SI KWELI PreGE2025 Zitto Kabwe asema CHADEMA imekufa kisiasa

SI KWELI PreGE2025 Zitto Kabwe asema CHADEMA imekufa kisiasa

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Source #1
View Source #1
SIKWELI_ZITTO_5MEI25.jpg
 
Tunachokijua
Zitto Kabwe ni mwenyekiti mstaafu wa chama cha ACT- Wazalendo aliyehudumu nafasi hiyo kwa muongo mmoja. Zitto alihamia ACT- Wazalendo mwaka 2015 baada ya kuvuliwa uanachama ndani ya CHADEMA kutokana na kukiuka katiba ya chama hicho kwa kupeleka mahakamani migogoro ambayo ilitakiwa kushughulikiwa ndani ya chama kwa mujibu wa katiba.

Kupitia tiketi ya CHADEMA Zitto aliwahi kuwa mbunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini mwaka 2005 mpaka 2015. Akiwa kiongozi mstaafu ndani ya ACT- Wazalendo ameendelea kuwa mwanachama muhimu ndani ya chama hicho kutokana na uzoefu wake wa muda mrefu katika siasa za Tanzania.


Madai

Kumekuwapo na chapisho linalosambazwa mtandaoni likidaiwa kuchapishwa na Jambo TV likirejea ujumbe unaoonekana kuchapishwa na Zitto Kabwe kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa X.

Je, ni upi uhalisia wa chapisho hilo?

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia maneno muhimu (Key Word Search) ulibaini kuwa taarifa hiyo Si ya Kweli, haijachapishwa kwenye ukurasa rasmi wa 'X' wa Zitto Kabwe. Pia, imegundulika kuwa grafiki ya taarifa hiyo haijatolewa na Jambo TV, bali imetengenezwa na wapotoshaji.

Aidha grafiki hiyo imetengenezwa kwa muundo ambao hautumiwi na Jambo TV hasa inaporejea maudhui inayoyanukuu kutoka kwenye machapisho ya watu mbalimbali hasa mtandao wa 'X'

Unaweza Kuthibitisha Taarifa kwa kuangalia iwapo imechapishwa na chanzo rasmi chenye grafiki husika.​
Back
Top Bottom