Ally Kanah
JF-Expert Member
- Jun 7, 2011
- 1,479
- 388
Kuchukua au kutochukua posho za vikao kama mbunge ni suala la misingi (principles) na sio suala la uwezo kifedha. Kuna wabunge matajiri sana lakini wakachukua posho na wengine wa kawaida kabisa hatuchukui posho. Sio posho tu, hata msamaha wa kodi wa kuingia magari nimeukataa sababu ya misingi tu, kwamba siwezi kuwa Waziri kivuli ninayepinga misamaha ya kodi wakati huo huo nikachukua misamaha ya kodi. Ninaamini katika siasa za kutenda ninachosema. Mjadala wa posho kwangu mimi nimeufunga toka Juni 8, 2011 nilipoacha kupokea posho za vikao. Mwaka huo pia nilikataa msamaha wa kodi ya kuingia gari. Ni msimamo tu, hapa mtu hupendi msimamo wangu isiwe uadui, wewe endelea kuchukua posho, omba ziwe nyingi zaidi na wala sitatia neno kwenye msimamo huo japo nitaudharau maana posho za vikao ni kuwaibia wananchi ambao hawana maji safi na salama, watoto wao hawana walimu sababu Serikali haiwalipi walimu vizuri, kina mama waja wazito wanakufa kutokana na huduma mbovu za afya huko vijijini nk. Haya ndio masuala ya wananchi wetu na sio kudai kuongezewa posho.
Habari wakuu,
Naomba nianze kwa kusema wazi kuwa naamini mimi kama watanzania wengine wengi ni muathirika wa utawala dhalimu wa serikali ya CCM na hivyo ni mtu nae tamani sana kuona ukombozi unapatikana kwa gharama yoyote ile ili tuondokane na huyu mkoloni mweusi (CCM).
Hata hivyo,nakiri kuwa vita hii ya ukombozi ni ngumu kwasababu makamanda wetu wana njaa.Unaweza ukawa na mshahara(kipato) kikubwa tu lakini kama hujaridhika wewe huna tofauti na mtu mwenye njaa na kwa lugha nyepesi njaa inakusumbua na mbaya zaidi ni kama utashindwa kudhibiti njaa yako.
Matokeo ya mtu kushindwa kudhibiti njaa yake na hapa nalenga wanasiasa wanaodai kutafuta ukombozi wa nchi hii hii ni kams haya yafuatayo:-
Usaliti:Mtu mwenye njaa ni rahisi kurubumiwa kwa fedha na kuwageuka wanaharakati wenzake.
Uroho wa madaraka:Mtu mwenye njaa anaamimi kupitia madaraka aliyonayo anaweza kutimiza malengo(mahitaji) yake.
Kung'ang'ania madaraka:Mtu mwenye njaa ana sifa ya kung'ang'ania madaraka kwani akiacha njaa yake haitaisha.
Majungu,fitina,uongo na umbeya:Mtu mwenye njaa siku zote hutumia mbinu chafu ili kumuhujumu yule ambae anaamini kuwa ni kikwazo kwake katika kuondokana na njaa yake.
Ubinafsi:Ubinafsi siku zote ni matokeo ya njaa.
Sasa wakati tunatamani na kulilia ukombozi tunapaswa kujiuliza kama wanasiasa wetu si watu wenye sifa hizo za mtu mwenje njaa.
Zitto katika Facebook wall yake leo.
Kuchukua au kutochukua posho za vikao kama mbunge ni suala la misingi (principles) na sio suala la uwezo kifedha. Kuna wabunge matajiri sana lakini wakachukua posho na wengine wa kawaida kabisa hatuchukui posho.
Sio posho tu, hata msamaha wa kodi wa kuingia magari nimeukataa sababu ya misingi tu, kwamba siwezi kuwa Waziri kivuli ninayepinga misamaha ya kodi wakati huo huo nikachukua misamaha ya kodi. Ninaamini katika siasa za kutenda ninachosema. Mjadala wa posho kwangu mimi nimeufunga toka Juni 8, 2011 nilipoacha kupokea posho za vikao.
Mwaka huo pia nilikataa msamaha wa kodi ya kuingia gari. Ni msimamo tu, hapa mtu hupendi msimamo wangu isiwe uadui, wewe endelea kuchukua posho, omba ziwe nyingi zaidi na wala sitatia neno kwenye msimamo huo japo nitaudharau maana posho za vikao ni kuwaibia wananchi ambao hawana maji safi na salama, watoto wao hawana walimu sababu Serikali haiwalipi walimu vizuri, kina mama waja wazito wanakufa kutokana na huduma mbovu za afya huko vijijini nk.
Haya ndio masuala ya wananchi wetu na sio kudai kuongezewa posho.