Zitto Kabwe kugombea Urais wa Tanzania 2025, Jimbo la Ubunge Kigoma mjini anawaachia Vijana wa ACT Wazalendo

Eti Jimbo anawaachia vijana...hivi unaachiaje kitu ambacho hujakishika na huna!?
 
KC Mstaafu wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe amekubali ombi la Mh. Ismail Jussa wa Zanzibar aliyemtaka agombee Urais wa JMT 2025 badala ya kurejea bungeni kama ilivyopangwa.

Zitto Kabwe amekubaliana na ombi hilo na kusema Sasa yuko tayari kuwa Rais wa JMT mnamo Uchaguzi mkuu wa 2025 na kwamba Ubunge anawaachia Vijana kutoka Ngome ya ACT Wazalendo.

My take; Lissu sasa arudi NCCR tu.

=====

Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Zanzibar, Ismail Jussa Ladhu amesema kuwa wao kama Chama katika miaka yao 10 kama Chama chenye usajili wa kudumu, wameweza kujijenga kitaasisi na hivyo wako tayari kuchukua mamlaka ya Nchi Zanzibar na Tanzania bara kwa kumsimamisha Kiongozi wao Mstaafu wa Chama Zitto Kabwe kuwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Jussa ameyasema hayo jana katika sherehe za kitaifa za maadhimisho ya miaka 10 ya ACT yaliyofanyika mkoani Kigoma ambapo amebainisha kuwa Zitto anayo nafasi kubwa ya kukivusha chama hicho na kuchukua uongozi wa Nchi.

“Tunajua Mnamtaka Zitto kuwa Mbunge wenu hapa mjini kwenye uchaguzi ujao lakini sisi kama chama tunataka atuvushe kwenye nafasi ya uraisi wa Tanzania kutokana na uwezo na nafasi aliyonayo na tunaomba mtoe baraka zenu kufanikisha hilo” — Jussa.

Kwa upaande wake kiongozi wa Chama Mstaafu, Zitto Kabwe amesema kuwa “Niko tayari na nimejianda kimaarifa na kusaikolojia kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wakati wowote mkinihitaji niko tayari, kuhusu ubunge hakuna shida wakina Nondo wapo na Vijana wengine wakati wowote tupo tayari kuleta mabadiliko ya ya Nchi yetu, mimi ni mstaafu napokea amri kutoka nyie Viongozi wangu”.

Zitto kabwe mbali na hayo amesema miaka 10 ya kuanzishwa kwa Chama hicho inatosha kukifanya kuwa Chama kikubwa Nchini na cha Watu hivyo mpango wa miaka 10 ijayo ni mkakati wa kuhakikisha Chama kinashika dola.

Kuhusu mpango wa Chama kumtaka kugombea Urais wa Tanzania katika uchaguzi mkuu wa 2025, Zitto alisema kuwa alijipanga kugombea Ubunge jimbo la Kigoma Mjini lakini Chama kinayo maamuzi na kama kitaamua hivyo basi hatokuwa na kipingamizi.

Millard Ayo

Zitto alishwauzia Chama Wazenji .... Naona Wazenji wanapiga somo huko Zanznzibar usiku na mchana. Wamesahau kuwa hiki chama pia kipo bara ambako ndiko waliko wengi wetu. Bila pesa ya Abdul .... kampeni za Zitto zitakuwa kama zile za Membe (RIP). Nakumbuka Membe alikuwa anahutubia watu 10 na jukwaa lake lilikuwa ni sawa na dining table!!
 
Ameshaahidiwa kitengo huko serikalini kupitia tiketi ya kugombea urais kama ilivyokuwa kwa wale wamama wawili waliogombea urais 2020
 
Back
Top Bottom