Zitto amkabidhi Maalim Seif kadi namba 1, Babu Duni namba 10

ACT Wazalendo ijiandae na migogoro ya kutengenezwa.Sasa hivi nguvu ya kuifanya TZ iwe ya Vi-wonder imehamishiwa katika kuuwa upinzani.Lakini wanasahau kwamba kwa mazingira ya siasa za sasa jambo hilo haliwezekani.Maalim Seif kuhamia ACT Wazalendo na kutengeneza upya vyama viwili vya upinzani vyenye nguvu ni mfano mzuri kwa hao wanaojihangaisha na siasa za kijinga za maji taka.

Naam. Nadhani nguvu ya upinzani itaongezeka baada ya CUF kufa rasmi. Ile ngome ya cuf ya mikoa ya kusini, pwani na Tanga ambayo ACT ilishaanza kunyemelea sasa njia nyeupe.
 
MMtu mzima Seif Sharif Hamad anapokabidhiwa kadi ya chama na mtoto mdogo Zitto Kabwe .Aiseee Lipumba kiboko
Halafu imekuwaje anauvaa mkenge inamaana yaliyokuwa yanatokea 2015 na baada ya uchaguzi alikuwa hayaoni
 
Siasa za Africa hazitabiriki. Huyu kaenda ugenini mwingine karudi nyumbani. Kitu kimoja kiko wazi, huu ni mwisho wa enzi ya madai ya CUF kuporwa kura.
 
Hivi hawa ACT wanachama wao walikuwa hawana kadi? How possible wanaanza kutoa kadi namba moja leo!!!!

Kwani Kadi na Namba aliyokuwa nayo Kitila kapewa nani?

Inawezekana aliyekuwa na Kadi namba 1 amekufa au Alihama Chama ndiyomana Kapewa Maalif Seif Sharif Hamad
 


Dar es Salaam. Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amewakabidhi kadi za uanachama wa chama hicho waliokuwa vigogo wa Chama cha Wananchi (CUF) huku Maalim Seif Sharif Hamad akipewa kadi namba moja na Juma Haji Duni akikabidhiwa kadi namba 10.

Shughuli ya kukabidhi kadi hizo inaendelea kufanyika leo Machi 19, 2019, makao makuu ya ACT- Wazalendo yaliyopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

Viongozi wengine ambao wamekabidhiwa kazi ni Ismail Jussa, Mbalala Maharangande na Sheweji Mketo,

Katika makabidhiano hayo, Zitto amesema hiyo namba kumi ambayo amekabidhiwa Duni ni kama mchezaji wa timu ya Liverpool.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa kadi, Maalim Seif amesema yeye ni mara ya kwanza kukanyaga ofisi za ACT- Wazalendo lakini anajiona ni mwenyeji.

“Nawashukuru sana kwa kukubali ombi letu kwamba tuje tuchangie nguvu katika chama cha ACT- Wazalendo na ninyi hamkuwa na ajizi mkatuambia njooni na haukuwa uamuzi wa viongozi pekee bali wa wanachama,” amesema Maalim Seif


Kama Maalim Seif Shariff Hamad kapewa Kadi Namba Moja ( 1 ) ina maana inawezekana Kadi ya Mwenye Chama chake ACT Zitto Kabwe ni namba Sifuri ( 0 ) au?
 
Kama Maalim Seif Shariff Hamad kapewa Kadi Namba Moja ( 1 ) ina maana inawezekana Kadi ya Mwenye Chama chake ACT Zitto Kabwe ni namba Sifuri ( 0 ) au?

Namba 1 ilikuwa ya Kitila lakini alihama na Namba 1 ikawa wazi ambayo Leo amekabidhiwa Maalim Seif.
Zito Yake ni above 10.

Namba ya Kadi ni sawa na Namba ya Jezi.
Kwa mfano Jezi Namba 10 ya Ronaldinho alipohama kapewa Messi.
 
Namba 1 ilikuwa ya Kitila lakini alihama na Namba 1 ikawa wazi ambayo Leo amekabidhiwa Maalim Seif.
Zito Yake ni above 10.

Namba ya Kadi ni sawa na Namba ya Jezi.
Kwa mfano Jezi Namba 10 ya Ronaldinho alipohama kapewa Messi.
Mwanzoni ilikuwa inamilikiwa na Albert Gasper Msando ambae alihamia Chama Cha Mapinduzi hivyo ilikuwa wazi "- Zitto Kabwe, akiwa Kipindi cha Jahazi cha Clouds FM
 
kadi namba 1 huwa wanapewa waanzilishi wa Chama, ACT wazalendo wanataka kutuambia kadi namba 1 haikuwa na mwenye nayo, hapa wanatupa sababu ya kuamini Seif sharrif Hamad katoa mzigo mzito wa kukinunua hiki chama. Ujinga kama huu huwezi kuukuta katika Chama Cha Mapinduzi
Kwenye chama cha mapinduzi kuna maujinğa mengi zaiđi ya ilo
 
Mtu mzima lowasa anapokabidhiwa kadi ya chama na kijana mtoto mdogo polepole, aisee Tundu Lissu ni kiboko
si aheri angekabidhiwa na polepole, kadi alipewa na katibu wa tawi kule monduli, tena kadi namba 6789864
n by the way yupo on probation.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom