Zitto aomba kuchangiwa mtandaoni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto aomba kuchangiwa mtandaoni

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Pengo, Aug 23, 2010.

 1. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #1
  Aug 23, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Zitto Zuberi Kabwe amejipanga kikamilifu kulitetea jimbo lake la Kigoma Kaskazini na kurudi bungeni kwa kuweka program ya michango mitandaoni.

  Kwa mujibu matangazo aliyoyaweka kwenye ukurasa wake wa Facebook, Zitto ametoa nambari mbalimbali za akaunti na kuwataka Watanzania wanaomuunga mkono, wamchangie fedha ili kutunisha mfuko wake wa kampeni.

  Katika maelezo yake, Zitto amewataka Watanzania wenye ni maendeleo ya demokrasia kumchangia ili aweze kurudi bungeni.

  “Tayari nimekabidhi fomu zangu kwa ajili ya kugombea ubunge Jimbo la Kigoma Kaskazini ili kuwatumikia tena wananchi wa Kigoma Kaskazini na Tanzania kwa jumla. Mimi nipo tayari,” ilisema taarifa ya Zitto Mtandaoni.

  Katika maelezo yake, Zitto alizitaja nambari za akaunti benki ya CRDB, 01J2082022500 ZITTO KABWE ZUBERI na NMB, 2012510971 KABWE ZUBERI ZITTO.

  Gazeti hili lilipowasiliana na Zitto wikiendi iliyopita alisema: “Nimeita michango mitandaoni kwa sababu naamini wengi wangependa kunichangia ili kukuza demokrasia. Wadau wanaweza kunipata kwa namba 0756-809535 na wakiweza wanitumie kwa M-Pesa.”

  Chanzo:-Global Publishers
   
 2. Nicky82

  Nicky82 JF-Expert Member

  #2
  Aug 23, 2010
  Joined: Mar 14, 2009
  Messages: 939
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tumekupata Mheshimiwa Zitto.

  Vipi kuhusu Raisi wetu Mtarajiwa Dk.Slaa kuna utaratibu gani umewekwa wa kumsupport??
   
 3. W

  WildCard JF-Expert Member

  #3
  Aug 23, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Tangazo lake hili limo pia kwenye gazeti la Mwananchi. Hata Ubunge wetu kwa mtu maarufu kama Zitto anahitaji mapesa mengi kiasi hiki!? Kile kiinua mgongo kisingetosha? Zile posho zote za ile tume ya madini, za vikao vya kamati yake ya mashirika ya UMMA, za vikao vya kawaida vya Bunge,.....Zitto, bado unatamani kuwachangisha watu masikini kabisa wa Nchi hii? Aibu.
   
 4. BinMgen

  BinMgen JF-Expert Member

  #4
  Aug 23, 2010
  Joined: Jun 18, 2008
  Messages: 1,816
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  kutoa ni moyo na wala si utajiri
   
 5. Joseph

  Joseph JF-Expert Member

  #5
  Aug 23, 2010
  Joined: Aug 3, 2007
  Messages: 3,527
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Kampeni si lelemama kama unavyodhani,hukuona tu wana CCM walivyotumia pesa nyingi katika kutafuta nafasi ya kuteuliwa?Kwa mtu kama Zitto kuomba kuchangiwa ni jambo la kawaida maana hata CCM wanaendesha harambee kila kukicha na hakuna hata mmoja aliyesema kuwa pesa nyingi wanazopata kama ruzuku zinakwenda wapi.
  Katika mambo ya msingi tuwe waungwana na tuchangie na kama hatuwezi basi tusibeze harakati za mapinduzi katika demokrasia.
   
 6. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #6
  Aug 23, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  sasa mbona zitto hajaja na humu kutoa tangazo? au ametoa sijaliona mie mwenzenu?:confused2:
   
 7. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #7
  Aug 23, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ina maana Zitto alikuwa hajajitayarisha mpaka wakati huu ndio anaomba achangiwe! Je, ana wasiwasi jimboni kwake hawamkubali kama tunavyodhania? Kwa nini hawamkubali wakati yeye ni maarufu? Kwa umaarufu wake angeliweza kupita bila kupingwa.
   
 8. W

  WildCard JF-Expert Member

  #8
  Aug 23, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Kwa Tanzania, Ubunge ni mali ya mtu mwenyewe. Unamsaidia yeye zaidi kama ulivyo utumishi mwingine wowote katika NCHI hii. Ni afadhali kama ingekuwa ni mara ya kwanza anagombea. Wabunge wote wamelipwa mamilioni juzi. Na Zitto hana majukumu ya kifamilia ya kutisha. Wapiga kura wetu wengi mazuzu! Ukimpa elfu moja anachekeleea. Zitto angeita wazito wenzake wachache akawachangisha basi. Vinginevyo baadhi yetu tutashindwa kumtofautisha na akina Kakobe, Mwingira, Mzee wa upako,......
   
 9. Nicky82

  Nicky82 JF-Expert Member

  #9
  Aug 23, 2010
  Joined: Mar 14, 2009
  Messages: 939
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Watu wengine bhana ni watu wa ajabu sana!! Kwani kuchangia kampeni no kaanzisha Zito??

  Ni imani yangu huo mchango hautamsaidia Zitto peke yake, kuna na madiwani pia.
  michango ya kampeni ni kitu cha kawaida kabisa, wala sijaona nn cha kushangaza hapo.

  Go! Zitto Go! were just behind you,Mbowe na Slaa katika harakati za kulikomboa taifa hili lenye madini ya kila aina na wanyama wasiopatikana kwingine kokote duniani zaidi ya hapa kwetu.
   
Loading...