Return Of Undertaker
JF-Expert Member
- Jun 12, 2012
- 4,572
- 26,885
Jana nilikuwa nazungumza na baadhi ya Wafanyabiashara wa Kigoma kuhusu hali za biashara zao. Msafirishaji mmoja ( transporter ) kaniambia siku hizi hawezi kufikisha abiria 20 katika basi la abiria 55 kutoka Kigoma kwenda Dar. Hii ni Kwa sababu wananchi hawana fedha na hivyo hawasafiri.
Nimeambiwa kuwa huko Kasulu mawakala wa pembejeo za ruzuku wanaoidai Serikali wameanza kupata misukosuko ikiwemo nyumba zao kupigwa mnada na mabenki. Kasulu peke yake nyumba 5 zimeshapigwa mnada mpaka sasa.
Serikali itazame masuala haya maana yanarudisha watu kwenye umasikini. Kuna haja ya Wabunge kuisimamia Serikali Kwa umadhubuti kwenye suala zima la Uchumi. Kitaani hali ni mbaya Sana