Zitto aongoza kwa umaarufu bungeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto aongoza kwa umaarufu bungeni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Josh Michael, Feb 23, 2010.

 1. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #1
  Feb 23, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Nora Damian


  MBUNGE wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe ameendelea kuwa mbunge maarufu kisiasa kuliko wabunge wote, huku akiwaacha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Spika wa Bunge Samuel Sitta wakiporomoka, utafiti uliofanywa na kampuni ya Synovate umeonyesha.

  Kampuni hiyo ambayo zamani ilikuwa inajulikana kama Steadman Group Tanzania, imetoa ripoti ya utafiti huo jana baada ya kuwahoji uso kwa uso watu 2,000 waliogawanywa sawa na uwiano wa idadi ya Watanzania.

  Kwa mujibu wa utafiti huo, Zitto aliongoza kwa kupata asilimia 31 ya kura zote akifuatiwa na Anne Kilango asilimia 13, Dk Willibrod Slaa asilimia 7, Dk Harison Mwakyembe asilimia sita, John Magufuli tatu na Lawrence Masha asilimia mbili.

  Pinda na Sitta, wamepata asilimia moja ya majibu ya swali lililowataka wahojiwa kumtaja mbunge ambaye ameonekana kufanya vyema katika kipindi cha mwisho cha mwaka 2009 na kutoa sababu za kumchagua mbunge huyo.

  Akitangaza matokeo ya utafiti huo jana meneja utafiti wa kampuni hiyo Abdalah Gunda aliwataja
  wabunge wengine waliopata asimilia moja katika swali hilo kuwa ni Philemon Ndesamburo na David Mathayo.

  Wengine ni Mark Mwandosya, Jenista Mhagama, John Nchimbi, Halima Mdee, Mohamed Dewji, John Cheyo na Hamisi Kagasheki.

  Hata hivyo alisema asilimia 21 ya watu walioulizwa swali hilo hawakuwa na jibu.

  Utafiti umeeleza msingi wa majibu ya swali hilo la umaarufu, ni mbunge kuwa mstari wa mbele katika kufichua maovu hasa rushwa na kusema ukweli bungeni.

  Sababu nyingine ni kuwasilisha matatizo ya wananchi wao, kufanya kazi nzuri katika majimbo yao, kuwa na mikakati mizuri ya kuleta maendeleo, kuwa wawazi na kuleta changamoto kwa wabunge wengine.
  Gunda alisema maswali mengine yaliyoulizwa katika utafiti huo ni 'Kama uchaguzi utafanyika leo, je utapiga kura? Na Unapofikiria Demokrasia, Tanzania ipo na katika hali gani?'

  Maswali mengine ni ' ni chama gani cha siasa ambacho uko karibu nacho, nani ungependa awe rais wako?'

  Alisema lengo la utafiti huo ilikuwa kupata maoni ya Watanzania katika mambo ya kijamii, kisiasa na kiuchumi ambayo ni muhimu katika kuimarisha agenda ya kitaifa ya uundwaji sera na mikakati ya kimaendeleo.

  Alisema utafiti huo uliofanywa kwa kipindi cha miezi mitatu; Oktoba hadi Desemba, umeonyesha kuwa CCM inaongoza kwa kupendwa na wananchi kwa asilimia 70 ikifuatiwa na Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na Chama Cha Wananchi (CUF).

  Chadema inachukua asilimia 17 na CUF asimilia tisa ya watanzania wote.

  Kwa mujibu wa Gunda, vyama vya UDP, TLP na NCCR-Mageuzi vinapendwa na Watanzania kwa asilimia moja.

  Alisema utafiti umeonyesha kuwa Rais Jakaya Kikwete atashinda kiti cha urais katika uchaguzi huo kwa asilimia 75 akifuatiwa na Freeman Mbowe wa Chadema aliyepata asilimia 10 na Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF mwenye asilimia tisa.

  Gunda alisema majibu ya swali lililowataka Watanzania kueleza wanayempenda kuwa rais wao yametoa nafasi ndogo kwa Zitto Kabwe, Dk Salim Ahmed Salim na John Cheyo.

  Wanasiasa hao wamepewa asilimia moja kila mmoja katika uwezekano wa kushinda kiti hicho. Asilimia mbili ya watu waliohojiwa walisema hawajui nani angefaa kuwa rais wao.

  Utafiti umeonyesha kuwa asilimia 94 ya Watanzania wamesema wako tayari kupiga kura katika uchaguzi mkuu huu na asilimia tano walisema hawatapiga kura.

  “Wengi wa wahojiwa ambao tuliwauliza sababu za kutopiga kura walisema wamechoshwa na mambo ya siasa, rushwa na wengine walidai wagombea hawawasaidii kitu chochote,” alisema Gunda.

  Alisema asilimia 57 ya watu waliohojiwa kuhusu demokrasia walisema wanaamini demokrasia ipo lakini, bado ina matatizo kidogo.

  "Asilimia 15 walisema kuna matatizo makubwa ya demokrasia nchini, asilimia tatu walisema Tanzania hakuna demokrasia na asilimia nne hawakuwa na jibu katika swali hilo,"alieleza Gunda.
  Huu ni utafiti wa kwanza kutolewa na kampuni hiyo mwaka huu. Utafiti wa mwisho wa aina hiyo ulitolewa Julai mwaka jana na kumpa maalimu Seif Sharif Hamad nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi mkuu mwaka huu kwa nafasi ya urais Zanzibar
   
 2. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #2
  Feb 23, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  jamni mbona mnarudia mapost yaliyokwisha tumwa?hii habari imeshapostiwa tangu jana na habari ndio hiyi hebu ifauatilie vizuri
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...