Zitto
Former MP Kigoma Urban
- Mar 2, 2007
- 1,562
- 10,886
Jana nilipokuwa natoa mada kuhusu miaka 50 ya Azimio la Arusha niliongelea pia suala la umakini wa viongozi katika kauli zao. Kwamba Kiongozi lazima ujue unatoa kauli gani wakati gani. Niliwaeleza wanachama na wageni wengjne katika mkutano wa ACT Wazalendo kuwa Amri ya kiholela aliyoitoa Rais John Magufuli kuzuia usafirishaji wa Mchanga wa Dhahabu imepelekea nchi yetu kupoteza USD 880m Kama kodi ya ongezeko la Mtaji kutokana na mauzo ya Acacia Mining.
Hivi sasa nchini kwetu kuna sheria ya kutoza 20% ya thamani ya mauzo iwapo kampuni zinauziana hisa. Tozo inayotozwa inaitwa Capital Gains Tax. Kodi hii mpya ilitungwa mwaka 2012 ili kukabili wawekezaji waliokuwa wanauziana makampuni juu Kwa juu bila Tanzania kupata lolote. Tanzania imeshafaidika na kodi hiyo Kwa mauzo mbali mbali ambayo yamekwisha fanyika kwenye sekta mbalimbali.
Wakati Rais anatoa AMRI kuhusu Mchanga wa madini kusafirishwa kwenye nje ya nchi kulikuwa na mazungumzo yanaendelea kati ya Kampuni ya Acacia mining ( yenye Assets zinazozalisha nchini Tanzania tu kwa sasa - Buzwagi, Bulyanhulu na North Mara) na kampuni nyengine ya nchini Canada kuhusu Acacia kununuliwa Kwa USD 4.4bn. Mara baada ya amri hiyo mazungumzo yalivunjika na hivyo mauzo kutofanyika.
Iwapo Rais angechelewa kutoa kauli yake Kwa wiki moja tu mazungumzo yale yangepelekea mkataba wa mauzo kusainiwa na hivyo Serikali ingepata 20% ya thamani ya Mauzo Kama kodi ya Ongezeko la Mtaji ( capital gains tax ). Hivyo kauli ya Rais imesababisha hasara Kwa nchi yenye thamani ya USD 880m sawa sawa na shilingi 1.8 trilioni.
Tafiti zinaonyesha kuwa gharama ya kujenga ' refinery ' ya kuchenjua dhahabu hapa nchini ni USD 800m. Hivyo mapato ambayo yangepatikana kutokana na kodi ya mauzo ya Acacia yangewezesha nchi kujenga refinery na kufikia lengo la Rais la kuwa na uchenjuaji wa mchanga ule hapa hapa nchini. Rais angetulia angeweza kuua ndege wawili Kwa jiwe moja, 1) kiwanda cha kuchenjua kingejengwa nchini na 2) mchanga usingesafirishwa tena kwenda China na Japan.
Hata hivyo Tanzania haina mchanga wa kutosha wa kushibisha hiyo refinery Kwa mujibu wa teknolojia ya sasa ( soma maelezo yangu hapa chini Kwa Mhariri wa RaiaMwema). Hivyo Rais angeweza kutumia mapato hayo Kwa matumizi mengine ya Maendeleo. Kwa mfano Bunge lilitenga kama USD 430m hivi kujenga Reli ya kisasa na tayari Serikali imeshaingia mkataba na kampuni kutoka Uturuki kujenga Reli hiyo kipande cha Dar es salaam mpaka Morogoro. Lakini gharama ya kipande hicho ni USD 1.2bn. Kwahiyo Rais angeweza kutumia mapato haya ya mauzo ya Acacia kuongezea kwenye kipande hiki na hivyo kuepuka kukopa kuziba nakisi ya USD 800m iliyopo Sasa na Bunge kwenye Bajeti ya 2017/18 lingetenga fedha za kuanzia Morogoro kwenda Dodoma.
Kama Mipango ya Reli ipo sawa, Rais angeweza kutumia fedha za capital gains tax kutoka Acacia kujenga vyuo vya VETA kila Wilaya na kila Kambi ya JKT na chenji ingebaki. Tanzania inahitaji tshs 750 bilioni kujenga vyuo vya VETA kila Halmashauri ya Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji nchini.
Rais angejifunza kujizuia kutoa matamko barabarani angeisaidia Sana nchi na kujisaidia yeye mwenyewe kutimiza ndoto zake kwa nchi anayoongoza. Mimi binafsi naunga mkono kuwa ni lazima tuchenjue dhahabu hapa hapa nchini badala ya kupeleka mchanga Japan na China. Lakini ni muhimu maamuzi hayo yawe na ushahidi wa kisayansi badala ya matamko holela ambayo madhara yake Kwa nchi ni makubwa mno.
Zitto Kabwe, Mb
Arusha
26/3/2017
==== maelezo yangu kwa Mhariri RaiaMwema ====
Agizo la kutosafirisha Mchanga Liende Sambamba na Kujenga Uwezo Wetu Kama Taifa Katika Uchenjuaji (Refining)
[Maoni Yangu ya Hatua ya Serikali Kuzuia Kusafirishwa kwa Mchanga Kutoka Migodini]
"Kumekuwa na maneno kuwa hatuna uwezo wa kuchenjua hapa nchini, haya ni mawazo ya kilofa na kasumba ya hatuwezi. Unahitaji tani 150,000 za mchanga kwa mwaka kuweza kuwa na kinu cha kuchenjua chenye manufaa (economies of scale) lakini sisi tunazalisha tani 40,000 hivi.
Pia tunahitaji umeme zaidi ya megawati 1500 kwa mwaka ambazo kwa sasa hatuna. Tunachoweza kufanya ni kwanza kutazama fursa (potential) ya ukanda wetu ya kuzalisha huo mchanga (copper concentrates) ili kuingia mikataba na nchi jirani ziweze kuleta mchanga wao hapa na sisi tuwe kituo cha uchenjuaji kwenye region (ukanda huu). Pili tunahitaji uwekezaji mkubwa kwenye uzalishaji wa umeme ili kufikia mahitaji hayo.
Sasa mjadala hapa ni kwanini tunazuia kabla ya kujenga huo uwezo? Inawezekana zuio lilitolewa na Serikali litaweza kuanzisha mjadala wa majawabu hayo kwani ni mjadala wa miaka mingi Sana. Kuna nyakati vijana wa Kahama walikuwa wanayapiga mawe magari yaliyobeba mchanga kwa hasira. Sisi wanasiasa tulikuwa tunaibua jambo hili kila mwaka kupinga mchanga kusafirishwa.
Kwahiyo AMRI hii ya Serikali itusaidie kuuleta mezani mjadala huu kisha tukubaliane mkakati wa kuhakikisha jawabu la kudumu linapatikana.
Lakini pia wataalamu wanaweza kukaa na kubuni teknolojia yenye uwezo wa kufanya uchenjuaji kwa kiwango cha mchanga tunachozalisha nchini. Haiwezekani dunia nzima ikawa na teknolojia moja tu ya tani 150,000 la hasha.
Ushauri wangu ni kwamba Serikali ikae na sekta ya madini ili kupata jawabu la kudumu na kuweka commitment (dhamira ya utekelezaji) ya muda maalumu wa kuendelea kusafirisha mchanga na baada ya muda huo mchanga huo uchenjuliwe nchini kwetu na kuzalisha ajira na kuongeza uwezo wetu wa kuzalisha.
Hii sio Zero - Sum game (Kama sio kusafirisha basi hakuna lingine). Hapana. Mjadala unaweza kuleta jawabu lenye faida kwa nchi".
Gazeti la [HASHTAG]#RaiaMwema[/HASHTAG] waliniuliza maoni yangu kuhusu zuio la kupeleka nje mchanga kutoka kwenye migodi ya uchimbaji madini nchini. Maelezo haya sehemu ya majibu yangu kwao ambayo yamenukuliwa na toleo la gazeti hilo, toleo namba 500 la machi 8, 2017. Kuweka zuio la kusafirisha mchanga wa dhahabu ni uamuzi sahihi uliofanywa bila kuzingatia kwanza uwezo wa ndani wa kuchenjua (refinery).
Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Mbunge - Kigoma Mjini (ACT Wazalendo)
Kibingo, Mwandiga Township
Kigoma
Machi 8, 2017
=====
October 19, 2017