Zitto atoa orodha ya wabunge wa upinzani wenye kesi mahakamani, walionusurika kuuawa na wale waliowahi kufungwa jela ktk utawala wa awamu ya 5

Hivi ile mahakama ya mafisadi (tena jengo lake lipo) inafanyakazi? Au Magu alitafakari na kukumbuka aliyoyafanya naye kupaswa kufikishwa kwenye ule mjengo kwa makosa aliyotenda kabla ya kuwa rais
 
Endelea kuishi kwa hisia!
 
Sio Nyerere tena manake alikuwa mpinzani wa wakoloni????!!!! Mwl. wenzio walimwita hivi hivi si unajua nyie mpo toka enzi na enzi.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwakani siyo mbali. Uchaguzi ndo huo na baadhi mulioifanya siasa ni ajira, majimbo ni giza! HUko magharibi pia muitikio ktk hoja zenu ni mdogo! Kila kitu kina mwisho. Siasa za upigaji mwisho ulishafika.
 
Mzee kiona mbali Kingunge alituusia: "Msimpeleke Ikulu MNYAMPARA". Maneno yake yanasadifu hivi sasa. Bahati mbaya hatukuwana choice nyingine. Lowasa hakufaa vile vile. Natamani kuwe na mgombea binafsi.
Afazali Lowasa. Kesi hizi na mauaji pamoja na utekaji usinge fikia kiwango hiki.
 
Wewe kiazi cha Magogoni.
 
Yuko wapi? Ameungana nao.
Bado unasema huyu alikuwa mpinzani?
 
Ni kufikiri kwa akili za kuazima tu ukidhani ni haki kuzushiana kesi uchwala hizi ili kunyamazisha kundi la wapinzani. Siku hawa wapinzani wakiisha atashitakiwa nani?

Kama uzwazwa huu ukiendelea 2020 CCM itapora viti vyote vya ubunge (maana haiwezi kushinda kwa haki bila msaada wa polisi). Tuone Kama mchawi hatatafutwa uvunguni. Angekuwa ni mbunge wa upinzani ndo katamka kwamba mbunge mwenzake anapaswa kutangulizwa (kuuawa) hata gerezani asingetosha nadhani. Ila kwa sababu yuko CCM ni sawa tu.

Mbeleni huko kuna maiti za watu zitafufuliwa ili tu zichapwe bakora
 
Kesi haichagui chama - toa na orodha ya wabunge wa CCM
Wabunge wa ccm waliofanyaje ?, nijuavyo mimi hakuna mbunge hata mmoja wa ccm aliyewahi kushitakiwa, kama mkurugenzi wa Itigi ameua mchana kweupe mpaka leo hii bado yuko ofisini, na kesi yake inaendesha kisaniikama vile hajaua, eti ushahidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…