Zitto atua Dodoma kuinadi ACT

ACT ndio chama bora cha upinzani kuwahi kutokea Tanzania
 
ACT inapendwa na watanzania wote,bila kujali dini wala kabila
 

Hiyo misingi imetoka wapi? wote hao hamna kitu. Fanya kazi, mkumbo tu mnafuata. Eti ACT, mtawadanganya sana waTZ. Kipi kipya ambacho viongozi wako hawajawahi kuongea kabla ya kutimkia huko? Wenye elimu ndogo mtawapata
 

DODOMA hatumtaki aende tu kuangalia gorofa zake alokuwa anazijenga pale Dodoma.
 
Anaenda Dodoma kuzungumzia nini ambacho hajawahi kuongea maana kwasasa anaongea porojo na kujisifia.ila mi nitakuja kukusanifu ili niongeze wingi wa watu .
 
Watanzania wanataka kusikia habari ya Katiba mpya kama inafaa ama haifai, Tume huru ya uchaguzi, Uandikishwaji wa daftari la kudumu la wapiga kura na Uchaguzi mkuu mwezi October - sasa mtu mwingine eti anatanganza chama chake kipya!!
Mkuu Chadema wapo Mtwara wanafanya mikutano yao wao sawa ATC wakifanya mikutano yao kwako tatizo vumulia dawa ikuingie.
 

Mvikeni kama ninyi msituhusishe sisi wagogo wote sisi tunajitambua hatuna mpango wowote na huyo ZZK na msimdanganye eti viti 30 yaani hadi nimecheka kwa Dodoma ninayoifahamu.
 
Kwa Dodoma hawezi kutudanganya lolote aende zake Kigoma huko.dodoma hatutaki watu wanaoeneza udini na wanajisifia maisha yao.sisi na CCM au wengine UKAWA basi.

acha kueneza chuki za udini mkuu.... hatujawasikia ACT Wazalendo jukwaani wakiongea habari za dini wala chama chochote cha upinzani zaidi ya kuishambulia Ccm kwa nn mnapigana na chama ambacho hakipigani na nyie.....
halafu usiwasemee watu wa Dodoma labda kama we we ndo msemaji wa Dodoma
 
TBC, Radio Uhuru, Magazeti ya Mzalendo na Uhuru, habari leo, hivi vyombo vinaandika na kutangaza sana habari za ziara ya Zitto Kabwe kuliko vinavyotangaza ziara za Kinana..... Watanzania wengi wana akili hivyo wanajua kinachoendelea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…