WAKATI Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kikimwandikia Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe barua ya kumtaka ajieleze dhidi ya tuhuma zinazomkabili, yeye ameamua kukimbilia polisi akimshitaki mmoja wa viongozi wenzake.
Habari za kuaminika zimedai kuwa Zitto ambaye hivi karibuni alivuliwa cheo chake cha unaibu katibu mkuu wa CHADEMA, inadaiwa amefungua mashitaka polisi akimtuhumu Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Dar es Salaam, Henry Kileo kwa madai ya kusambaza waraka katika mitandao ya kijamii.
Akithibitisha tukio hilo, wakili wa Kileo, Peter Kibatara, alisema kuwa mteja wake amemriwa kufika makao makuu ya Jeshi la Polisi leo Jumatano saa nane mchana na kuonana na mmoja wa maofisa wa juu wa jeshi hilo, aliyetajwa kwa jina moja tu la Mbutta, kufuatia mashitaka yaliyofunguliwa na Zitto dhidi yake.
Akizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wetu, Kileo alikiri kuitwa polisi, ingawa alidai hajui ni waraka gani anaotuhumiwa kuusambaza unaomchafua Zitto.
"Kwa kweli sijui hata mimi ni waraka gani, ingawa hivi karibuni kulikuwa na waraka wa siri uliodaiwa kutoka CHADEMA, na ambao ulijaa tuhuma za usaliti. Lakini huo tuliishaukana siku nyingi. Labda kuna mwingine," alisema Kileo.
Zitto kutwa nzima ya jana hakuweza kupatikana kwa njia ya simu kufafanua mashitaka aliyofungua polisi. Simu zake zote za kiganjani zilikuwa zimezimwa.
-Tanzania daima.
ZZK anataka kuondoka CHADEMA na mtu wa kumsindikiza.......
Mfa maji haachi kutapatapa. So my comrade Kilewo vuta subira na hakika kesi hii utashinda na hatimaye litakuwa pigo lingine tena kwa Zitto na hatimaye tutamsahau kabisa kisiasa. Walikutengenezea ya UGAIDI sembuse hii. Shame on them.
Kitufe kimekodiswa kule Lumumba, kwa sasa wanakitumia kugongeana like huko ofisi kwao,Mods rudisheni kitufe cha "LIKE" tunasumbuka wadau wenu......
Mimi hapa ndio napozidi kumuona Zitto ndumi la kuwili,kwa sababu kwenye press conference hakukanusha wala kufafanua waraka huu wa yeye kuhongwa pesa na pia kushirikiana na TISS na hata hajazungumzia uhusiano wake na Jack Zoka na Ighondu na mnyumbuliko wa pesa hizo kutoka NMB kwenda Ujerumani kwa Andrea na pia kuwatumia wakina Kitila,Mwampamba,Mchange,Ben Saanane,Juliana Shonza etc.
Baadala yake kakimbilia Polisi na kufungua defamation case ili suala hili liishe kimya kimya na kuepusha kwa Zitto kufafanua bali Kileo na obviously Polisi inajulikana kwenye siasa inavyotumika!!
Ben Saanane upo kwenye waraka ule kuwa ulitumiwa pesa na Zitto,please tueleze ulipewa kwa minajili gani??!!
Hizi sasa sarakasi. Hivi yule aliyeuweka waraka ule kwenye blog yake siye huyu? Mbona mnacheza na akili za wananchi!WAKATI Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kikimwandikia Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe barua ya kumtaka ajieleze dhidi ya tuhuma zinazomkabili, yeye ameamua kukimbilia polisi akimshitaki mmoja wa viongozi wenzake.
Habari za kuaminika zimedai kuwa Zitto ambaye hivi karibuni alivuliwa cheo chake cha unaibu katibu mkuu wa CHADEMA, inadaiwa amefungua mashitaka polisi akimtuhumu Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Dar es Salaam, Henry Kileo kwa madai ya kusambaza waraka katika mitandao ya kijamii.
Akithibitisha tukio hilo, wakili wa Kileo, Peter Kibatara, alisema kuwa mteja wake amemriwa kufika makao makuu ya Jeshi la Polisi leo Jumatano saa nane mchana na kuonana na mmoja wa maofisa wa juu wa jeshi hilo, aliyetajwa kwa jina moja tu la Mbutta, kufuatia mashitaka yaliyofunguliwa na Zitto dhidi yake.
Akizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wetu, Kileo alikiri kuitwa polisi, ingawa alidai hajui ni waraka gani anaotuhumiwa kuusambaza unaomchafua Zitto.
"Kwa kweli sijui hata mimi ni waraka gani, ingawa hivi karibuni kulikuwa na waraka wa siri uliodaiwa kutoka CHADEMA, na ambao ulijaa tuhuma za usaliti. Lakini huo tuliishaukana siku nyingi. Labda kuna mwingine," alisema Kileo.
Zitto kutwa nzima ya jana hakuweza kupatikana kwa njia ya simu kufafanua mashitaka aliyofungua polisi. Simu zake zote za kiganjani zilikuwa zimezimwa.
-Tanzania daima.
Chadema punguzeni hizo siku badala ya 14 ziwe saba atimuliwe huyu msaliti