Zitto Kabwe: Bei ya vyakula imeongezeka, kipato kimepungua

Casuist

JF-Expert Member
Jul 23, 2014
1,189
2,970
Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe akiwa kwenye uzinduzi wa ripoti ya TWAWEZA inayozungumzia wananchi kukumbwa na njaa, amesema bei ya chakula imeongezeka huku uchumi kuendelea kubana kwa wananchi.

Amesema pia gesi ya kupikia imepanda hivyo kuna haja ya serikali kuchukua hatua ili kuwasaidia wananchi ikiwemo kuchukua chakula kwenye ghala la taifa kama kipo na kukiingiza kwenye maeneo ambayo chakula ni ghali ili kupunguza pressure ya bei.

 
Kweli ndg.... Juzijuzi unga nilinunua unga.....1800/-kwa kilo.... Leo hii nimenunua tshs 1900...dukani.... Kwa kilo..
 
Tangu ameingia madarakani rais Magufuli amekuwa akijinasibu kuwa yeye ni rais wa wanyonge, kauli hii imekuwa ikinishangaza sana, hivi rais Magufuli ni rais wa wanyonge wapi? Tangu ameingia madarakani hao wanyonge wamenufaika vipi na uongozi wake.

Rais aliingia madarakani wanyonge wakinunua sukari 1800/= leo hii 3000/=, unga 800/= leo hii 1200/=~1,500/= hao wanyonge anaowasaidia ni wa nchi gani?

Kipindi cha nyuma kulikuwa na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa wakulima lakini tangu aingie madarakani ruzuku hiyo haipo, watoto wa wanyonge waliokuwa waingie vyuo vikuu hawana mikopo wapo nyumbani wamekaa, kuna wanyonge wamemaliza vyuo vikuu lakini mpaka sasa hawana ajira na hawajui hatma zao, rais ameua elimu kwenye shule za kata ambazo watoto wa wanyonge wanasoma.
Kwa ufupi ni kwamba ameongeza umaskini kwa jamii, lakini cha ajabu kila akisimama anajinasibu yeye ni rais wa wanyonge, wanyonge wapi hao.
 
Ilo la Ruzuka upo sahii sana mkuu.

Kipindi cha Rais wetu mpendwa hata wafugaji wa samaki walipata chakula cha ruzuku. Yani kilo ya floating pellets iliyokuwa ikiuzwa sh 3000. Wafugaji walinunua kwa 500. Yan serkali ililipa 2500. Ni hii ilikuwa kila mwaka kinatoka mara mbili.

Ila awamu ya Raisi wa Wanyonge mnyongeni kitu kama hiki kutokea ni ndoto.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom