Stabilaiza
JF-Expert Member
- Jul 11, 2012
- 1,843
- 1,143
Pamoja na kuwa Zitto anapendwa na wana-CCM, jambo moja linanishangaza sana. Sielewi ni kwa nini Zitto anamshupalia sana mh. Pinda. Kuna wakati alifikia hatua ya kukusanya saini ili Pinda ajiuzulu. Halafu akasema Pinda analipwa mshahara wa milioni 30. Halafu issue inapotokea bungeni Zitto anamng'ang'ania Pinda ajiuzulu, kwa nini? Hivi karibuni Pinda alisema kuwa Zitto anamzushia uwongo hadi Mh. Pinda akataja mshahara wake kuwa ni mil 6 na pia akataja mshahara wa rais.
Je Zitto anafanya kampeni aliyotumwa ili mtu wao aje kuwa waziri mkuu? Nina wasiwasi Zitto ametumwa na mtu mzito katika CCM na mkubwa katika serikali ili Pinda aondolewe kwenye uwaziri mkuu na huyo mtu wao waliyemuandaa apewe nafasi hiyo. Vinginevyo sioni kwa nini Zitto kila wakati anamwandama mh. Pinda. Kama ndivyo Zitto anafaidika vipi katika kampeni yake ya kumwondoa Pinda kwenye uwaziri mkuu?