Mwananchi Huru
JF-Expert Member
- Nov 20, 2021
- 1,835
- 1,566
Katika ukurasa wake wa tweeter X Mkurugenzi Mtendaji wa PPP-Cetre Tanzania Bw. David Kafulila amesema, kauli ya Rais Samia kufungua nchi kwenye takwimu za kiuchumi inaongea kwa sauti ya juu zaidi hasa kwenye kipindi hiki kifupi cha miaka Mitatu.
Kafulila anasema, kabla ya Rais Samia kuingia madarakani mauzo ya ndani na nje yalikuwa na Jumla ya US$ 17.4bn sawa na karibu TZS 47,000,000,000,000 lakini miaka mitatu tu baadae mauzo hayo hayo yamefikia US$ 31.4bn karibu sawa na TZS 87,000,000,000,000 ambalo hii ni sawa na Ongezeko la 84%
Kafulila anaendele kusisitiza kuwa pamoja na kufanya biashara kubwa ya kuuza na kununua nje bado kukopa kwetu pia nje kumeongezeka kwa asilimia 33 tu yaani kutoka US$ 24.4bn mwaka 2021 hadi US$32.6bn mwaka 2024 jambo ambalo ni lakujipiga piga kifua.
Nawaza tu kwa sauti kama mambo yenyewe ni haya Kuna haja yoyote ya mtu kutoka ndani au nje ya CCM kupambana na mama 2025 kama kweli tutatanguliza mbele Uzalendo kwa Taifa letu?
Binafsi naamini itatuchukua miaka zaidi ya 100 kumpata Rais Samia mwingine.