DCONSCIOUS
JF-Expert Member
- Oct 4, 2010
- 1,269
- 473
Acha tabia ya kuongeza na kupunguza maneno. Zitto hakusema anataka kupambana na DR SLAA. Wewe ni mtu mzima na unategemewa tayari kuwa na uwezo wa kujicontrol, hivi vimaneno vya uzushi uzushi vinawashushia sana watu heshima ndugu yangu, Kwani unapungukiwa nini ukiandika ukweli? utaugua? utakosa pesa? vipi bwana.
Zitto alisema kama chama KITAMTEUA.
Au nyie wengine hampati usingizi mpaka nafsi zenu ziburudike kwa kusema uongo.
Kati kampeni za udiwani kata ya kiwira Zitto zuberi kabwe alisikika mara nyingi akimsifia sana slaa kwanza alisema DR Slaa ndie mtu aliye mfundisha kazi za bunge na kumpa uzoefu pamoja na mbinu. Pia alisema bila umakini wa Slaa leo watanzania wasingejua kama kuna ufisadi BOT pia alisema chadema ni makini kwani kina viongozi makini kama Mboye.
Nikajiuliza hivi ni kweli Zitto alitangaza nia ya kupambana na Slaa kuwania Urais kwenye kura za maoni?
Mkuu ulimuondoa moyoni kwa kuwa hakumsifia Dr. Slaa au kwa kuwa alitangaza kuutaka Urais kama chama kitampitisha? Vipi amekana kwamba hautaki Urais?.
Mwana mpotevu kwa hakika akirudi kwa babae na kuungama kosa lake hupokewa, huvikwa joho na kuchinjiwa mwana mbuzi mnono. Ni kweli Zitto ni kajana mzuri sana na mahiri na jambo moja tu linaloweza kumfikisha katika kilele cha mafanikio yake katika siasa ni kukaa chini ya watangulizi wake wa kisiasa, kuheshimu taratibu na kushaurika. Mh Zitto ni miungoni mwa wanasiasa niliowatarajia kufanikisha lengo la kuikomboa Tanzania. Japo alinikwaza kwa haraka yake, kwa yeye kuiona hiyo mistake natangaza kumsamehe kabisa na ninamrudisha katika sehemu yake stahiki ndani ya moyo wangu. Big up Zitto, una nafasi muhimu sana katika siasa ya nchi yetu, usikubali kuyumbishwa/kujiyumbisha kwa vyovyote vile.
.
Atapotea na kurudi na kuchinjiwa kondoo mara ngapi? Hao kondoo zizini atakaokuwa akichinjiwa mwana mpotevu mara kwa mara si wataisha sasa?.
Mwana mpotevu kwa hakika akirudi kwa babae na kuungama kosa lake hupokewa, huvikwa joho na kuchinjiwa mwana mbuzi mnono...
Enyi MAFISADI wote pamoja na chama CCM eleweni hili vema na kwa uwazi wake wote, ukweli wote ni kwamba;
... WaTanzania sote TUMESHAAMUA kwamba mambo yote ya ukombozi wa MTANZANIA kuondokana na MAFISADI ni kwa CHADEMA.
Je ni nani tena wa kutuzuia?????????????
... after a witness of a nationwide fury over Zitto's most tragic stategic blunder in announcing his distasteful bid for presidency at a time of a crucial party business on the grounds of Mwanza and Arumeru Mashariki, the inexperienced CHADEMA political lieutenant reads before our eyes to be attempting a technical tactical political retreat with his mentors in mind.
CHADEMA, if you please you can very well choose to forgive BUT never to FORGET or get humbled at a mere retreat NOT accompanied by an unquestionable flow of actions and commitment to our fold. And that's it as you stay with eyes wide cast in the horizons ayonder.
Kwani Slaa ameteuliwa lini tena kugombea Urais 2015?Nikajiuliza hivi ni kweli Zitto alitangaza nia ya kupambana na Slaa kuwania Urais kwenye kura za maoni?
Mboye ni nani?