Zingatia: Simu na mwanadamu, zaidi watoto

Zingatia: Simu na mwanadamu, zaidi watoto

clion dismas

Senior Member
Joined
Aug 6, 2017
Posts
185
Reaction score
169
SIMU: ONGEZA UMAKINI

Habari ndugu zangu, poleni na shughuli za ujenzi wa taifa. Tumshukuru MUNGU kutupa fursa ya kuiona leo, kutuepusha na ajali lakini pia kuturuhusu tupitie jambo fulani gumu ili kupitia jambo ilo, ukuu wake udhihirike kwa watu wote.

Naomba niongelee SIMU , kifaa cha mawasiliano ya haraka. Mwisho wa somo hili nitataka ufahamu mambo yafuatayo:-

· Simu ni nini

· Madhara yake katika jamii

· Matumizi sahihi kwa afya yako na jamii


SIMU NI NINI?

Kwa ufupi kabisa, ni kifaa cha mawasiliano ya haraka zaidi kwa njia ya mionzi ya umeme.Kwa mara ya kwanza kabisa ilitumika kurahisisha shughuli za kivita, Simu yoyote ile ina antena moja ya njia 2(dipole) inayomuwezesha mtu anayewasiliana kutuma na kupokea taarifa(signal) kwa wakati mmoja.

Simu ni kama KIFAA CHA MICROWAVE, ndiyo, ile unayookea na kupashia vyakula majumbani na mahotelini. Utofauti wa kifaa hiki cha kupashia vyakula na simu ni umeme au kiasi cha nguvu ya umeme kinachotumiwa na kila kimoja. Simu inatumia nguvu kidogo, ikikadiriwa WATI 1, microwave, WATI 1000. Inakadiriwa Zaidi ya watu bilioni 6 ulimwenguni kote wanamiliki kifaa hiki na kadhalika watu Zaidi ya bilioni 7 ulimwenguni kote wanakitumia kwa njia ya mawasiliano. KWA UFUPI, WAKAAZI KARIBU WOTE SAYARI YA TATU( 89%) WANATUMIA SIMU.



MADHARA YAKE KATIKA JAMII




Ifahamike wazi kabisa, hakuna kifaa hata kimoja kisicho na madhara.

Madhara ya simu yamejengeka katika mfumo mzima wa taarifa/signal za simu ambazo haziko katika mpangilio pamoja na uwezo wa kuharibu au kuingilia jozi za vinasaba( DNA). Na madhara yake hayako katika nguvu au power ambayo signal ya simu imebeba, yaani ile wati moja.

Ifahamike vizuri, kila kifaa cha kielektroniki kinatoa mionzi na hii mionzi ni hatari kwa mwanadamu.zitakuja kuongelewa nadharia nyingi juu ya SAR na nyingine ila, umewahi ongea na simu kwa muda mrefu? Uwa wajisikieje kichwa chako? Au umewahi kaa eneo la karibu na mnara wa simu kwa muda? Uwa wajisikieje? Au kulala chumba ambacho vifaa vya umeme vimewaka usiku kucha,? Uwa wajisikieje?

Kuna aina nyingi za uchafuzi wa mazingira,( katika hewa, maji, ardhi na kelele) lakini inayoongoza ulimwenguni ni ELECTRICAL POLLUTION( uchafuzi wa mazingira kwa sababu ya mionzi itolewayo na umeme pamoja na vifaa vya umeme). Laiti umeme na mionzi ingekua inaonekana kwa macho, usingeweza kuona hata kidole cha mguu wako, kwa maana kila kona mionzi imetapakaa kwa uwingi sana, sanasana maeneo ya mijini au yaliyoendelea sana kiteknolojia. kwa mtu yeyote mfanyabiashara hana budi kumfahamisha mteja wa bidhaa yake faida zake pamoja na hasara zake zote kabla biashara haijafanyika. Kwa lugha nyingine, mtu anunue kitu akifahamu kiundani kabisa namna gani yuko salama au katika hatari na kitu kile.

Nitatembea na wazo la kwamba kila mtu anayemiliki simu anafahamu vizuri kabisa faida zake pamoja na hasara zake na ameamua kununua iyo simu akifahamu yote.( taaluma zetu zinafundisha hivyo).


1. USABABISHA SARATANI.


Saratani ni makuzi ya seli mpya bila ya sababu malum ambazo uleta madhara katika mwili wa binadamu. Kisababishi chochote cha saratani ufahamika kama KASINOJENI, simu ni kasinojeni na imewekwa katika daraja la 2B, May 31, 2011, World Health Organization (WHO)/International Agency for Research on Cancer (IARC), “Dr Jonathan Samet (University of Southern California, USA), overall Chairman of the Working Group, indicated that “the evidence, while still accumulating, is strong enough to support a conclusion and the 2B classification. The conclusion means that there could be some risk, and therefore we need to keep a close watch for a link between cell phones and cancer risk.”

“Given the potential consequences for public health of this classification and findings,” said IARC Director Christopher Wild, “it is important that additional research be conducted into the long‐term, heavy use of mobile phones. Pending the availability of such information, it is important to take pragmatic measures to reduce exposure such as hands‐free devices or texting.”

Pia Katika habari ya ENVIRONMENTAL HEALTH TRUST’S LETTER, iliongelea binti mmoja (marehemu sasa), miaka 21 kwa umri, aliyekuwa na tabia ya kuweka simu yake ndani ya sindiria siku huku sindiria akiwa ameivaa. Alikutwa na uvimbe katika matiti yote mawili. Wataalamu wa saratani, Robert Nagourney na John West walisema kulikuwa na uwezekano wa sababu nyingine ambayo ingeweza kusababisha ile saratani yake ya matiti tofauti na simu. Lakini ushahidi ulikuwa wazi, kwa maana, hata seli za saratani zilichukua umbo la simu ambayo ilikua ikivaliwa kwenye sindiria.


Kadhalika na mwanariadha mmoja, umri wa miaka 34 alikutwa na uvimbe wa saratani katika titi lake, yeye aliweka simu kwenye sindiria masa 4 kila siku kwa miaka 10.




Pia jopo la watafiti nchini ISRAEL walibaini ongezeko la saratani ya tezi parotid, kuna tezi inaitwa parotid, aina ya tezi mate( salivary gland) iliyoko karibu na sikio, pale ambapo hua unashikilia simu yako wakati unaongea nayo. Tafiti ilionyesha, mwaka 1970-2006 kulikuwa na ongezeko la juu sana la saratani ya tezi parotid wakati tezi mate nyingine hazikuwa na tatizo hilo.



Mwaka 2008 Dr. Siegal Sadetzki, aliyekuwa mkuu wa timu ya utafiti huu aliieleza seneti ya marekani juu ya tatizo hili. (U.S. Senate Hearing).

Wakati akiishuhudia seneti alisema yafuatayo kwa ufupi:-

· Mtu yuko katika hatari ya kupatwa ugonjwa huu kwa asilimia 34 kama ni mtumiaji wa simu kila siku na kwa walau miaka 5.

· Mtu yuko katika hatari ya kupatwa ugonjwa huu kwa asilimia 58 kama umewahi ongea na simu kwa masaa 5500 katika maisha yako yote.

· Mtu yuko katika hatari ya kupatwa ugonjwa huu kwa asilimia 49 kama ameweza kuongea kwa masaa 266 na dakika 18.

Saratani hizi zote zinawaathiri sana watoto, kwa sababu, seli zao zinakua kwa haraka sana, ngozi yao laini kadhalika fuvu lao mionzi kupita na kuingia katika ubongo wa kati ni kwa uwepesi sana. Kwanini uangamize maisha ya mwanao? Kijana wako? Au mtoto wa jirani yako?

clip_image016.png


Tafiti zinaonyesha watoto wadogo wanawepesi wa kupata saratani ya ubongo ukilinganisha na watu wazima. brain cancer



clip_image018.jpg


UMEWAHI JIULIZA KWANINI “STEVE JOB”, HAKURUHUSU WATOTO WAKE KUTUMIA IPAD WAKATI YEYE NDIYE MWANZILISHI WAKE? KAMA ULIKUA HUJUI, ELEWA LEO, HUYU MTU KATIKA UTOTOT, WATOTO WAKE HAWAKUTUMIA KIFAA HIKI, MPAKA WALIPOKUA WATU WAZIMA.

clip_image020.jpg


NCHI ZILIZOENDELEA NYINGI ZIMEWEKA SHERIA KALI KUWALINDA WATOTO NA MATUMIZI YA SIMU.

clip_image022.jpg




Mwananchi, ndugu yangu mpendwa, hapo sijagusia saratani ya ubongo. matumizi ya simu hayazuiliki lakini, zingatia MUDA WOTE SIMU YAKO IWEKE UMBALI WA INCHI 6-8, YAANI SENTIMENTA 12-16 KWA USALAMA WAKO. SIMU NI MBAYA, TAFITI ZINASEMA, USITEGEMEE KWAMBA ANAEUZA SIMU AU KAMPUNI YA SIMU ITAKUBALIANA NA UKWELI HUU, WALE POLISI?. USIBEBE SIMU MWILINI MWAKO, SEHEMU YOYOTE ILE.

2. SHIDA YA KUMBUKUMBU NA UGUMU KATIKA KUJIFUNZA TABIA MPYA KWA WATOTO WALIOZALIWA

Tafiti zimeonyesha kwamba watoto watumiao simu wanaathiriwa ubongo kama hapo juu tulivyo ona. Lakini kama mojawapo ya gonjwa la akili, kusahau imekuwa shida kubwa kwa wale watoto ambao, wazazi wao kipindi cha mimba waliruhusu sana simu zikawa karibu na maeneo ya matumbo yao yaliyobeba viumbe hawa.

Tafiti iliyofanyika mwaka 2008, karibu watoto waliozaliwa 13,000 ambao eidha wazazi walitumia simu wakiwa wajawazito au wariruhusu watoto watumie simu utotoni walikutwa na ugumu wa kujifunza tabia, ikiwemo kusahau.

clip_image024.jpg


clip_image026.jpg


clip_image028.jpg


Baada ya kuona shida ya namna hii, baadhi ya mataifa walianzisha kampeni ya kumlinda mtoto na mionzi ya simu.
clip_image030.jpg


3. KUUA SELI ZA UZAZI, KUKOSA RUTUBA PAMOJA NA MAUMIVU YA MIFUPA KATIKA MAENEO YA KIUNO( PELVIS) ,SIMU INAKOWEKWA.

Kulingana na uhusiano uliopo kati ya mionzi ya simu na vinasaba, umonesha seli zikiwemo na za uzazi huaribika. Ukirejea tafiti iliyofanywa na Dr. Martin Blank katika hotuba yake, November 18, 2010 Commonwealth Club of California program, “The Health Effects of Electromagnetic Fields,” kasema vizuri, kwanini mionzi ya kila aina ni mibaya kwa vinasaba vyako. Pia ukisoma International Journal of Radiation Biology, April 2011, utaona Dhahiri kwamba DNA ina umbo kama lenye sifa za antena ambazo kwa wepesi Zaidi zinaweza kuathiriwa na mionzi.

clip_image032.jpg


clip_image034.jpg


clip_image036.jpg



clip_image038.jpg


clip_image040.jpg



Pia tafiti iliyochapishwa mwaka 2009, imeonyesha kuweka simu kiunoni ufanya pelvis( kwa wepesi ni ina ya mfupa ulio katika umbo la U unaotoa msaada au unaolinda kibofu cha mkojo, rectum na genital rgans) kuwa dhaifu sana. Kwa kutumia X-ray density ya mfupa upande wa kiuno ambako simu imekua ikiwekwa, wanaume 150 ambao kwa siku waliweka simu kwa masaa 15 kwa miaka 6 ilipimwa na kubaini kwamba, wale watu waliokua wakiweka simu viunoni uzito( density) wa madini ulikua mdogo sana na walisumbuliwa na matatizo ya mifupa( OSTEOPOROSIS) kuliko watu ambao walikua hawaweki simu viunoni.

KWA UFUPI , SIMU INAPOKUA MWILINI AU KARIBU NA MWILI SEHEMU YOYOTE ILE CHINI YA INCHI 6-8, KUNA MADHARA. MADHARA UTOFAUTIANA SEHEMU MOJA NA NYINGINE. EPUKA JAMBO HILI.


MATUMIZI SAHIHI KWA AFYA YAKO NA JAMII

· Tumia mara nyingi ujumbe mfupi kuliko kuongea

· Kama simu haina matumizi, izime na iweke mbali nawe

· Muda wa kulala, zima simu na vifaa vyote vya kielektroniki na ikiwezekana viweke chumba tofauti na unacholala.

· Tumia simu za mezani, kwani usalama ni bora, kuliko za mikononi

· Tumia vifaa kama headphone au earphone maalum. Ambazo zimewekewa ulinzi wa mionzi. Zingatia, vifaa hivi mara nyingi ni hatari kama havina ulinzi wa mionzi katika nyaya zake, maana zinakusanya mionzi na kuisogeza karibu kabisa na ubongo wako.

· Nunua kifaa maalum cha kubebea simu na sio kuibeba mwilini mwako

· Soma taratibu sahihi za kiafya kwenye simu yako, mara nyingi ziko katika setting ya simu.

· Funga vifaa vya kuchuja mionzi katika eneo lako.

· Tumia simu yako kwa ajili ya kuongea endapo tuu, mtandao umejaa, yaani, BARS zipo zote za mtandao. Kwani simu inatumia power kubwa sana kufanya mawasiliano pale ambapo bar iko chini na nguvu hii usababisha mionzi kuwa mingi na madhara yake uongezeka.

· Zuia watoto wako kutumia simu, walau baada ya miaka 15( inawezekana, kama kweli unamtakia future njema).

· Tumia simu zile za zamani, zitumiazo 900 MHZ, simu hizi mara nyingi hazitoi mionzi kama hazitumiki pia mionzi yake iko chini.

· Epuka sana vitu vinavyoitwa “ WIRELESS”, jitahidi kutumia vifaa ambavyo ni wired.



“KUMBUKA, HAKUNA MIONZI MIZURI WALA MIBAYA. MONZI YOTE MIBAYA”


NAJUA

MAKAMPUNI YAFANYAYO BIASHARA HII HAYAWEZI FURAHIA JAMBO KAMA HILI, ELIMU KAMA HII NA HATA IVYO, WAO SIO WAKWANZA KUFANYA IVYO. YAPO MAKAMPNI MENGI SANA YAMEPINGA TAFITI HIZI, YAMEKUJA NA TAFITI ZAO WAO WENYEWE NA KUONESHA MADHARA NI NADRA SANA, LAKINI, NDUGU, CHEZA SALAMA.

Mfano

clip_image042.jpg


clip_image044.jpg



“ WATAIFAHAMU KWELI, NAYO KWELI, ITAWAWEKA HURU”

MBARIKIWE.

Clio odhiambO

odhiamboclion@gmail.com
 
Asante kwa ufafanuz juu ya matumizi ya simu japo na mimi ni mtumiaji wa simu hasa kuongea lakni leo nimepata mwanga mzuri. Mungu akubariki ndugu.
 
Lile zoezi la TCRA la kukagua na kuzizima simu fake liliishia wapi? Kwanini taasisi zetu zinafanya kazi kwa hisia na mihemko?
Lile zoezi lilitakiwa liwe endelevu, simu original zina madhara lakini sio makubwa sana kama hizi fake. Hata ufanisi kwenye matumizi pia ni wa kiwango cha juu.
 
Simu ina madhara sana ila serikali za dunia hawataki kusema maana uchumi wa dunia unategemea sana technolgy....
Simu kwa sasa ni kama sigara miaka ya 1950's ilichukua muda kukiri sigara ina madhara mpaka walipopata mbadala wa sigara kiuchumi...
 
Simu ina madhara sana ila serikali za dunia hawataki kusema maana uchumi wa dunia unategemea sana technolgy....
Simu kwa sasa ni kama sigara miaka ya 1950's ilichukua muda kukiri sigara ina madhara mpaka walipopata mbadala wa sigara kiuchumi...

Ndugu mhandisi,
Tunasomeshwa kwa fedha nyingi sana, tunatumia miaka mingi sana kupata elimu hizi lakini, tunapangiwa cha kutenda na kusema na wasio na taaluma na hakika wana nguvu sana. Ndiyo dunia ya leo ambayo taaluma imebaki ndani ya bahasha.
 
Last night, a fellow editor emailed me a link to yet another study purporting to show that cellphone use could be associated with cancer. This one was worth looking at in more detail, however, because it purported to see an increase in a specific cancer—the same type of cancer that was increased in a problematic US government study.

A quick glance at the study identified significant issues with its primary conclusion. Normally, at this point, the decision would be to skip coverage unless the study picked up unwarranted attention from the rest of the media. (See: Scott Kelly's DNA). But in this case, we thought we'd describe how we went about evaluating the paper, since it could help more people identify similar issues in the future.

Background checks

The first step in evaluating a scientific paper is to get ahold of a copy of the paper. Fortunately, this one has been placed online by an organization that consistently promotes the idea that cell phones create health risks. The Environmental Health Trust's involvement shouldn't be seen as a positive or a negative; they've promoted very low-quality material in the past, but the organization would undoubtedly promote higher quality studies if those agreed with its stance.

The study itself has been accepted for publication, which means it has been through peer review. It will appear in a journal called Environmental Research, but journal quality matters. While lots of research that ends up being published in lower-profile journals ends up being significant, the rise of online journals has spawned a host of predatory publishers that will publish anything as long as the authors pay them a publication fee.

Advertisement
Environmental Research isn't one of those; it's published by Elsevier, a large publishing house that has been handling science journals for decades. And this particular journal has been around since the 1960s. A journal's "impact factor" is an imperfect measurement of whether the articles it publishes end up influencing other research. Environmental Research's score is typical of a decent-quality journal that serves a specialized audience.

All of this suggests that this cellphone paper probably went through some decent peer review, so it shouldn't be dismissed out of hand.

Next when in the evaluating process, we typically give the author list a quick look. Something that is a bit unusual here is that every author comes from the same institution, Italy's Instituto Ramazzini. Typically, an author list this large involves a collaboration among several research centers, but this makes it relatively easy to check into the Ramazzini's background. It turns out the Institute is widely recognized for its cancer studies, and it has been doing them for decades. There has been some controversy about some of the organization's conclusions and arguments in Congress over whether US government funds should be going to a foreign institution. But in at least one situation, outside experts were called in by the US government, and they found that at least some of the Ramazzini's work was scientifically valid.

Adding all of this up, this looks like a paper that should be taken seriously. So that's what we'll do.

Stats vs. numbers

Like other studies of its kind, this new research involves long-term exposure of rats to cellphone signals. Like the US government study, it involves unusually long exposures (19 hours a day), but it uses much lower doses, ones similar to what someone might actually experience. It uses a very large number of animals (nearly 2,500 in total), which should provide good statistical power. So far, so good.

But things start to go wrong in the abstract. There, the authors of the paper talk about three increases in the incidence of cancer in animals exposed to cellphone radiation. But two of these weren't statistically significant, meaning there's a greater than five percent chance the difference would occur at random. If we're going to allow non-significant changes into the conclusions, then the data would just as easily support reporting that cellphones reduce the risk of cancer in some of the experimental groups.

That's bad. But there's still one significant increase in cancer in their data, so let's look more closely at that: "A statistically significant increase in the incidence of heart Schwannomas was observed in treated male rats at the highest dose." When it comes to this type of cancer, the control group of 817 rats developed four tumors. But critically, all of those tumors occurred in females; none in males. This apparent sex bias will necessarily exaggerate the impact of any tumors in any of the male experimental populations.

And that's exactly what you see happening. In one female population, 2.2 percent of an experimental group developed this type of tumor, but that was not a statistically significant result. By contrast, in this male population with the significant difference, only 1.5 percent of the animals developed these tumors. A low-dose group of males had the same number of tumors, but the group was larger and so the result slipped below significance.

These numbers suggest that the one statistical effect seen in this study is caused by the unusually low tumor incidence in the control group, rather than a specific effect of cellphone radiation.

As we mentioned above, the normal response to a study like this would be to simply ignore it unless it became widely discussed. But highlighting the process that we use to decide to ignore it should give you a sense of how we determine what to cover when it comes to scientific studies at Ars. And, if you decide to try this method at home, it can also help you determine which results to pay attention to

source:arstechnica.com
 
Back
Top Bottom