Zitto anapotosha umma kuhusu uhaini Zanzibar

Kizimbuzi

JF-Expert Member
Jul 31, 2013
1,569
739
Zitto amekuwa akidai kuwa, Dr. Shein anatenda kosa la uhaini kwa kuendelea kuwa madarakani Zanzibar, kinyume na katiba. Kisheria, Serikali ya Zanzibar haiwezi kutendewa uhaini maana Zanzibar si dola huru. Ili entity iwe dola huru inahitaji kuwa na:

1. watu, 2. serikali 3. mipaka 4. uhuru (uhuru wa ndani na nje). Zanzibar ina sifa tatu pekee ambazo ni kuwa na watu, serikali, na mipaka ila haina uhuru wa ndani na nje. Haina uhuru wa nje kwa sababu haina uwezo kusaini mikataba na mataifa ya nje, haina kiti umoja wa mataifa, na haitambuliki kama moja nchi huru duniani.

Haina uhuru wa ndani maana sheria zake zinatungwa na Tanzania na kutekelezwa/kusimamiwa na Tanzania. Kwa hiyo, hata kama leo hii mtu 'akiipindua' serikali ya Zanzibar, hawezi kupatikana na kosa la uhaini. Zitto, kama msomi wa sheria, aache kupotosha umma.
 
Zitto si Mwanasheria. Ni layperson na hajui chochote kuhusu Sheria na hasa tafsiri ya uhaini.Amesema hivyo kama Mwanasiasa tu. Labda mtafutie kesi ya akina Juma Duni Haji ili imuongoze kuhusu tafsiri ya Uhaini hasa inapohusika Zanzibar. Msamehe bure Mkuu
 
Namshauri zito atulie kama ananyolewa. Pilipili iliyo shamba yamuwashiani? Ndugu wakigombana shika jembe ukalime.
 
Zitto si Mwanasheria. Ni layperson na hajui chochote kuhusu Sheria na hasa tafsiri ya uhaini.Amesema hivyo kama Mwanasiasa tu. Labda mtafutie kesi ya akina Juma Duni Haji ili imuongoze kuhusu tafsiri ya Uhaini hasa inapohusika Zanzibar. Msamehe bure Mkuu

Nimemsamehe mkuu. Ila imewahi kuripotiwa kuwa amesoma law na kafanya internship kwa Mkono.
 
Zitto si Mwanasheria. Ni layperson na hajui chochote kuhusu Sheria na hasa tafsiri ya uhaini.Amesema hivyo kama Mwanasiasa tu. Labda mtafutie kesi ya akina Juma Duni Haji ili imuongoze kuhusu tafsiri ya Uhaini hasa inapohusika Zanzibar. Msamehe bure Mkuu

mkuu ili mtu awe mwanasheria inahitajika nini? nakumbuka alisema degree ya pili alifanya sheria na kuna wakati alikuwa kwa mkono advocate wakati amemaliza au akiendelea ana elimu yake
Naomba kueleweshwa
 
..naona hii imekaa kisheria zaidi,na kama kweli alikuwa na mtazamo huo basi alipotoka kimktadha wa kisheria..
 
Zitto kaliongea kisiasa ila before the eyes of law inajulikana Zanzibar is not a state.
 
Last edited by a moderator:
Wachangiaji wote wameliona hili la uhaini tu; je uhalali wa Dr Shein kuendelea kuwa madarakani hebu tupeni ufafanuzi wa kesheria.
 
Mnakumbuka zegere lililotokea baada ya Pinda kusema Zanzibar sio nchi?
Kumbukeni hilo linganisheni na na haya mnayoyasema sasa hivi.
 
Zitto si Mwanasheria. Ni layperson na hajui chochote kuhusu Sheria na hasa tafsiri ya uhaini.Amesema hivyo kama Mwanasiasa tu. Labda mtafutie kesi ya akina Juma Duni Haji ili imuongoze kuhusu tafsiri ya Uhaini hasa inapohusika Zanzibar. Msamehe bure Mkuu

Hakuna neno uhaini katika ushauri wa zitto......ww kitu chochote atakachosema zitto lazima upinge.

Sasa tueleze uhalali wa Shein kubaki madarakani
 
S.M.Z. vs. Machano Khamis Ali & Others (Criminal Application No. 8 of 2000) [2000] TZCA 1 (21 November 2000)

hii case ndio itawapa muungozo kuhusu zanzibar achaneni na zito kabwe he think not like a lawyer but a politician
 
mkuu ili mtu awe mwanasheria inahitajika nini? nakumbuka alisema degree ya pili alifanya sheria na kuna wakati alikuwa kwa mkono advocate wakati amemaliza au akiendelea ana elimu yake
Naomba kueleweshwa

Mwanasheria ni mtu yeyote mwenye Shahada ya Kwanza ya Sheria (Bachelor of Laws) na si vinginevyo.Si Shahada ya pili (Master of Laws) ya tatu (Ph.D) Stashahada (Diploma) wala Astashahada (Certificate)ya Sheria.
 
Kifupi ili uwe mwanasheria lazima uwe na LLB yeye hana eti degree ya pili tehetehetehe!
 
Hili lipo wazi hakuna uhaini dhidi ya Zanzibar maana siyo nchi rejeeni kauli ya mwanasheria mizengo pita pinda
 
Zitto si Mwanasheria. Ni layperson na hajui chochote kuhusu Sheria na hasa tafsiri ya uhaini.Amesema hivyo kama Mwanasiasa tu. Labda mtafutie kesi ya akina Juma Duni Haji ili imuongoze kuhusu tafsiri ya Uhaini hasa inapohusika Zanzibar. Msamehe bure Mkuu

Hee kumbe ndo maana ya uhaini? Sasa mbona Tindu Lissu yalimtoka mate alipokua ana report kufukuzwa ZZK chadema alimuita "mhaini"?au chadema ni dola?maana nasikia hata portfolio ya EL ni Rais ndani ya CDM?
 
Back
Top Bottom