Zitto Kabwe amefunguka mazito katika ukurasa wa twitter juu ya Shambulio la Mh.Tundu Lissu

Abdul Nondo

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
515
2,875
Leo siku ya tarehe 7/Sept. 2019 ,ndio tarehe na mwezi ambao Mh.Tundu Lisu alipigwa Risasi na watu wanaoitwa wasiojulikana,siku hii imemfanya Mh.Zitto Kabwe kutokujizuia na ameandika maneno mazito huko twitter.

Ameandika tweets 10 ambazo nimekuletea hapa chini.

1." *Leo imetimia miaka 2* tangu shambulizi lililokusudia kumwua Mbunge mwenzetu Tundu Lissu. Tunamshukuru sana Mungu kwa uwezo wake na maajabu yake ambayo yamemweka hai mwenzetu na sasa amepona na kuweza kushiriki nasi katika mapambano ya kuhami na kukomaza demokrasia yetu."

2." *Siku ya Tarehe 7/9/2017* ilianza kama siku nyengine tu kwa Wabunge na Watanzania. Rais @MagufuliJP alikuwa Ikulu akizungumzia sarakasi za makanikia, Tundu akiwa Bungeni akitimiza majukumu yake kwa kujadili Azimio la Malawi-Tanzania ( Mto Songwe). Ilipofika saa 7/8 mchana mzizimo"

3." *Mapito ambayo alipita ndugu Lissu* siku hiyo hakuna mtu anatamani kupita. Nchi nzima ilitaharuki. Macho na masikio yakawa General Hospital Dodoma na baadaye Nairobi kisha Leuven, Belgium. Mbunge kushambuliwa na risasi saa saba mchana akiingia nyumbani haijapata kutokea TANZANIA"

4." *Haijapata kutokea pia tukio kama hilo kutochunguzwa* na vyombo vya Dola vyenye mamlaka ya uchunguzi. Miaka 2 sio tu hajakamatwa hata panzi, bali pia Tundu Lissu alinyimwa matibabu, kazushiwa kila aina ya propaganda na sasa kavuliwa ubunge. Ukatili ambao haumithiliki"

5. *Kabla ya tarehe 7/9/2017 binafsi nilikuwa nabadili Siasa* kwa imani kuwa labda utawala mpya una nia ya dhati kwa nchi yetu. Baada ya tarehe 7/9/2017 na haswa baada ya kumwona Tundu hospitali, niliazimia ndani ya nafsi yangu kuwa huu ni utawala KATILI kuliko zote TANZANIA

6. *Wenzangu waliniuliza mbona umekuwa mkali sana post Sept 7, 2017?* Nikawaambia kuwa lengo la waliomshambulia Lissu ni kutunyamazisha. Tukinyamaza watakuwa wameshinda. Sasa sote twapaswa kuwa Tundu Lissu ili kutowapa ushindi watu katili na dhalimu. Mwenendo wa Siasa ulibadilika

7. *Nimemwona Tundu akiwa kwenye matibabu mara 5*. Mara 2 Nairobi na mara 3 Ubelgiji ikiwemo ya juzi ambayo niliweza kutembea naye mtaani. Mungu ni mkubwa sana. Lakini pia Mungu hufanya baadhi ya maajabu yake kwa sababu maalumu. Naamini alimponya Lissu ili kuiponya demokrasia yetu

8. *Kuna watu hupenda kurudisha nyakati na kuonyesha kuwa Mimi na Lissu tulikuwa maadui*. Hatukuwa maadui Lakini pia hatukuwa na mwono mmoja kisiasa. Sote tumegundua tofauti zetu hazikuwa na msingi wowote na waliotufitini kama Dkt. Slaa sasa ni mabalozi wa utawala Katili.

9. *Mimi na Lissu tumeamua kwa dhati kufanya kazi pamoja kwa kuweka maslahi ya nchi yetu mbele*. Wanaoturudisha nyuma wakidhani watazuia umoja huu wanajisumbua. Nchi yetu ni kubwa zaidi ya zilizokuwa tofauti zetu. Kuhami na kukomaza demokrasia yetu ni kazi ya utukufu na TUTAIFANYA.

10. *Tunamwomba Mungu aendelee kutuweka hai tutimize wajibu wa kizazi chetu* kwa kuongoza mabadiliko makubwa ya kisiasa yatakayowezesha wananchi kuwa na maisha mazuri ya raha na furaha. Nawataka wana demokrasia wengine wote tutazame mbele. Nkrumah alisema *FORWARD EVER, BACKWARD NEVER*

Maneno ya Kiongozi huyo wa Chama na Mbunge wa Kigoma Mjini ,Mh.Zitto Kabwe yanatia moyo na hari ya mapambano huko tuendako,maneno haya yanalengo kuleta pamoja vyama vyote pinzani kusahau tofauti za jana na leo.

Kudumisha umoja wa hali ya juu kwa ustawi wa demokrasia yetu na maslahi ya watu wetu,jamii yetu na taifa letu kwa ujumla.

Aliyewahi kuwa kiongozi mkubwa wa Chama pinzani huko New Zealand ,Dr.Don Brash aliwahi sema

"Opposition parties don’t have the same resources as the Government and the Executive, so we have to work twice as hard to get the same results" alimanisha vyama pinzani hawana rasilimali kama ambavyo serikali au chama kilicho madarakani wanayo mfano,fedha na mambo mengine hivyo kuna haja ya vyama pinzani kufanya kazi mara mbili au zaidi ili kuweza kukabiliana.

Umoja ,mshikamano,upendo na ushirikiano wa vyama pinzani bila chuki,tamaa na hisia dhidi ya mwingine ndio nguzo haswa wa vyama pinzani kukabiliana na CCM zaidi ya hapo.Hakuna chochote zaidi ya kujifurahisha.

Abdul Nondo.

abdulnondo10@gmail.com
 
Hakika ni siku wasiojulikana walinifanya nishindwe kula nyama nikaifanya siku ile kua yakuiazimisha Kama nifanyavyo ijumaa kuu siku zote Kama mkatholiki. Siku zote giza halijawahi kushinda nuru
 
Kwahiyo?
 
Laiti kama Mungu angeruhusu kuombea watu laana basi waliopanga, waliotekeleza na wale woote waliofurahi tundu lisu kupigwa risasi wooote nawaombea laana.

OVER
Mungu mponye mtu wako adui ameshindwa
 
Kupona kwa Lissu ilikuwa lazima maana ni yeye pekee alikuwa akiongea na kumpinga Jiwe hadharani, pamoja na kupelekwa mahakamani ila aliwashinds siku zote. Shetani alipotaka Lissu aondoke Mungu akasema hapana ngoja aishi ili wahusika wajue kuwa yupo Mungu
 
Nchi haijawahi kuwa na kiongozi katili kama huyu wa sasa. Anapenda sifa kiasi cha kutoa uhai wa binadamu wenzake, ameamrisha serikali nzima ifanye kazi ya kumsifu na kumtukuza kwa mapambio nk huku pesa ya kodi zetu akitumia kama zake binafsi. Kwetu tunaamini uwepo wa Mungu aliye hai, tuna hakika kuwa atapata malipo yake hapa hapa katika maisha haya
 
Uzuri wa twitter unaweza ukaandika watu wakadhani una hisia kali kumbe umejifunika shuka nyumbani.
 
Laiti kama Mungu angeruhusu kuombea watu laana basi waliopanga, waliotekeleza na wale woote waliofurahi tundu lisu kupigwa risasi wooote nawaombea laana.

OVER
Mbona Tayari Laana imeshawwandama?.
Huko ndani kwenye genge la wauwaji ,hali si shwari,
Watamalizana wenyewe kwa wenyewe hawa.wee tulia hadi 2020 uone move,
 
Back
Top Bottom