Zitambue Sifa za Kiongozi bora

Zitambue Sifa za Kiongozi bora

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Joined
Aug 7, 2018
Posts
693
Reaction score
1,162
20210129_104008_0000.png


Viongozi huunda mataifa yetu, jamii, na mashirika. Tunahitaji viongozi bora watusaidie kutuongoza na kufanya maamuzi muhimu makubwa ambayo yanafanya ulimwengu kusonga mbele.

Kiongozi bora ana sifa zifuatazo:-

Maono

Kiongozi ni lazima awe na maono ambayo ni tofauti wengine. Lazima awe na uwezo wa kuona vitu ambavyo watu wengine hawana uwezo wa kuviona.

Uwajibikaji

Kiongozi bora lazima aweze kuwajibika. Kuwajibika katika kutenda kazi na kusaidia watu. Pia kuwa tayari kung’atuka pale itakapoonekana kuwa ameshindwa kutekeleza matakwa ya watu wake.

Uwezo wa kukabidhi madaraka

Kiongozi bora hafanyi majukumu yote peke yake huwapa nafasi watu wengine kufanya kazi.

Kujiamini

Kujiamini ni sifa kubwa katika kufanya mambo mengi. Ili uweze kujiamini ni lazima pia uwe na mtazamo chanya. Bila kujiamini na kuwa na mtazamo chanya na wenye kujenga sahau kuwa kiongozi mkubwa na bora.

Kuwa na uwezo wa kubadili mwelekeo

Kuna wakati kiongozi hulazimika kubadili mwelekeo wa nguvu zake ama sera zake. Kama kiongozi bora kuwa na uwezo huo kutakusaidia sana katika kufanya maamuzi. Ni wakati gani wa kutumia nguvu kubwa, wakati gani utumie nguvu ndogo.

Ushawishi

Kwa watu wengine, "ushawishi" huhisi kama neno chafu. Lakini kuweza kuwashawishi watu kupitia ushiriki ni sehemu ya kuwa kiongozi mwenye msukumo na mzuri. Ushawishi ni tofauti kabisa na ujanja ujanja.

Ujasiri

Badala ya kuzuia shida au kuruhusu mizozo kuongezeka, ujasiri huwawezesha viongozi kupiga hatua na kusongesha mambo katika mwelekeo sahihi.

Heshima

Kuwatendea watu kwa heshima kila siku ni moja ya mambo muhimu sana ambayo kiongozi anaweza kufanya. Itapunguza mvutano na mizozo, itaunda uaminifu, na kuboresha ufanisi.
 
Duh, mbona hata sifa moja hana sasa !!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom