Zitto Kabwe adanganya tena!

Salim Khatri

Member
Mar 6, 2015
69
21
Wanajamvi,

Huko nyuma nilipata kuandika makala "Uongo wa Taarifa ya Kamati ya PAC Kuhusu Sakata la Escrow" (unaweza kuisoma hapa Index of /escrow/viambatanisho) ambayo ilikuwa summary ya yale ambayo tuliyachambua kwenye Ukumbi wa Wanazuoni (http://www.yahoogroups.com/wanazuoni). Mh. Zitto Kabwe alikuwa mwanachama wa huo ukumbi na alikuwa anachangia kwenye hiyo majadala pale alipokuwa anaona convinience kwake na mara nyingi alikuwa "anauchuna" pale maswali magumu yalipokuwa yanaulizwa. Mara ya mwisho Mh. Zitto alinituhumu kuwa mimi natumiwa na Bwana James Rugemalira kama consultant wake katika kueneza UONGO dhidi yake. Nilim-challenge Zitto tufanye mdahalo wa wazi (open public debate) kati yangu mimi na yeye halafu tuwaache audience (wasikilizaji) waamue nani muongo na nani mkweli. Japo alikubali na kuthibitisha kuwa yuko tayari kwa mdahalo huo lakini mpaka leo "kaingia mitini" na hata Ukumbi wa Wanazuoni amejitoa.

Tarehe 22 Januari 2016, IPTL waliweka Press Release (PR) iliyoitwa "Conflict of Interest and Unconstitutionality of Intention to Reintroduce the Tegeta Escrow Account Issue in the Parliament" kwenye magazeti ya Daily News, Mwananchi na Mtanzania. PR hiyo unaweza kuisoma hapa Conflict of Interest and Unconstitutionality of Intention to Reintroduce the Tegeta Escrow Account Issue in the Parliament Pia unaweza kupakua nakala ya mashtaka na utetezi wa Mh. Zitto kwenye huo ukurasa.

Kati ya mambo kadhaa kwenye hiyo PR mojawapo ni kueleza umma kuwa Mh. Zitto Kabwe alikuwa na mgongano wa kimaslahi na suala la Tegeta Escrow Account kwani alikuwa ameshtakiwa mahakamani kwenye kesi ya madai namba 175 ya 2014 katika Mahakama Kuu ya Tanzania ambayo hakuitangaza (declare) muda wote wa sakata hili linaendelea bungeni mpaka yeye Zitto kuwasilisha Ripoti ya PAC mwezi Novemba 2014. Mh. Zitto na gazeti la Raia Mwema walishtakiwa kwenye kesi hiyo ya madai kutokana na makala yenye kichwa "Fedha za IPTL ni Mali ya Umma" ilyoandikwa kwenye gazeti hilo tarehe 13 Agosti 2014.

Katika harakati ya kujibu hizo tuhuma za kuwepo kwa mgongano wa maslahi (conflict of interest), Mh. Zitto kupitia kwa mwanasheria wake Emmanuel Lazarus Mvula wa kampuni ya Gabriel & Co Attorneys At Law wametoa Press Release ambayo imebandikwa kweye ukurasa wa Facebook wa Mh. Zitto hapa Zitto Kabwe - REF: CONFLICT OF INTEREST AND... | Facebook Katika paragraph ya pili ya hiyo Press Release, mwanasheria wa Zitto anadai:

"... Hon. Zitto Zuberi Kabwe at the time of presenting the report and during the entire parliamentary proceedings relating to the saga and in fact during the whole parliamentary session was not aware of the Civil Case No. 175 of 2014 pending in the High Court of Tanzania (District Registry) at Dar es Salaam. He became aware of the Civil Case nearly six (6) months later when he was served with the same on the 23rd April 2015. ( See the published copy of the Plaint). How on earth would Hon. Zitto be aware of the case on November 2014 while he was served in April 2015. We guess if he would have been aware of the same then he would make the best Astrologist than a great MP he is and probably IPTL/PAP his clients"​

Madai haya ya kuwa Mh. Zitto alikuwa hafahamu kuwepo kwa kesi hiyo isipokuwa mpaka mwezi April 2015 ni UONGO MKUBWA kabisa. Uwepo wa kesi hii iliripotiwa na takriban magazeti yote mwezi wa Septemba 2014. Baadhi ya magazeti yaliyoripoti hii kesi ni IPP Media (Home) na hata kwenye JamiiForums ilibandikwa na kujadiliwa (IPTL yamdai Zitto bilioni 500 mahakamani).

Cha ajabu yeye mwenyewe Zitto mnamo tarehe Septemba 10, 2014 ali-tweet kutoka kwenye Twitter Account yake kuhusiana na hiyo kesi na kudai:

"#IPTL wanatumia mahakama kuziba watu kusema? Wasubiri ripoti ya Ukaguzi Maalum kutoka kwa CAG. Wasubiri taarifa... Zitto Kabwe - Téléchargements mobiles | Facebook"
Source: Zitto Kabwe Ruyagwa on Twitter

Na siku hiyo hiyo kwenye ukurasa wake wa Facebook (Zitto Kabwe Ruyagwa on Twitter) ameweka picha ya gazeti la Mtanzania inayoripoti hiyo kesi "IPTL yamshtaki Zitto" na akaweka comment kama hiyo hapo juu ya kwenye Twitter.

Septemba 2014 unadai kuwa kesi uliyofunguliwa dhidi yako ni kitendo cha kukufunga mdomo halafu January 2016 unadai kuwa ulikuwa hujui (not aware) uwepo wa hiyo kesi ni UONGO mtupu.

Wanasema WAONGO wanatakiwa wawe na kumbukumbu nzuri lakini Mh. Zitto amedanganya mchana kweupe bila ya aibu kwenye hiyo Press Release yake bila ya kuwa na kumbukumbu ya yale aliyopata kuandika huko nyuma.
 
Nakubaliana na wewe kuwa Zito sometimes hupotosha sana,nakumbuka Escrow kabla Cag hajatoa ripoti publically alikuwa humu na kusisitiza kuwa "hakuna mjadala,CAG kasema wazi pesa ni za umma",nilivopata repoti wala haikuwa ivo,CAG mwenyewe hakuna certain kama Zito alivodanganya
 
Umeeleza kwa kina na kueleweka.
Wrote tunahasira na IPTL,lakini hiyo haiondoi maadili ya viongozi
Zitto hana credibility tena ya kuongea jambo na watu wakamtumaini
Alipiga figisufigisu kuhusu fedha za Uswis,alishupalia kutwa ushujaa wa sakata la Escrow scandal mbele ya Kafulila!
 
Mara tunaelezwa Zitto alikula fedha za Escrow na akaamua kupoozesha mjadala bungeni mara tunaelezwa Escrow wanamfungulia kesi Zitto mara tunaelezwa Zitto anatumiwa na Like Mkono na Mengi kwa kukosa mgao wa Escrow!!!
SIJUI LIPI NI LIPI?
 
Acha upotoshaji kumbuka hasard za CAF .tra na pccb
Nakubaliana na wewe kuwa Zito sometimes hupotosha sana,nakumbuka Escrow kabla Cag hajatoa ripoti publically alikuwa humu na kusisitiza nkuwa "hakuna mjadala,CAG kasema wazi pesa ni za umma",nilivopata repoti wala haikuwa ivo,CAG mwenyewe hakuna certain kama Zito alivodanganya
 
Mara tunaelezwa Zitto alikula fedha za Escrow na akaamua kupoozesha mjadala bungeni mara tunaelezwa Escrow wanamfungulia kesi Zitto mara tunaelezwa Zitto anatumiwa na Like Mkono na Mengi kwa kukosa mgao wa Escrow!!!
SIJUI LIPI NI LIPI?
Siasa zetu bila shombo haziendi
 
Wanajamvi,

Huko nyuma nilipata kuandika makala "Uongo wa Taarifa ya Kamati ya PAC Kuhusu Sakata la Escrow" (unaweza kuisoma hapa Index of /escrow/viambatanisho) ambayo ilikuwa summary ya yale ambayo tuliyachambua kwenye Ukumbi wa Wanazuoni (http://www.yahoogroups.com/wanazuoni). Mh. Zitto Kabwe alikuwa mwanachama wa huo ukumbi na alikuwa anachangia kwenye hiyo majadala pale alipokuwa anaona convinience kwake na mara nyingi alikuwa "anauchuna" pale maswali magumu yalipokuwa yanaulizwa. Mara ya mwisho Mh. Zitto alinituhumu kuwa mimi natumiwa na Bwana James Rugemalira kama consultant wake katika kueneza UONGO dhidi yake. Nilim-challenge Zitto tufanye mdahalo wa wazi (open public debate) kati yangu mimi na yeye halafu tuwaache audience (wasikilizaji) waamue nani muongo na nani mkweli. Japo alikubali na kuthibitisha kuwa yuko tayari kwa mdahalo huo lakini mpaka leo "kaingia mitini" na hata Ukumbi wa Wanazuoni amejitoa.

Tarehe 22 Januari 2016, IPTL waliweka Press Release (PR) iliyoitwa "Conflict of Interest and Unconstitutionality of Intention to Reintroduce the Tegeta Escrow Account Issue in the Parliament" kwenye magazeti ya Daily News, Mwananchi na Mtanzania. PR hiyo unaweza kuisoma hapa Conflict of Interest and Unconstitutionality of Intention to Reintroduce the Tegeta Escrow Account Issue in the Parliament Pia unaweza kupakua nakala ya mashtaka na utetezi wa Mh. Zitto kwenye huo ukurasa.

Kati ya mambo kadhaa kwenye hiyo PR mojawapo ni kueleza umma kuwa Mh. Zitto Kabwe alikuwa na mgongano wa kimaslahi na suala la Tegeta Escrow Account kwani alikuwa ameshtakiwa mahakamani kwenye kesi ya madai namba 175 ya 2014 katika Mahakama Kuu ya Tanzania ambayo hakuitangaza (declare) muda wote wa sakata hili linaendelea bungeni mpaka yeye Zitto kuwasilisha Ripoti ya PAC mwezi Novemba 2014. Mh. Zitto na gazeti la Raia Mwema walishtakiwa kwenye kesi hiyo ya madai kutokana na makala yenye kichwa "Fedha za IPTL ni Mali ya Umma" ilyoandikwa kwenye gazeti hilo tarehe 13 Agosti 2014.

Katika harakati ya kujibu hizo tuhuma za kuwepo kwa mgongano wa maslahi (conflict of interest), Mh. Zitto kupitia kwa mwanasheria wake Emmanuel Lazarus Mvula wa kampuni ya Gabriel & Co Attorneys At Law wametoa Press Release ambayo imebandikwa kweye ukurasa wa Facebook wa Mh. Zitto hapa Zitto Kabwe - REF: CONFLICT OF INTEREST AND... | Facebook Katika paragraph ya pili ya hiyo Press Release, mwanasheria wa Zitto anadai:

"... Hon. Zitto Zuberi Kabwe at the time of presenting the report and during the entire parliamentary proceedings relating to the saga and in fact during the whole parliamentary session was not aware of the Civil Case No. 175 of 2014 pending in the High Court of Tanzania (District Registry) at Dar es Salaam. He became aware of the Civil Case nearly six (6) months later when he was served with the same on the 23rd April 2015. ( See the published copy of the Plaint). How on earth would Hon. Zitto be aware of the case on November 2014 while he was served in April 2015. We guess if he would have been aware of the same then he would make the best Astrologist than a great MP he is and probably IPTL/PAP his clients"​

Madai haya ya kuwa Mh. Zitto alikuwa hafahamu kuwepo kwa kesi hiyo isipokuwa mpaka mwezi April 2015 ni UONGO MKUBWA kabisa. Uwepo wa kesi hii iliripotiwa na takriban magazeti yote mwezi wa Septemba 2014. Baadhi ya magazeti yaliyoripoti hii kesi ni IPP Media (Home) na hata kwenye JamiiForums ilibandikwa na kujadiliwa (IPTL yamdai Zitto bilioni 500 mahakamani).

Cha ajabu yeye mwenyewe Zitto mnamo tarehe Septemba 10, 2014 ali-tweet kutoka kwenye Twitter Account yake kuhusiana na hiyo kesi na kudai:

"#IPTL wanatumia mahakama kuziba watu kusema? Wasubiri ripoti ya Ukaguzi Maalum kutoka kwa CAG. Wasubiri taarifa... Zitto Kabwe - Téléchargements mobiles | Facebook"
Source: Zitto Kabwe Ruyagwa on Twitter

Na siku hiyo hiyo kwenye ukurasa wake wa Facebook (Zitto Kabwe Ruyagwa on Twitter) ameweka picha ya gazeti la Mtanzania inayoripoti hiyo kesi "IPTL yamshtaki Zitto" na akaweka comment kama hiyo hapo juu ya kwenye Twitter.

Septemba 2014 unadai kuwa kesi uliyofunguliwa dhidi yako ni kitendo cha kukufunga mdomo halafu January 2016 unadai kuwa ulikuwa hujui (not aware) uwepo wa hiyo kesi ni UONGO mtupu.

Wanasema WAONGO wanatakiwa wawe na kumbukumbu nzuri lakini Mh. Zitto amedanganya mchana kweupe bila ya aibu kwenye hiyo Press Release yake bila ya kuwa na kumbukumbu ya yale aliyopata kuandika huko nyuma.

Vidokezi:- Kesi ya kumshtaki zito ilifunguliwa lini na IPTL,haijatajwa,manake umetaja namba ya kesi 175 ya mwaka 2014.
Makala iliandikwa Raia mwema Agosti 13 2014
Zitto aliwasilisha ripoti ya PAC Mwezi novemba 2014
Septemba 14 zitto anadai kesi iliyofunguliwa dhidi yake ni ya kumfunga mdomo.

Juzi tu hawa jamaa wametoa press release ,na wewe unatoa (press release ) kijanja humu JF .Boss unatumika Period! Hata ukisoma press release yao ni kama wanataka hisani kwa wananchi.Bunge ni muhimili unaosimamia na kuishauri serikali kulingana na katiba wataishauri vipi bila kuipitia escrow ,wewe ni jipu.
 
Mara tunaelezwa Zitto alikula fedha za Escrow na akaamua kupoozesha mjadala bungeni mara tunaelezwa Escrow wanamfungulia kesi Zitto mara tunaelezwa Zitto anatumiwa na Like Mkono na Mengi kwa kukosa mgao wa Escrow!!!
SIJUI LIPI NI LIPI?
Zitto sio mtu wa kuaminika sio kwa sababu ni mwana siasa (wanasema usimuamini mwanasiasa) ila kwa sababu haeleweki anachosimamia katika maslahi ya nchi hii,kumbuka hoja ya Buzwagi iliyopelekea kuundwa ile tume ya mambo ya madini ambapo alikua mjumbe alitoka na tuhuma lukuki Za kujinufaisha, ishu ya Escrow anatuhumiwa kunufaika binafsi.
 
Tutajie Mwanasiasa gani wa kumuamini hapa Bongo nihamishie Imani yangu kwake?
 
Umeeleza kwa kina na kueleweka.
Wrote tunahasira na IPTL,lakini hiyo haiondoi maadili ya viongozi
Zitto hana credibility tena ya kuongea jambo na watu wakamtumaini
Alipiga figisufigisu kuhusu fedha za Uswis,alishupalia kutwa ushujaa wa sakata la Escrow scandal mbele ya Kafulila!
ila wa kuaminiwa ni viongozi wa ukawa waloimba kutwa nzima lowasa fisadi kilichotokea wakatwambia wamebadilishia gia angani
 
INTEGRITY IS THE NUMBER ONE QUALITY OF A TRUE POLITICAL LEADER.

NI DHAMBI YA KIHISTORIA KUTAKA KUTUAMINISHA KUWE WEWE NI MKWELI HUKU MOYONI MWAKO UNAJUA UNATUDANGANYA.

WANASIASA WANAPASWA KUJITATHMINI. DUNIA YA SASA SIO YA SIASA ZA KIUJANJAUJANJA
 
Wanajamvi,

Na siku hiyo hiyo kwenye ukurasa wake wa Facebook (Zitto Kabwe Ruyagwa on Twitter) ameweka picha ya gazeti la Mtanzania inayoripoti hiyo kesi "IPTL yamshtaki Zitto" na akaweka comment kama hiyo hapo juu ya kwenye Twitter

Ikiwa barua ya mahakama ilimfikia katika tarehe ambayo wakili wake ameandika na kumbukumbu za rejista ya kupokelea barua zinaonesha zito amesaini tarehe hiyo, na ikiwa magazeti hayo hayakuwa tangazo rasmi la mahakama (kwa kuwa mdaiwa hapatikani katika anwani yake), kisheria Zitto alikuwa hana taarifa za uwepo wa kesi dhidi yake hata kama mazeti ya nchi nzima na nchi jirani yaliandika.

Ni vema uchambuzi ukawa wa kimantiki zaidi kuliko kutaka kuonesha kuwa ulikwa sahihi kuchukua upande wa IPTL.
 
Back
Top Bottom