Zitto afichua siri yake na Kikwete...

Zitto afichua siri yake na Kikwete...

Ili kuthibitisha uzalendo wako ZZK ni vema uachie Ubunge kwa kipindi kimoja ili ukaimarishe chama na kujenga safu ya ushindi kwa CDM kwa ajili ya nafasi ya Urais.
 
Umenena mkuu, ila mwananchi lina siri nzito na Zitto!

Tuanchane na hilo!

Hongera jf,

Binafsi kutoka moyoni ZITTO ni mnafiki na muuongo mkubwa!

Amejaribu kutumia jf na kulaghai watu nashanga kweli watu wanaojiita GT wamelaghaika na wanamshangilia!

Kweli kabisa mkuu,ni lazima tuwe makini na huyu kamanda wetu zitto ni mjanja sana hakawii kutuingiza mkenge.Siku za nyuma zitto aliaminika sana..lakini kwa sasa kutokana matamshi yake mbalimbali yasiyoeleweka amewapa wananchi maswali yasiyo na majibu.
 
JF, the home of GREAT NEWS!! Habari nyingii za TV na magazeti tunazipata kwanza hapa ndipo tunazisikia jioni!!! Na nyingine nyingi hukud wanashindwa kuzichukua maana ni nyingi mno. JF JF JF JF!!! Tunagawana masaa!!! Zito ana lake jambo!! Si nasiki anataka anataka anataka ile ...... Ha ha ha!!Tusubiri mwisho wa siku ukweli zaidi utatimia i,e maandiko yatatimia kati ya Mfalme na Zito, na Zito na familia ya mfamle kwa ujumla na Zito na SSM!!
 
Big up jf, mmefanya kazi nzuri sana ya mahojiano na zitto na karibu maswali yote muhimu tuliyochangia kuuliza yameulizwa.

Ngoja nimalizie kusoma mahojiano yote halafu nitarudi. Wakati naendelea kusoma pia natafakari kauli hii ya zitto;



“Sioni NCCR ikidumu. Sioni future (tumaini) ya UDP bila Cheyo na TLP bila Mrema,” alisema.

Hata hivyo, alisema kuna uwezekano CCM kumeguka na kundi kubwa litakalotokana na tukio hilo likaunda chama kingine cha siasa ambacho kinaweza kuwa na nguvu zaidi hata ya Chadema"

CCM imeguke kipande kiwe na nguvu zaidi hata ya CHADEMA!
 
MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amefichua siri ya uhusiano wake na Rais Jakaya Kikwete kuwa, unatokana na kuheshimu mchango wake anaoutoa kwa taifa.

Kutokana heshima hiyo, Zitto anasema ndiyo maana Rais Kikwete hakufika jimboni kwake katika uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2005 na mwaka 2010 kumnadi mgombe wa CCM.



Zitto ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema alisema hayo katika mahojiano maalum na Mtandao wa Jamii Forum juzi.
Aidha, Zitto alisema anamheshimu Rais Kikwete kama mzee wake na kwamba, kuwaita kuwa wao ni marafiki ni kukosea.

“Kuita sisi ni marafiki ‘is understatement’, yeye ni mzee wangu. Tunaheshimiana, lakini ninaiheshimu zaidi Tanzania na ninaipenda zaidi Tanzania,” Zitto alisema.

Alichokifanya Rais Kikwete kutokuja katika jumbo langu si jambo geni, kwani hata vyama vingine vimewahi kuvifanya.
(vijana wengi wanaochipukia kwenye siasa hufanya siasa ni ugomvi usikwisha,kukoseana heshima,kutukanana,igeni mfano kidogo,kwa zitto kabwe tumthamini anaelijali taifa letu!!
shukrani za dhati kwa mh:jk ipo siku wa tz watakulilia!!!
 
This is Holy ****....
Mleta Bandiko kwa nini un aduplicate ile thread ambayo Zitto alikuwa anajibu straight.
Hata mumpake mafuta kiasi gani, Mimi Kwangu Zitto ni Mnafik
 
Last edited by a moderator:
kijana endelea kukaza buti nafikiri tutafika pazuri tuko nyuma yako
tukijitahidi kuangalia jinsi ya michakato mizima,inavyoweza kuleta mabadiliko katka taifa letu
 
Umenena mkuu, ila mwananchi lina siri nzito na Zitto!

Tuanchane na hilo!

Hongera jf,

Binafsi kutoka moyoni ZITTO ni mnafiki na muuongo mkubwa!

Amejaribu kutumia jf na kulaghai watu nashanga kweli watu wanaojiita GT wamelaghaika na wanamshangilia!
Urais si Urahisi, Zitto bado hatoshi kuwania Urais 2015, Watanzania hatuko tayari tena kuigeuza taasisi ya Urais kama chombo cha majaribio, Zitto anajiandaa kwenda kumalizia PHD yake ndio sababu kuu ya kutangaza kutogombea Ubunge 2015. Tuache kudanganyana.
 
I loveed this part!, this shows what I call "political maturity" for both of them and even more the part that, the Prez didnt camp in Kigoma Kask. When you do your work well you dont need no single soul to prove it for you, you build the wall of respect and dignity around yourself, you SHINE on your own and keep all the negativity away from you but unfortunately most of our viongozi cant differentiate between HAVING THE JOB and actually DOING THE JOB THEY HAVE, its like they're travelling to get to a certain point and somewhere along that someone give them a golden key, but instead of using the key to move forward wanakaa chini, wanakenua meno na kuanza kuushangaa huo ufunguo mxx! ovyoo. Thanks JF for this interview you have shed some light and now at least we know a bit more about him. Keep it up mheshimwa ZK!

KABWE 2015!
 
zitto_jk.jpg


Rais Kikwete na Zitto Kabwe

NDIYO ILIYOMFANYA ASIFIKE JIMBONI KWAKE KUMNADI MGOMBEA CCM

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amefichua siri ya uhusiano wake na Rais Jakaya Kikwete kuwa, unatokana na kuheshimu mchango wake anaoutoa kwa taifa.

Kutokana heshima hiyo, Zitto anasema ndiyo maana Rais Kikwete hakufika jimboni kwake katika uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2005 na mwaka 2010 kumnadi mgombe wa CCM.

Zitto ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema alisema hayo katika mahojiano maalum na Mtandao wa Jamii Forum juzi.

Mbunge huyo ambaye pia ni Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, jana alilithibitishia gazeti hili kwamba alihojiwa na mtandao huo kwa saa nane.

“Kweli ni mahojiano baina yangu na Jamii Forum. Kwa Kfupi ni kwamba, yalikuwa mahojiano ya saa nane, kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa kumi jioni na walionihoji kwa njia ya mtandao walikuwa wakituma maswali na mimi nawajibu,” alisema Zitto.

Alisema yeye na Rais Kikwete wana uhusiano nje ya siasa na hata siku moja hawajadili mambo ya vyama vyao wanapokutana na kwamba, Rais anaamini katika uzalendo wake.

Zitto alisema kutokana Rais Kikwete kuthamini mchango wake, ndiyo maana hajawahi kwenda kwenye jimbo lake kumfanyia kampeni mgombea wa chama chake cha CCM katika chaguzi za mwaka 2005 na 2010.

“Hatuna makubaliano yeyote, bali anaheshimu mchango wangu kwenye nchi yangu. Mwaka 2005 hakuja Kigoma Kaskazini na 2010 pia hakuja Kigoma Kaskazini,” alisema.

Alisema kama ilivyo kwa wengine wenye uamuzi ya kuthamini kazi za wagombea wa vyama vingine, Rais Kikwete naye anayo haki ya kuheshimu na kuthamini kazi zake.

Aithdha, Zitto alisema anamheshimu Rais Kikwete kama mzee wake na kwamba, kuwaita kuwa wao ni marafiki ni kukosea.

“Kuita sisi ni marafiki ‘is understatement’, yeye ni mzee wangu. Tunaheshimiana, lakini ninaiheshimu zaidi Tanzania na ninaipenda zaidi Tanzania,” Zitto alisema.

Alichokifanya Rais Kikwete kutokuja katika jumbo langu si jambo geni, kwani hata vyama vingine vimewahi kuvifanya.

Alitoa mfano wa aliyekuwa mgombea wa urais kupitia Chadema katika uchaguzi mkuu mwaka 2005, Freeman Mbowe alipofika katika Jimbo la Musoma Mjini, alimpigia kampeni mgombea wa CUF.
Zitto afichua siri yake na JK - Siasa - mwananchi.co.tz




 
Naitoa shilingi .. Sijui Kama ntairudisha tena..
 
Back
Top Bottom