. Zitto, Mama Zitto, Dr kitila na Shilungushela wa shinyanga wakawa ndo watu pekee waliomtetea Shibuda abaki ktk nafasi hiyo. Wajumbe wengi wote wa kamati kuu walimpinga Shibuda. Mapacha hawa nao wakakwama tena. Shibuda akatimuliwa ktk nafasi hiyo.
3) Hivi sasa kuna fununu kuwa mshauri huyo wa Zitto wanatafakari nafasi ya kumpa ikiwemo ukatibu mkuu wa Chama (Nafasi ya Slaa). Je, watafanikiwa? Harakati hizi zinaendelea wakati ambao Dr Kitila anajua uswahiba kati ya Zitto na Jack Zoka (Mkurugenzi mkuu msaidizi wa usalama wa Taifa) na Rostam Aziz zilizowekwa hadharani na gazeti la MwanaHalisi.
Sijapata msimamo wa Zitto na Kitila ktk suala la kutimua madiwani wa Arusha.
Kuna watu wanaona mbali aisee.
Kumbe haya mambo yalishatabiriwa ati?
binafsi nampenda zitto kama mtendaji zaidi kuliko zitto mwanasiasa,ila siwezi unga mkono kila hoja ya kumkosoa.kwasasa issue ni mafuta,ufisadi n.k na sio kuibua upuuzi.kitila ni mtu mwenye nidhamu na maadili ya utawala kijana.
atakayeamini upuuzi huu ni mtu aliyechizika
:smile-big::smile-big::amen: