Zitto asema hoja yao iko pale pale | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto asema hoja yao iko pale pale

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EasyFit, May 5, 2012.

 1. EasyFit

  EasyFit JF-Expert Member

  #1
  May 5, 2012
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 1,244
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe alisema mabadiliko hayo ya baraza la mawaziri hayatoi uhalali wa wao kutoa hoja yao ya kutaka waziri mkuu awajibike, bali uamuzi wa pamoja wa wabunge waliotia saini kutaka kupiga kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu ndiyo utakaofuatwa.

  Alisema kutokana na mabadiliko hayo Bunge limekuwa imara na limeonyesha dhamira ya kweli ya kuisimamia serikali kwa ajili ya maslahi ya wananchi na kwamba sasa taarifa ya CAG itakuwa inathaminiwa kwa kiwango kikubwa.

  “Ile dharau inayoonyeshwa na mawaziri katika ripoti mbali mbali juu ya wizara zao sasa tunaamini haitakuwepo na wataheshimu maamuzi ya kamati mbali mbali pamoja na taarifa ya CAG,” alisema Zitto.

  Aliongeza kuwa hatua hiyo ni kuelekea kujenga Bunge imara la kuweza kuwawajibisha watendaji wanaokiuka maadili na kushindwa kulinda mali ya umma.

  Filikunjombe aunga mkono

  Naye Mbunge wa Ludewa, Deo Fillikunjombe, ambaye katika Bunge lililopita alikuwa miongoni mwa vinara waliotaka mawaziri wawajibishwe kwa maslahi ya taifa alisema hatua hiyo ni nuru njema kwa Watanzania.

  Alirejea kauli yake kuwa maamuzi hayo ya kubadilishwa mawaziri ni kutokana na nguvu ya Bunge na kwamba wao walisimamia maslahi ya wananchi.

  Alisema ilikuwa ni kawaida kwa serikali kutofanyia kazi maazimio mbalimbali yanayotolewa bungeni na kwamba huo ni mwanzo wa kuhakikisha serikali inatambua kuwa Bunge lipo.

  CHANZO: Tanzania Daima
   
 2. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #2
  May 5, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Hoja iendelee kwa sababu mbona Maghembe na Mkuchika wameendelea kupeta wizarani?. Na vipi kuhusu hatua za kisheria dhidi ya hawa wezi!
   
 3. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #3
  May 5, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Kikubwa hapo ni juu ya hao wezi mawaziri na maibu wazir kama maghembe, malima bado wapo humo kwenye wizara. Pia tunataka wezi wawajibishwe ili liwe funzo.
   
 4. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #4
  May 5, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,799
  Likes Received: 3,884
  Trophy Points: 280
  maghembe. chiza, mwannri,, mkuchika wote niwatuhumiwa!!!anyway unajua jk ameshazoea kutuona sote ni wajinga au watoto! slaa alituonya kumchagua ni janga hatukusikia kwani utawala wake umejaa skendo tuu hakuna tija wala maendeleo
   
 5. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #5
  May 5, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Hoja ikibarikiwa kujadiliwa zito n cn watashindwa mbaya.Nadhani mnafahamu chama cha wanafiki
   
 6. E

  EMMANUEL NSAMBI JF-Expert Member

  #6
  May 5, 2012
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 402
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hivi Wana JF,
  Kwa yaliyotekea kwa mawaziri wetu,lugha sahihi ya kutumiwa ni kuwa walifukuzwa uwaziri au wamejiuzulu?
  Manake waligoma kujiuzulu mpaka JK alipotangaza wapya.Sasa tusija kesho kusikia mawaziri waliojiuzulu!
   
 7. THE BIG SHOW

  THE BIG SHOW JF-Expert Member

  #7
  May 5, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 13,929
  Likes Received: 1,861
  Trophy Points: 280
  zitto nae ni fisadi tuh
  atuambie hiii brand new range rover sport anayotamba nayo huku tabata kaipataje pataje hali ya kua yeye ni mbunge tuh?
  Familia yake maskin haina hata historia ya kumilimiki bajaji,leo kwa kazi ya kuwawakilisha wananchi wa kigoma kusini tuh hana biashara hana historia ya pesa kaipata pata vip luxury n expensive car kama hili?
  Tanzanians we r smarter than that
  tutairekebisha ccm ibadilike,waingie watu safi wachafu waondoke kuliko kuwapa watu wa siasa za maji machafu nchii hii waiharibu,watu wa ukanda,watu wa ukabila,watu wa udini
  katu kamwe hatuwez thubutu..!
   
 8. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #8
  May 5, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Hoja iendelee as bado kuna viwavi kwa baraza jipya.
  Huwezi mtoa kafala mkuu na kumrudisha mdogo
   
 9. Chakunyuma

  Chakunyuma JF-Expert Member

  #9
  May 5, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 811
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mbona hajasema what next? au wabunge waliotia sahihi watakutana ili kutoa uamuzi wa pamoja kuendelea na hoja yao na kama ndio hivyo watakutana lini?
   
 10. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #10
  May 5, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,276
  Trophy Points: 280
  Kuna ********* mmoja anaitwa Kigwangwalla alikataa kusaini fomu ya Zitto akidhani atachaguliwa kuwa Waziri wa afya, ******* kabisa huyu.
   
 11. Chakunyuma

  Chakunyuma JF-Expert Member

  #11
  May 5, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 811
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ficha upumbavu wako ukanda upi? ukabila gani? udini upi? acha kufikiri kijingajinga yaani badala ya kujenga hoja we unaanza kukashifu watu! what a shame? Tunarudishwa nyuma na watu wasiofikiria sawasawa.Je hujui ubadhilifu unahitaji kufuatiliwa ili wabadhilifu warudishe mali zetu na wahukumiwe kwa makosa yao? Je haudhani kwamba tukipunguza ufisadi kama sio kuuondoa kabisa tutapiga hatua kubwa ya kimaendeleo? Think big buddy!!!!
   
 12. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #12
  May 5, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Your thinking is too low and pathetic.
   
 13. Kiona

  Kiona JF-Expert Member

  #13
  May 5, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 936
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35

  Wamesahaulika
   
 14. Mark Francis

  Mark Francis Verified User

  #14
  May 5, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 605
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  JK kaishiwa watu, mkitaka wavunje tena baraza la mawaziri itabidi achague wabunge wapya ili awape tena uwaziri.... Tumuache sasa atulie manake atakonda kwa pressure!!
   
 15. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #15
  May 5, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,539
  Likes Received: 10,460
  Trophy Points: 280
  kweli mkuu kwa maana ile sura na kauli za jana jamaa anaonekana safari hii ameamua.
   
 16. sun wu

  sun wu JF-Expert Member

  #16
  May 5, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 2,025
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 0
  Hii ndio good news ya kwanza kuipata baada ya usanii wa jana

  kubadilisha baraza la mawaziri jana hakuonyeshi kwamba jana Pinda kaanza kufanya kazi..

  Kama alikuwa hana meno sio kweli kwamba meno kayapata jana
   
 17. measkron

  measkron JF-Expert Member

  #17
  May 5, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 3,713
  Likes Received: 365
  Trophy Points: 180
  Mkuu hao jamaa wamefukuzwa, JK banaaa! Mwanzo aliwaambia huo ni upepo tu utapita kumbe alikuwa anawalia timing wasijiuzulu na sasa amewafukuza!! Aibu... Hawa mawaziri wangesoma alama za nyakati na kujiuzulu kuliko kusubiri kufukizwa
   
 18. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #18
  May 5, 2012
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  [​IMG]

  Watanzania hamna shukrani kabisa, mbona tayari mitambo wa kusaga pesa zetu zimefumuliwa?  [​IMG]
   
 19. THE BIG SHOW

  THE BIG SHOW JF-Expert Member

  #19
  May 5, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 13,929
  Likes Received: 1,861
  Trophy Points: 280
  my thinkin is too low and pathetic
  sawa,so according to you great thinker what makes u to believe that chadema will change the situation?
  Dont u realize that hao pia wanapigania matumbo yao?
  Me nashangaaa sana watz kwa kukaa na kutemegemea kua wanasiasa watabadilisha hali ya nchi hii na kuacha jambo muhim la kufanya waamuz wa mambo ya nchi hii wawe wenyew wananch kwa kuihangaikia na kuhamishana kuhus katiba yenye muelekeo,whats the difference btn slaa na jk?lipumba n mbatia?maalim seif n mrema?
  Wote walikua ccm,wote wanapigania matumbo yao?
  Ktk msafara wa mamba kenge pia wamo,acha kufuata mkumbo kama kenge,et great thinker..!great thinker utakua wewe?
  Wanasiasa wote ni wanafiki nan asiejua?badala ya kukaa na kuhangaikia katiba itayobadilisha muelekeo wa nchi wewe umekaa m4c..!m4c..!haya wakija kufanya madudu zaid ya haya utafanya nin?utalilia changes zingne?
  U think mbowe,slaa,zitto gives a damn bout you?
  Litakuchwea na naona mishipa ya shingo inakutoka kushupalia ulafi wa wenzake kwa rasilimali za wanyonge wadanganyika
  chadema ni wakanda,wakabila,wadini
  kama ilivokawa cuf pia,,na kuitoa ccm wafanye kazi kweli kweli
  sio kirahis kama wanavofikiria..!
   
 20. vipik2

  vipik2 JF-Expert Member

  #20
  May 5, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 1,175
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Nyambafu huyu alikuwa anatusumbua kumsubiri uwanja wa ndege Mwanza kisa eti yeye ni Waziri

  [​IMG]
   
Loading...