Kizimbuzi
JF-Expert Member
- Jul 31, 2013
- 1,569
- 743
Zitto amekuwa akidai kuwa, Dr. Shein anatenda kosa la uhaini kwa kuendelea kuwa madarakani Zanzibar, kinyume na katiba. Kisheria, Serikali ya Zanzibar haiwezi kutendewa uhaini maana Zanzibar si dola huru. Ili entity iwe dola huru inahitaji kuwa na:
1. watu, 2. serikali 3. mipaka 4. uhuru (uhuru wa ndani na nje). Zanzibar ina sifa tatu pekee ambazo ni kuwa na watu, serikali, na mipaka ila haina uhuru wa ndani na nje. Haina uhuru wa nje kwa sababu haina uwezo kusaini mikataba na mataifa ya nje, haina kiti umoja wa mataifa, na haitambuliki kama moja nchi huru duniani.
Haina uhuru wa ndani maana sheria zake zinatungwa na Tanzania na kutekelezwa/kusimamiwa na Tanzania. Kwa hiyo, hata kama leo hii mtu 'akiipindua' serikali ya Zanzibar, hawezi kupatikana na kosa la uhaini. Zitto, kama msomi wa sheria, aache kupotosha umma.