Zitto azidi kuwaumiza wabunge wa CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto azidi kuwaumiza wabunge wa CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Jun 13, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 13, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,600
  Trophy Points: 280
  Exuper Kachenje, Dodoma

  KAULI ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe kuwa uanzishwaji wa Chuo Kikuu cha Dodoma haumo katika Ilani ya CCM na kuwa chama hicho kimeshindwa kufikia hata nusu ya utekelezaji ahadi za Ilani yake, imeendelea kuwaumiza vichwa wabunge wa CCM na kuwalazimisha kujibu wakitetea chama chao.

  Hali hiyo ilijitokeza juzi jioni na jana wakati wabunge hao wakichangia hotuba ya bajeti ya serikali kwa mwaka 2010/2011 bungeni mjini Dodoma.


  Juzi asubuhi Zitto alisema; "CCM imeshindwa kutekeleza hata nusu ya ahadi zake katika miaka mitano iliyopita, ujenzi wa Chuo Kikuu Dodoma nashangaa CCM wanajisifu, lakini hilo halipo katika ahadi za ilani yake. Kama yupo mbunge wa CCM anayeweza, asimame aje aonyeshe ni wapi Ilani ya CCM ilipotoa ahadi itajenga Udom, hakuna, hakuna, ‘nachallenge' kama yupo anayeweza kuonysha aje. Ujenzi wa Udom ni wazo na ahadi ya Chadema ya mwaka 1992".


  Maneno hayo makali yalimwinua mbunge wa Ukerewe Getrude Mongella katika kiti akidai Mwongozo wa Spika.


  "Hivi ni utaratibu mzuri kuwaambia Watanzania kupitia bunge kwamba CCM ilidanganya," alihoji Mongella baada ya kumyamazisha Zitto kwa kuomba mwongozo wa Spika.


  Hoja hiyo ya Mongella ambaye ni mbunge wa Ukerewe mkoani Mwanza (CCM), iliungwa mkono na Naibu Spika Anne Makinda, aliyeongoza kikao hicho jana asubuhi.


  "Upo sahihi mheshimiwa Mongella, lakini lazima tukubali kuwa katika wakati huu, ndio wakati hayo yatatokea tu", alisema Makinda.


  Lakini wabunge wote wa CCM waliopata nafasi ya kuchangia bajeti hiyo jioni ya juzi na jana waligusia suala la ujenzi wa Chuo Kikuu hicho wakisema ni kazi ya Rais Jakaya Kikwete akitekeleza ilani ya CCM.


  Mbunge wa Ilala Mussa Azzan Zungu alisema ujenzi wa Chuo Kikuu Dodoma ni utekelezaji wa Ilani ya CCM na kazi nzuri ya Rais Kikwete.


  "Ujenzi wa Chuo Kikuu Dodoma ni matunda ya Ilani ya CCM na kazi nzuri ya Rais Jakaya Kikwete"alisema.


  Kuhusu bajeti ya mwaka 2010/2011 Zungu alisema bajeti hiyo itapunguza idadi ya wapinzani bungeni na kwamba wanaosema bajeti itainyonga CCM walie tu. Bajeti hii itapunguza idadi ya wapinzani bungeni.


  Joseph Mungai ambaye ni Mbunge wa Mufindi mkoani Iringa alisema, hatua ya Zitto kueleza ujenzi wa chuo hicho ni sera ya Chadema ni sawa na kufafanua msahafu usio wake.


  "Jana (juzi) nilisikia mbunge mwenzangu Zitto Kabwe akisema ujenzi wa Chuo Kikuu Dodoma ni sera ya Chadema, hapo naona amejiingiza katika kutafsiri msahafu usio wake, ujenzi huo ni matunda ya Ilani nzuri ya CCM, katika ilani huwezi kufafanua kila ‘detail' lakini ilani imeweka wazi mkakati wa kuboresha na kuinua elimu nchini," alisema Mungai.


  Wengine waliochangia hotuba hiyo ya bajeti na kuponda kauli ya Zitto wakikitetea CCM ni pamoja na Kidawa Hamid Saleh(CCM), Dunstun Mkapa, Juma Ngasongwa na Balozi Idd Mshangama.


  Zitto azidi kuwaumiza wabunge wa CCM
   
 2. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #2
  Jun 13, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  huyu jamaa...ataaa, kwangu kaluzi credibility...
   
 3. M

  Marigwe JF-Expert Member

  #3
  Jun 13, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 226
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Hiyo kauli ya Zitto bungeni ya kitoto mno. Anataka kusema kuwa Ilani ya Uchaguzi ya CCM has nothing on elimu.

  Hebu aache siasa za kijinga namna hiyo. Hicho chuo kilipigiwa debe na CHADEMA? Tangu kimeanza hajawa
  hi kusema maneno hayo. Shame on you Honorable. What cheap politics. AAGH
   
 4. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #4
  Jun 13, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Tusimwonee Zitto yeye kauliza swali simple sana aonyeshwe kwenye ilani ya CCM kama iliahidi kujenga Chuo cha Dodoma, hata wewe kama unayo tusaidie, vinginevyo tujue serikali inafanya vitu bila mpangilio inakurupuka.
   
 5. m

  muheza2007 JF-Expert Member

  #5
  Jun 13, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 232
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 60
  Kwahiyo serikali inatakiwa itekeleze yale tu ambayo yameandikwa kwenye ilani yake? Ujenzi wa chuo kikuu cha DODOMA ni mafanikio ya serikali ya JK. Mbona wanalaumiwa kwa kushindwa kuwashughulikia mafisadi, kwani waliandika kwenye ilani kwamba watafunga mafisadi wote?

  Ilani ni dira tu juu ya vipaumbele vya chama kama kikichaguliwa kuingia ndani. Details zake za utekelezaji zinaonyeshwa kwenye budget wakati serikali inapoanza kutekeleza.

  Zitto alichambua vizuri sana hiyo budget na hakukuwa na sababu ya kuongezea hilo la UDOM kutokuwa kwenye ilani maani ni wazi limo kwenye ilani chini ya kuendeleza elimu nchini.
   
Loading...