Zitto Kabwe akamatwa, afikishwa mahakamani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto Kabwe akamatwa, afikishwa mahakamani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Dingswayo, Dec 25, 2010.

 1. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #1
  Dec 25, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145


  Na Mwandishi wetu  25th December 2010
  [​IMG] Ni baada ya kuhutubia mkutano jimboni kwake
  [​IMG] Adaiwa kutorosha mtuhumiwa kituo cha polisi  [​IMG]
  Zitto Zuberi Kabwe
  Mbunge wa Kigoma Kaskazini kwa tiketi ya Chama cha Maendeleo (Chadema), Zitto Zuberi Kabwe, amekamatwa na askari wa Jeshi laPolisi kisha kupandishwa kizimbani na kusomewa shtaka la jinai.
  Zitto alikamatwa juzi jioni majira ya saa 12:00 akiwa njiani kurejea nyumbani kwake Mwandiga muda mfupi baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Kawawa katika Manispaa ya Kigoma/Ujiji.
  Baada ya kumkamata askari hao walimpeleka moja kwa mojaKituo Kikuu cha Polisi Mkoa wa Kigoma kwa mahojiano kisha kumwachia kwa kumpa masharti ya kuripoti jana asubuhi kituoni hapo.
  Zitto (34) ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, alitii amri hiyo na kukamatwa na askari baada ya kuwasili kisha kumfikisha Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mkoa wa Kigoma.
  Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Emmanuel Mlangu, ilidaiwa naMwendesha Mashitaka, Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Amoni Chale kuwa Oktoba 27, mwaka huu majira ya saa 5:00 asubuhi katika Kituo cha Polisi Mahembe, mshtakiwa huyo alitumia nguvu kumtoa mtuhumiwa huyo Peter Kibwega ambaye alikuwa chini ya ulinzi halali wa polisi na kumtorosha.
  Ilidaiwa kuwa mtuhumiwa huyo ambaye ni mwanachama wa Chadema alikamatwa na polisi kwa kutoa lugha ya matusi dhidi ya Alexander Bagambena na kumtishia kumuua Nicodemus Stephano na kufunguliwa kesi namba IR/130/20010 kabla ya kudaiwa kutoroshwa na mshtakiwa huyo.
  Mshtakiwa huyo alikana shtaka hilo na kuachiwa baada ya baba yake mzazi, Alhaji Menge Bakari kutimiza masharti ya kuwasilisha barua kutoka kwa afisa mtendaji wa kata kwa dhamana ya Sh. 1,000,000.
  Kesi hiyo iliahirishwa hadi Febuari 10, mwakani itakapoanza kusikilizwa baada ya upande wa mashtaka kudai upelelezi wake umekamilika.
  Baadhi ya wanachama wa Chadema walikusanyika katika mahakama hiyo wakiongozwa na Katibu wa chama hicho Mkoa wa Kigoma, Msafiri Wamarwa na kutawanyika baada ya Zito kuachiwa kwa dhamana.  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Dec 25, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,497
  Likes Received: 19,909
  Trophy Points: 280
  ulikuwa jela nini? hii stori ilikuwa hapa toka jana
   
 3. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #3
  Dec 29, 2010
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Ametoka usingizini
   
Loading...