Zipi kazi na Yapi ni Majukumu ya Mwanamke au Mwanaume? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zipi kazi na Yapi ni Majukumu ya Mwanamke au Mwanaume?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Kigarama, Oct 31, 2012.

 1. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #1
  Oct 31, 2012
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kwa mila na desturi za duniani kuna mgawanyo wa Kazi na Majukumu ya wanawake au wanaume. Lakini kutokana na kubadilika kwa mitizamo ya wanadamu baadhi ya vitu vinatakwa kufanywa na jinsi zote. Kwenye Orodha ifuatayo nimeweka kazi na majukumu ya wanawake na wanaume kama kuna jambo hukulibalini nalo jenga hoja.


  1. Kubadilisha nepi za mtoto na kumuogesha (Mwanamke)
  2. Kuosha vyombo, kupika,kutoa vyombo mezani (Mwanamke)
  3. Kutandika kitanda na usafi wa chumba (Mwanamke)
  4. KUfua nguo za mwenza na kuzipanga Kabatini (mwanamke)
  5. Kusimamia nidhamu ya watoto nyumbani (Mwanaume)
  6. KUtunza Bustani na Mazingira ya nyumba (Mwanaume)
  7. Kulima shambani (Mwanamke na mwanaume)
  8. Kulipa ada ya shule (Mwanaume)
  9. Kutoa hela za matumizi nyumbani (Mwanaume)
  10. Gharama za matumizi ya Gari (Mwanaume)
  11. Kulipa bili ya chakula Hotelini au pombe Baa (Mwanaume)
  12. Ulinzi wa nyumba (Mwanaume

  Kama unaona kuna kazi au majukumu ya Mwanamke au mwanaume ambayo sijaorodhesha yaweke na kama yapo niliyoyaorodhesha lakini nimekosea kuweka Mhusika wake yakosoe!!
   
 2. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #2
  Oct 31, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  saluni....mwanamke
  kuosha miguu....mwanamke
  kununua nguo mpya kila weekend na hereni na chupi.....mwanamke
  kutunza wazazi pande zote na ndugu wengine ...mwanaume
  michango ya harusi....mwanaume
  endelea@Lara1
   
 3. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #3
  Oct 31, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,657
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Bado unapewa vitu?
   
 4. C

  CAY JF-Expert Member

  #4
  Oct 31, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 501
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Namba 7 hapana.Hiyo ni kazi ya mwanaume.Ni katika kuhakikisha nyumba yake ina chakula cha kutosha.Pia umesahau kutafuta house girl/boy-Mwanamke
   
 5. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #5
  Oct 31, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  hiyo ya kufua siiwezi hata kidogo na sina nia ya kuja kuiweza........

  Mtu akavae ma-jeans huko nikamfulie mie, kisa?
   
 6. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #6
  Oct 31, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  bado napokea .unataka kunipa?
   
 7. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #7
  Oct 31, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  hapo kwenye red ni jukumu la wote ,ile kauli ya wamama wengine wanasema subiri baba yako aje !!!mbaya nidhamu na usafi ni kwa watu wote
   
 8. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #8
  Oct 31, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  kuna mashine siku hizi,but mi napenda kufua sana sana ,nitakusaidia
   
 9. HoneyBee

  HoneyBee JF-Expert Member

  #9
  Oct 31, 2012
  Joined: Oct 23, 2012
  Messages: 673
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 60
  Ukizingtia kuwa wanawake siku hizi wanafanya kazi nje ya nyumba ni vigumu kusimamia kazi za nyumbani bila Msaada toka kwa mfanyakazi, ndugu, au Kama wana bahati, waume zao. Kama mama mwenye nyumba anasaidia kuleta kipato nyumbani sioni tatizo baba akisaidia kubadilisha nepi mtoto huku mama akiandaa chakula. marriage is team work after all. Binafsi Mimi na mume wangu tunasaidiana kazi zote, ila mara nyingi ni Mimi ninaefanyaga kazi za "kike" kwasababu naziweza zaidi na si kwasababu amekataa kwakuwa yeye ni mwanamme. I cook, clean, work and take care of the baby. Every now and then he takes care of the baby so I can do my own thing as well. Ushauri kwa akina baba, jaribuni kujenga uhusiano na watoto wenu. Kulipia gharama za nyumbani pekee haitoshi. hakuna kitu kizuri kama uhusiano mzuri Kati ya wazazi na watoto.
  Great topic Kigarama!   
 10. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #10
  Oct 31, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Kwa mashine sawa, ila kwa mkono hapana hata kidogo.

  Unaonaje akifua mwenyewe mpaka apate watoto wakiume waje wamsaidie?
   
 11. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #11
  Oct 31, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  [​IMG]
  hii picha inakuhusu sana wewe mtoto wa kike tena mtanzania msafi mumeo bibi mfulie wewe ngoja wengine wamfulie ukome kabisa au peleka mwenyewe dry cleaner wacha ushamba.
   
 12. Ralphryder

  Ralphryder JF-Expert Member

  #12
  Oct 31, 2012
  Joined: Nov 16, 2011
  Messages: 4,588
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Soma Biblia takatifu, Waefeso 5:22-31.
   
 13. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #13
  Oct 31, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  unajua kuwakosha wanaume wa humu basi wanakasirikajeeeeeeeeeeeeeeee kwiwkiwkiwkiwkwiwki
   
 14. Nicole

  Nicole JF-Expert Member

  #14
  Oct 31, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 4,284
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  hapo chacha, za kwangu mwenyewe sifui.....
   
 15. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #15
  Oct 31, 2012
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  I think am 'addicted' to that...in red! Kwa hiyo inabidi iwe....mwanamke na mwanaume
   
 16. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #16
  Oct 31, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,657
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Ndiyo nataka
   
 17. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #17
  Oct 31, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Kwanza naona upo katika wale watu wanaoishia kwenye ku-assume vitu na kuviamini wao wenyewe.

  Nani aliyekwambia mie ni Mtanzania safi?

  Pili kutomfulia mume ni ushamba kwa mujibu wa mamlaka gani?

  Msitake watu wote waishi kwa misingi mliojipangia nyie. Watu wanatofautiana, na kimsingi wanayoweza kufanya kwa wenza wao yanatofautiana vile vile.
   
 18. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #18
  Oct 31, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  na hiyo misingi ndio itakumaliza end of the day kip it up,ukukua utajua ninachokisema hapa .uwe mtz usiwe hainihusu mradi unaelewa kiswahili hiki tunachotumia hapa
   
 19. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #19
  Oct 31, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  nipe basi
   
 20. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #20
  Oct 31, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Watu wanasema hawawezi kumalizwa kwa kufua ma-jeans ya wanaume, wewe unasema mtu atamalizwa kwa kutokufua. Atamalizwa vipi?

  Au ndizo zile fikra za kimfumo dume kuwa kama hujamtumikia mume kama wewe punda wake kirongwe basi atakutafutia nyumba ndogo?

  Pole sana, manake huko ni kushikiwa akili na mfumo-dume
   
Loading...