Uchaguzi 2020 Zitto: Ilani ya ACT Wazalendo na utekelezaji wake

Zitto

Former MP Kigoma Urban
Mar 2, 2007
1,562
10,880
Ahadi za ACT Wazalendo Jamhuri ya Muungano ZITATEKELEZWAJE?

1. Elimu ya Juu: Kufuta mikopo yote ya miaka ya nyuma iliyotolewa kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu na kuanza kutekeleza Mfumo mpya wa kugharamia Elimu ya Juu. Serikali italipia Ada ya Masomo (Tuition Fee), Fedha za Vitabu (Stationeries), na gharama za Mafunzo kwa Vitendo (Field Studies/Internship) kwa kila mwanafunzi anayedahiliwa kwenye Chuo Kikuu. Wanafunzi watachukua mikopo, Kwa wanaotaka, Kwa ajili ya gharama za maisha tu ( Meals and Accommodation ). Mfumo mpya utaanza Mwaka wa Masomo 2021/2022.

FEDHA ZA KUTEKELEZA ZITATOKA WAPI?

- Gharama za Elimu Ufundi na Elimu ya Juu zitatokana na Mapato ya Tozo ya kuongeza ujuzi ( Skills Development Levy - SDL ). Tozo hii itatozwa kutoka Waajiri wa sekta binafsi na sekta ya Umma Kwa kiwango cha 2% ya gharama za mishahara. Sasa hivi tozo hii inatozwa kwa sekta binafsi peke yake Kwa kiwango cha 4% ya gharama zote kwa Wafanyakazi walioajiriwa na kampuni husika ( SDL is charged based on the gross pay of all payments made by the employer to the employees employed by such employer ). Baada ya marekebisho ya kupanua wigo wa walipaji, Serikali itakuwa na uwezo wa kukusanya shilingi Bilioni 470 kila Mwaka. Mapato haya yataongezeka kulingana na kuongezeka kwa shughuli za Uchumi Nchi na Ajira nyingi zaidi kutengenezwa.

2. Bima ya Afya kwa Wote: Kuboresha mfuko wa Bima ya Afya kwa kuunganisha na mifumo ya Hifadhi ya Jamii, ili kila Mtanzania anapochangia hifadhi ya jamii awe anapata huduma ya Afya moja kwa moja. Kwa mfumo huu, mfuko wa Bima ya Afya utaweza pia kupata fedha kwa wakati na kulipa watoa huduma kwa wakati. Bima ya Afya ni haki ya kila Mtanzania. Itaisimamia kikamilifu haki ya kila Mtanzania kuwa na Bima ya Afya yenye kumpa kinga ya matibabu bila kujali hali yake ya kiafya (wakati wa kujiunga na bima).

FEDHA ZA KUTEKELEZA ZITATOKA WAPI?

- Kupitia vyama vya Ushirika na vikundi vya uzalishaji vya Wananchi haswa Wakulima, Wafugaji na Wavuvi Serikali itaanzisha Mfumo wa kuchangia wananchi wanaochangia Skimu ya Hifadhi ya Jamii. Serikali itatenga Fedha kutoka kwenye Bajeti kila Mwaka kuchangia michango ya Wananchi kwenye Hifadhi ya Jamii ( matching scheme). Kwa mfano katika mchango wa Shs 30,000 kwa Mwezi, Serikali itamchangia Mwananchi Shs 10,000. Kwa njia hii kila Mtanzania atakuwa na Bima ya Afya Kama Fao katika Skimu ya Hifadhi ya Jamii. Skimu hii itawezesha Taifa kuwa na Akiba kubwa kwa uwiano wa Pato la Taifa (savings - GDP ratio) na hivyo kuwezesha uwekezaji mkubwa na wa muda mrefu kufanyika. Kwa Makadirio ya Watu Milioni 6 watakaojiunga na Skimu ya Hifadhi ya Jamii, Mfuko utakuwa makusanyo ya Shilingi Trilioni 2.2 kwa Mwaka, katika hizo Shilingi Bilioni 648 zitachangiwa na Serikali kutoka kwenye Bajeti.

3. Maji safi na salama kwa kila Mtanzania: Kuwekeza kiasi cha shilingi Trilioni 10 ndani ya miaka mitano, wastani wa Shilingi Trilioni 2 kwa kila mwaka, kwenye kumaliza kabisa tatizo la maji safi na salama kwa Wananchi. Hii ni pamoja na kujenga na kupanua miundombinu ya maji safi na maji taka.

FEDHA ZA KUTEKELEZA ZITATOKA WAPI?

- Gharama za Ujenzi wa Miradi ya Maji zitagharamiwa na Tozo Maalumu ya Matumizi ya Mafuta ya Petroli. Serikali itachukua Mkopo nafuu wa Muda mrefu wa Shilingi Trilioni 10 kutoka Benki za Maendeleo ili kutekeleza mradi kwa mara moja na Mapato ya ‘fuel levy’ yatahudumia mkopo huo mpaka utakapomalizika kulipwa. Tozo ya shilingi 200 kwa kila lita ya Mafuta itazalisha Jumla ya shilingi Bilioni 700 kila Mwaka zinazoweza kutumika kulipa mkopo wa muda mrefu wa miaka 15.

4. Barabara ya Korosho: Kuwezesha Ujenzi wa barabara ya korosho (cashew ring road) – Nangurukuru – Liwale – Nachingwea – Masasi – Newala – Tandahimba – Mtwara – Lindi - Nangurukuru kutoka mapato ya ushuru wa korosho kwa kutumia mfumo wa “development finance” ili kufungua wilaya zinazolima korosho. Vile vile kufungua Wilaya ya Liwale kwa kufungua barabara za Songea-Liwale na Liwale-Morogoro

FEDHA ZA KUTEKELEZA ZITATOKA WAPI?

- Gharama za Ujenzi wa Barabara ya Korosho (Cashew Ring Road) zitalipiwa na 50% ya Mapato ya Ushuru wa Korosho (exports levy) ambapo Serikali itachukua mkopo nafuu wa muda wa kati ili kupata fedha za ujenzi wa barabara hiyo mara moja na mapato ya exports levy yatahudumia mkopo huo mpaka utakapomalizika kulipwa. Ushuru wa Korosho unakadiriwa kuingiza mapato ya zaidi ya shilingi Bilioni 245 kila Mwaka ambazo nusu yake inaweza kulipa mkopo wa barabara hiyo na barabara za Songea-Liwale na Liwale-Morogoro kwa muda wa miaka 10.

5. Kilimo cha kimapinduzi: Kusimamia Ujenzi wa mabwawa makubwa 5 ya kuzuia mafuriko na kujenga skimu kubwa za umwagiliaji zenye jumla ya hekta 1,000,000 zitakazowezesha Kilimo cha kimapinduzi, mamilioni ya ajira, uzalishaji wa mazao ya mafuta ya kula, sukari na chakula hivyo kuokoa fedha za kigeni zinazotumika kuagiza sukari na mafuta ya kula kutoka nje, na kuongeza Mapato ya Fedha za Kigeni.

FEDHA ZA KUTEKELEZA ZITATOKA WAPI?

- Gharama za Miradi mikubwa ya Umwagiliaji zitalipiwa kutoka uwekezaji wa skimu ya Hifadhi ya Jamii kwa Wakulima kama uwekezaji wa Skimu wa muda mrefu. Jumla ya Shilingi Trilioni 2.5 zitawekezwa kwenye miradi hii ya uwekezaji kutoka Skimu ya Hifadhi ya Jamii kama Uwekezaji wa kuongeza shughuli za uchumi Kwa kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo na Viwanda vya kuongeza mazao ya Kilimo.

Kitengo cha Kampeni ACT Wazalendo
Agosti 7, 2020
 
Safi sana hii imekaa vizuri. hizi ndo issues tunazotaka kuzisikia kwa sasa!

Lakini pamoja na hayo vipi kuhusu

1. Maslahi ya watumishi wa Umma?
2. Katiba mpya?
3. Wafanyabiashara ndogondogo?
4. Mna mpango gani wa kukuza ajira nyingine ukiacha Kupitia Kilimo?
5. Plan yenu ya kuinua wanawake ikoje?
6. Plan yenu ya kupambana na Ufisadi ikoje?
7.Kuhusu gesi mna mkakati gani
8. Vipi kuhusu kupunguza tatizo la kudumaa watoto wachanga kwa kukosa Lishe bora?
9. Vipi kuhusu Viwanda mna plan gani?
 
Hongera kiongozi
Umeandika kila kitu na suluhisho lake

Hapo kwenye mikopo ya wanafunzi mtachukua credit sana ,Waambieni wazazi akina Baba na akina Mama jinsi wanavyoteseka na gharama za mikopo kwa watoto wao

Waambieni mtafuta asilimia ile 15 aliyoileta Bwana mkubwa kwa vijana wao ,Hivyo vijana watakuwa na pesa ya kuwasaidia wazazi

Hili hata sisi watetea chama humu tutakuunga mkono

Wanafunzi ambao wanaanza maisha unachaji asilimia 15 haikubaliki

Kwa hili mwambie hata Tundu lisu tutamuunga mkono
 
Ilani ni kitabu kizima...kama mnayo (na hamsubiri ku-plagiarise ya CCM) pakia 'upload' watanzania waione
 
Na uccm wangu Mkuu kwenye hoja ya mkopo naunga mkono unaweza fanya nisimchague mgombea wangu ujue
Lkn hebu angalia maslahi Ya watumishi ya
 
ZZK heshima kwako..

Leo Mh Membe amechukua form kugombea urais kama mgombea kutoka ACT.
Bila shala kesho pia TL atachukua form kugombea urais kwa tiketi ya CDM.
Kifupi upinzani kupitia vyama viwili vyenye nguvu na wafuasi mnasimamisha wagombea wawili kwa nafasi moja kwa maana you compete each other hamuoni hapa mnagawa kura za upinzania na kumpa urahisi mgombea wa CCM?..

Hamuoni hali hii ya nyie wenyewe kuwa washindani na pia kushindana na JPM mwenye kura zisizogawika nyingi mnakatisha tamaa wapenda mabadiriko na kuona haina maana tena kuendelea kussuport upinzani wenye kuangalia maslahi binafsi?

Kama upinzani mmeshindwa kukaa chini na kukibaliana hamuoni hali hii inatia shaka kwenye mustakabali mzima wa kuwapa nchi kama si watu mnaoweza kujadili, kukubaliana na kuamua?.

Nini Lengo la ACT kuilekea uchaguzi mkuu?

Je ACT mmemfanyia Mh Membe vetting ya kutosha na kujiridhisha anafaa kugombea uraisi??.
 
Tunataka ilani kama hizo, zinazogusa maslahi ya watu. Miundombinu ni muhimu baada ya maisha ya watu kwanza.

Ilani ya CCM tunaisubiri kwa hamu
 
Mpango wa Bima ya Afya kwa wote tayari uko jikoni mwaka wa pili sasa, na naimani Magu na Jenista Mhagama wameshaisema hadharani mara kadhaa. Utapitishwa na bunge lijalo.
 
Hongereni ACT wazalendo lakini hiki mlichoandika kina mapungufu makubwa mno Mfano hakijaeleza ilani iliyopita utekelezaji wake ulikuwaje kwenye Maeneo ambayo ACT wazalendo inaongoza mfano halmashauri ya Ujiji .Mlitakiwa muanze na taarifa ya utekelezaji wa ilani iliyopita kwenye Maeneo yenu Huwezi rusha future Bila past report

CCM huwa tunaanza na kuelezea ilani iliyopita tuliahidi Nini na tumetekeleza Nini ndipo tunaleta ilani mpya

Ila Hongereni mumejitahidi walau kuweka matumaini hewa
 
ZZK heshima kwako..

Leo Mh Membe amechukua form kugombea urais kama mgombea kutoka ACT.
Bila shala kesho pia TL atachukua form kugombea urais kwa tiketi ya CDM.
Kifupi upinzani kupitia vyama viwili vyenye nguvu na wafuasi mnasimamisha wagombea wawili kwa nafasi moja kwa maana you compete each other hamuoni hapa mnagawa kura za upinzania na kumpa urahisi mgombea wa CCM?..

Hamuoni hali hii ya nyie wenyewe kuwa washindani na pia kushindana na JPM mwenye kura zisizogawika nyingi mnakatisha tamaa wapenda mabadiriko na kuona haina maana tena kuendelea kussuport upinzani wenye kuangalia maslahi binafsi?

Kama upinzani mmeshindwa kukaa chini na kukibaliana hamuoni hali hii inatia shaka kwenye mustakabali mzima wa kuwapa nchi kama si watu mnaoweza kujadili, kukubaliana na kuamua?.

Nini Lengo la ACT kuilekea uchaguzi mkuu?

Je ACT mmemfanyia Mh Membe vetting ya kutosha na kujiridhisha anafaa kugombea uraisi??.
Wanaweza kwenda kimkakati kama Malawi. Endapo CDM na ACT pamoja watapata walau asilimia 50 ya kura, na CCM pungufu ya 50 (45% -49%). Uchaguzi utarudiwa ili mshindi apate 50% plus, hapo wapinzani waungane na kusimamisha mgombea mmoja

ACT wakipata kura nyingi za Urais za Znz, Kanda ya Kusini na Pwani na CHADEMA kanda ya kaskazini na Miji Mikubwa. Wapinzani washindane kimkakati kupata kura nyingi maeneo wenye ushawishi.
 
ZZK heshima kwako..

Leo Mh Membe amechukua form kugombea urais kama mgombea kutoka ACT.
Bila shala kesho pia TL atachukua form kugombea urais kwa tiketi ya CDM.
Kifupi upinzani kupitia vyama viwili vyenye nguvu na wafuasi mnasimamisha wagombea wawili kwa nafasi moja kwa maana you compete each other hamuoni hapa mnagawa kura za upinzania na kumpa urahisi mgombea wa CCM?..

Hamuoni hali hii ya nyie wenyewe kuwa washindani na pia kushindana na JPM mwenye kura zisizogawika nyingi mnakatisha tamaa wapenda mabadiriko na kuona haina maana tena kuendelea kussuport upinzani wenye kuangalia maslahi binafsi?

Kama upinzani mmeshindwa kukaa chini na kukibaliana hamuoni hali hii inatia shaka kwenye mustakabali mzima wa kuwapa nchi kama si watu mnaoweza kujadili, kukubaliana na kuamua?.

Nini Lengo la ACT kuilekea uchaguzi mkuu?

Je ACT mmemfanyia Mh Membe vetting ya kutosha na kujiridhisha anafaa kugombea uraisi??.
Katika hili wamezengua sana hawa jamaa. Wote ACT na CHADEMA.

Kiufupi ni wamefanya tathmini na nahisi wamejiridhisha kwamba hawawezi kumuondoa Mheshimiwa rais Magufuli madarakani, hivyo wanachokifanya ni kujaribu tu kuwa chama kuku cha upinzani. Yaani CDM na ACT wote wanagombania nafasi ya pili.

Kadi yangu ya CCM sijailipia mwaka wa kumi sasa ila kwa upumbavu huu naenda kuilipia soon.

Wangari Maathai
 
Hongereni ACT wazalendo lakini hiki mlichoandika kina mapungufu makubwa mno Mfano hakijaeleza ilani iliyopita utekelezaji wake ulikuwaje kwenye Maeneo ambayo ACT wazalendo inaongoza mfano halmashauri ya Ujiji .Mlitakiwa muanze na taarifa ya utekelezaji wa ilani iliyopita kwenye Maeneo yenu Huwezi rusha future Bila past report

CCM huwa tunaanza na kuelezea ilani iliyopita tuliahidi Nini na tumetekeleza Nini ndipo tunaleta ilani mpya

Ila Hongereni mumejitahidi walau kuweka matumaini hewa
Una hoja ila utekelezaji kwa kodi zipi mkuu?

Maamuzi mengi makubwa ya kisera/sheria yanafanywa na serikali iliyo madarakani. Madiwani na Halmashauri zinaishia kutunga sheria ndogo zisizo na mashiko.

Tungekuwa na mfumo wa majimbo labda
 
Back
Top Bottom