Zitto amshangaa Pinda kufunga mdomo vurugu Arusha

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
234
Zitto amshangaa Pinda kufunga mdomo vurugu Arusha


NAIBU Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe amesema anashangazwa na ukimya wa Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuhusu mgogoro wa kisiasa uliozuka mkoani Arusha na kuwa chanzo cha vurugu zilizosababisha vifo vya watu watatu na kujeruhi wengine zaidi ya 20.

Kabwe, ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini alisema jana kuwa Pinda ana mamlaka ya kuingilia kati suala hilo hasa ikizingatia limetokea kwenye ngazi za kiserikali ambazo zimo chini yake.

Alisema sheria ya miji ya mwaka 1982 inampa mamlaka Waziri Mkuu kutoa agizo la kufuta uchaguzi na kuamuru kufanyika uchaguzi mwingine ulio huru na haki pindi inapobainika taratibu hazikufaatwa katika uchaguzi husika. “Tatizo la Arusha na uchaguzi wa Meya ulifanywa kinyume na taratibu na sheria za uchaguzi zimekiukwa," alidai Zitto kwenye mahojiano na Shirika la Utangaza la Uingereza (BBC), jana.

Alisisitiza kwamba vurugu za Arusha ni “tatizo la uchaguzi wa Meya na mwenye dhamana ya kufuta na kuamru kufanyika kwa uchaguzi mwingine ulio huru na haki ni Waziri Mkuu. Nashangaa yeye kukaa kimya wakati kila kitu kinaeleweka,” alisema. Alisema miongoni mwa mambo yaliyokiukwa ni pamoja na CCM kumuingiza mbunge mmoja wa viti maalumu Marry Chatanda kupiga kura kinyume na sheria.

Alisema Chatanda ambaye ni katibu wa CCM Mkoa wa Arusha si mwakilishi wa Mkoa huo na kwamba ni mbunge anayewakilishi mkoa wa Tanga ambaye kisheria hakusitahili kupiga kura kwenye uchaguzi huo. “Mgogoro wa Arusha si ugomvi baina ya CCM na Chadema wala Chadema na Jeshi la Polisi, bali umetokana na ukiukwaji wa makusudi wa sheria na taratibu za uchaguzi wa Umeya, uliowanyima madiwani wa Chadema ambao ni wengi kupiga kura,” alisema Zitto.
Katika hatua nyingine mmoja wa washiriki wa maandamano hayo, Dadi Igogo alilieleza Shirika hilo la utangazaji la BBC namna alivyopigwa na polisi na kuwekwa rumenda bila hata ya kupelekwa hosptalini licha ya kuumizwa vibaya.

Alisema Polisi walikamata na kumpiga kisha kumtupa kwenye gari lao na walipokuwa wanaenda kituoni walimkanyaga na kumsababishia maumivu sehemu mbalimbali hususan, kiuno.

Alisema mara baada ya kufikishwa kituoni alitupwa rumande na kwamba licha ya kuwaomba askari hao kumpeleka Hosptali walikataa na kumlazimisha kulala humo hadi kesho yake mchana. “Mimi nilipigwa na hata nilipowaomba wanapeleka hosptalini walikataa na kunilaza ndani hadi siku ya pili tulipotolewa na kupelekwa mahakamani ndipo nilipopata fursa ya kwenda kutibiwa,” alisema Igogo.

Igogo ambaye awali alikuwa akifanya kazi za kisheria katika makao makuu ya Chadema alisema akiwa kituoni alishuhudia ukiukwaji wa haki za binadamu.

“Nikiwa ndani, aliletwa mtu akiwa anabubujika damu lakini polisi walikataa kumpeleka hosptalini licha ya watu wengi kushauri walidharau. Mbaya zaidi alibaki huko hata mimi nilipotoka jana (juzi) yeye nilimuacha humo bila ya matibabu yoyote” alisema Igogo wakati akihojiwa na BBC.

Chanzo: Mwananchi JUMAPILI
 
Na huyo waziri wake wa TAMISEMI, Mkuchika, mbona kimya naye? Kule kwake Newala hakushinda, walichakachua. Mwaka juzi alizomewa na wapiga kura wake mbele ya Pinda kutokana na tatizo la maji. Wengi wameshangaa kwa nini kapewa tena uwaziri, ambao unamshinda.

Angalau katika wizara yake ya awali alikuwa anajishughilisha kidogo, kukabidhi timu zetu bendera kwenda kufanya aibu katika mashindano nchi za nje, na kufungia magazeti.
 
Nchi hii tangu kupata uhuru haijawahi kuwa na waziri mkuu asiye na maamuzi kama Pinda........nikweli sio mwizi lakini hana nguvu za kiutendaji hivyo napata mashaka kama nafasi hiyo inamfaa.............Hawa ni watu walio zoea kufanya kazi chini ya mtu hakika ni mchapakazi akifanya kazi kwa maelekezo.
 
Jamani mnapigia mbuzi gitaa Pinda ni kopo tupu hajui hata kwanini ni waziri mkuu.
 
Pinda is a stooge!
Ni kwamba anajaza tu hitajio la katiba la kuwa na waziri mkuu!
 
Nyinyi kama ni wasomi wa kweli na mna habari za kiintelejinsia mngeweza kupekuwa huko tutokako ,Pinda ni nani ,alikuwa nani,alipokuwa huko ni misheni gani alizitekeleza au zilitekelezwa chini ya uongozi wake mkijua yote hayo hamtashindwa kuelewa kwa nini anakaa kimya kwenye mambo kama haya !
 
Nyinyi kama ni wasomi wa kweli na mna habari za kiintelejinsia mngeweza kupekuwa huko tutokako ,Pinda ni nani ,alikuwa nani,alipokuwa huko ni misheni gani alizitekeleza au zilitekelezwa chini ya uongozi wake mkijua yote hayo hamtashindwa kuelewa kwa nini anakaa kimya kwenye mambo kama haya !
a bit of crap!
 
nyinyi kama ni wasomi wa kweli na mna habari za kiintelejinsia mngeweza kupekuwa huko tutokako ,pinda ni nani ,alikuwa nani,alipokuwa huko ni misheni gani alizitekeleza au zilitekelezwa chini ya uongozi wake mkijua yote hayo hamtashindwa kuelewa kwa nini anakaa kimya kwenye mambo kama haya !

c.r.a.p
 
hebu weka historia ya Pinda hapa ,inawezekana huelewwi huyu mtu alikuwa akifanya kazi gani.hulaumiki.
HEAVY CRAP!
.
.
Wewe unashindwa kutumia kompyuta yako?
Kwanini nikuwekee mimi..soma!
 
Pinda hawezi kufanya lolote ktk hili kwa kuwa naye ni ccm,na ndio waliosababisha yote haya.Kitendo cha yeye kutoa kauli atakuwa anawaumbua wenzake na chama chake,pia itadhihirika wazi kuwa walifanya umafia.Kauli yoyote atakayotoa inayolenga kulaani kilichotokea Arusha kinapaswa kuenda sanjari na kuwawajibisha wote walisababisha mgogoro huu....!
 
Back
Top Bottom