Zitto Kabwe atakuwa anapata shida sana

Zitto Kabwe atakuwa anapata shida sana

mtafuta-maisha

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2016
Posts
1,982
Reaction score
2,934
Katika watu waliosoma wakaelimika na wenye upeo wa kujua na kuelewa mambo mengi katika kizazi hiki hapa Tanzania, Zitto ni mmoja wa watu hao.

Nikisiliza michango yake bungeni na hata akifanyiwa mahojiano, jinsi anavyojenga hoja na kueleza mambo utagundua ana upeo mkubwa wa kuelewa na kuchambua mambo na ni mtu ambaye anapenda kusoma sana.

katika kujenga hoja kwake uwa hatumii maneno ya kuudhi wala kutukana na hii ni jambo ambalo hata akiwa anaibana serikali bungeni uwa spika anakosa sababu ya kumnyamazisha maana spika akiongea tu Zitto atakaa kimya na kukaa mpaka spika amruhusu kuendelea.

Lakini namuonea huruma maana mambo anayoongea bungeni ni wabunge wachache wanaomuelewa maana wengi ni wazee wa ndiyo mzee akiwachambulia mambo hata hawaelewi, bado wananchi wa kawaida ambao akiwachambulia ripoti ya CAG akawatajia na Tillion hawapati hata picha ya ni pesa kiasi gani hiyo.

Pia Zitto ni mtu ambaye ana mtazamo huru na nadhani ndicho kinamfanya aonekane msaliti kwakuwa haongozwi na uchama zaidi bali mawazo huru.

Nimetokeo kupenda sana kusikiliza michango yake huyu jamaa.

Ni mtazamo wangu tu.
 
Tatizo lake ni moja tuu haaminiki. hata mie nampenda Sana.
 
Tatizo lake ni moja tuu haaminiki. hata mie nampenda Sana.
Ana fikra huru siyo mtu ambaye sote tulalie kushoto haya huhoji unalala tu, sote tulale kulia huhoji unalala tu, hata wapinzani wakiwa hivyo kutakuwa hakuna tofauti na CCM maana nao mwenyekiti akisema hili sawa bungeni watahakikisha linapita.
 
Back
Top Bottom